Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali
katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na
Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam
leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizindua Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi
na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar
es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina
Chuwa akiongea na wadau mbalimbali katika Uzinduzi wa Matokeo ya
Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka
2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Sylivia
Meku akielezea kwa wadau wa afya Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na
Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es
Salaam leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dr. Albina Chuwa kabla ya uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa
Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16
Tanzania jijini Dar es Salaam leo, katikati ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Mohamed Ally.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja wadau mbalimbali
wa Takwimu na Afya katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya
Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini
Dar es Salaam leo. Picha na Benjamin Sawe- Maelezo
SERIKALI imezindua ripoti ya
utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria ya mwaka
2015/16 mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni awamu ya tatu
katika ugonjwa wa malaria ambapo ripoti imeonesha kupungua kwa vifo vya
watoto wadogo...
Akizungumza katika uzinduzi huo
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu
kwa kuaanda ripoti iliyoonesha Taifa kupiga hatua katika utoaji wa
huduma ya mama na mtoto.
Waziri Ummy ameeleza kuwa ripoti
hiyo itaisaidia Wizara ya Afya na serikali kwa ujumla katika kutathmini
na kufuatilia utekelezaji wa mipango endelevu katika huduma za afya hapa
nchini ili kuboresha utoaji wa huduma ambazo ripoti imeonesha
haikufanya vizuri kutokana na changamoto mbalimbali ambazo ripoti
imezibainisha.
“Ripoti hii imeonesha kuwa bado
kuna changamoto katika mimba za utotoni kwani zimeongezeka
ukilinganisha na mwaka 2010 ambapo watoto 23 kati ya mia moja walipata
mimba wakiwa na umri mdogo ukilinganisha na sasa watoto 27 kati ya mia
moja hupata mimba katika umri mdogo hivyo kuna haja ya jamii kuelimishwa
juu ya madhara ya mimba za utotoni”, alisema Waziri Ummy.
Aliongeza kuwa kuna haja ya
serikali kuangalia upya sheria ya kuruhusu mwanafunzi kuendelea na
masomo endapo akipata mimba akiwa shuleni kwani kumzuia kuendelea na
masomo ni kupoteza nguvu kazi ya taifa na kuikwamisha serikali kufikia
malengo yake ya uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa iwapo huduma
za afya zitaboreshwa zitapelekea ukuaji wa uchumi kwasababu ya uwepo wa
nguvu kazi ya uhakika na kuongeza uzalishaji kwa Taifa.
“Wananchi wakiwa hawana afya ya
kutosha na kuugua mara kwa mara uchumi wa nchi yoyote Duniani hupungua
kasi ya ukuaji kwa kuwa rasilimali fedha ambazo zingeelekezwa kukuza
sekta nyingine hupungua na hata nguvu kazi kupungua” alisema Dkt. Chuwa.
Aidha Dkt. Chuwa aliongeza kuwa
kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 inatamka kuwa yeyote
atakaepotosha Takwimu hizi kwa makusudi atachukuliwa hatua za kisheria
kupitia kifungu cha 37 cha sheria hiyo.
Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto
wa mwaka 1991-92 ulionyesha kuwa katika kila watoto 1000 wanaozaliwa
hai, watoto 141 walikuwa wakifariki kabla ya kufikia umri wa miaka
mitano ila utafiti huu umebaini kuwa ni watoto 67tu ndiyo wanaofariki
kati ya watoto 1000.
No comments :
Post a Comment