Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto) akipata
maelezo ya ramani ya Ujenzi wa Daraja la Kilombero kutoka kwa Mkandarasi
wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania. Daraja hilo lipo
katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto) akipata
maelezo Ujenzi wa Daraja la Kilombero kutoka kwa Mkandarasi wa kampuni
ya Rv associates India& AES Tanzania. Daraja hilo lipo katika
barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (aliyenyoosha kidole) akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES
Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja hilo lipo katika
barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa pili kulia), akiendelea na
ukaguzi wa sehemu ya juu ya daraja la Kilombero.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Mbele) akitoa akisisitiza jambo
kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania
anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya
Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa tatu kushoto) akifafanua
jambo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES
Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero.Daraja hilo lipo katika barabara
kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa tatu kulia) akijadiliana
jambo na Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania
anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya
Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Muonekano wa Daraja la Kilombero
lenye urefu wa Mita 384 ambapo ujenzi wake unaendelea, Daraja hilo lipo
katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
……………..
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amemuagiza Mkandarasi wa kampuni
ya Rv associates India & AES Tanzania anayejenga daraja la
Kilombero lenye urefu wa mita 384 kukamilisha ujenzi huo mapema ifikapo
januari mwakani ili daraja hilo lianze kutumiwa na wananchi wa Mkoa wa
Morogoro.
Mhandisi Ngonyani ametoa agizo
mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa
mita 384 linalounganisha barabara kuu ya Ifakara –Mahenge mkoni
Morogoro.
“Wananchi wa Ifakara wanahamu ya
kuona daraja hili linakamilika na kuanza kutumika mapema, hivyo ongezeni
kasi ya ujenzi wa daraja hili ili likamilike haraka na kwa ubora
uliokusudiwa ili liweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu”. amesisitiza
Mhandisi Ngonyani.
Ameongeza kuwa kukamilka kwa
daraja hilo kutawafanya wananchi kuachana na usafiri wa kutumia kivuko
cha Mv. Kilombero ambacho wakati wa mvua kubwa hushindwa kutoa huduma za
usafiri kwa wananchi hao na hivyo kukwamisha shughuli zao za
kimaendeleo.
Katika hatua nyingine Mhandisi
Ngonyani amekagua barabara ya kuu ya kitaifa (Trunk roads) ya kutoka
Mikumi-Mahenge, Kilosa kwa mpepo-Londo ambopo amesema kuwa Serikali
itaanza ujenzi wa barabara ya Kidatu –Ifakara(KM 67) kwa kiwango cha
lami ifikapo machi mwakani wakati barabara ya Lupilo hadi Lumecha
upembuzi yakinifu unaendelea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
halmashauri ya mji Ifakara Bw. Mashaka Mbilinyi ameelezea umuhimu wa
barabara hiyo kuwa itakuwa kichocheo cha mendeleo ya kiuchumi kwa
majimbo manne ya Mlimba, Malinyi, Ulanga na Kilombero.
“Barabara hii itakapokamilika
itawawezesha wananchi kupata huduma katika sehemu mbalimbali za majimbo
yetu na pia kusafirisha kusafirisha mizigo ya nafaka kwenda katika
masoko mbalimbali na hivyo kukuza kipato cha mwananchi na taifa kwa
ujumla”. amesema Bw. Mbilinyi.
Naye Mbunge wa Jimmbo la Mlimba
Mhe. Suzani Kiwanga na Mbunge wa Kilombero Mhe. Peter Lijuakali kwa
pamoja wameishukuru Serikali na kusema kuwa ujenzi wa barabara hiyo
itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kanda ya Kusini kwa vile itaunganisha
Kilombero, Malinyi na Ulanga na Mkoa wa Ruvuma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya
kukagua Miundombinu ya barabara, Madaraja na Reli.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments :
Post a Comment