PICHA KWA HISANI YA https://globalpublishers.co.tz
DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa
Jamii Media Limited na Mwanzilishi wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence
Melo, leo Desemba 19, 2016 ameachiliwa kwa dhamana na Mahakama Hakimu
Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya kukaa lupango kwa takribani
siku 7.
Melo ambaye anakabiliwa na
mashtaka matatu likiwemo la kuendesha tovuti ambayo haijasajiliwa
nchini, amedhaminiwa na wadhamini wawili ambao ni Judith Kapinga na
Kiiya Joel Kiiya, wote wawili wametakiwa kuweka bondi ya Tsh. Milioni 5
kila mmoja ili wamdhamini jambo amabalo wametekeleza.
Mbali
kuweka bondi hiyo, wadhamini hao pia walitakiwa kuambatanisha na kuacha
mahakamani hapo barua za utambulisho wa kazi na mahali wanapofanyia
kazi jambo ambalo pia walitekeleza.
Baada ya kupata dhamana, kesi hiyo Melo itatajwa tena Desemba 29 mwaka huu.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana,
Melo aliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena,
Posta jijini hapa ambapo mbali na mambo mengine, amewashukuru waandishi
wa habari kwa jinsi walivyokuwa wakiripoti suala la kesi yake, na
kuwataka wasiogope kutoa taarifa au kuwasilisha mawazo yao kwenye vyombo
vya habari na kuongeza kuwa hatakuwa na mengi ya kuzungumza kwa sababu
tayari suala hilo lipo mahakamani.
No comments :
Post a Comment