Meneja
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Meshack Bandawe, akizungumza kwenye
mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu na michezo ya kuigiza mkoani
Mara.
Mafunzo
hayo yalanza Disemba 14 na yanafikia tamati leo Disemba 16, 2016 katika
ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Musoma. Yameandaliwa na Bodi ya
Filamu nchini ili kuwajengea uwezo wadau wa filamu ili kuzalisha kazi
zenye ubora.
#BMGHabari
Wadau
wa filamu mkoani Mara wakimsikiliza Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa,
Meshack Bandawe, wakati akiwaeleza umuhimu wa kujiunga na mfuko huo
Afisa Masoko PPF, Evance Baguma, akiwasilisha mada kwa wadau wa filamu na maigizo mkoani Mara
Wadau wa filamu mkoani Mara wakifuatilia mada kutoka kwa Afisa Masoko PPF, Evance Baguma
Wadau
wa filamu na maigizo mkoani Mara wamefurahishwa na mada kuhusu mifuko
ya hifadhi ya jamii kutoka PPF na kuonesha mwitiko mkubwa wa kujiunga na
mfuko wa Pensheni wa PPF.
Mfuko
wa Pesheni wa PPF umesema umedhamiria kuhakikisha kwamba wananchi wengi
walio kwenye sekta zisizo rasmi ikiwemo wajasiriamali wananufaika na
mafao ya hifadhi za jamii kupitia huduma ya Wote Scheme.
Meneja
wa mfuko huo Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, ameyasema hayo Musoma
mkoani Mara, wakati akieleza umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo
mbele ya wadau wa filamu mkoani humo.
Amesema
wananchi wasio kwenye sekta rasmi wakiwemo wajasiriamali wanayo fursa
ya kujiunga na mfuko wa PPF na kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo
huduma za matibabu, mikopo ya elimu, maendeleo pamoja na mafao ya uzeeni
kwa kila mwanachama kuchangia shilingi elfu 20 kwa mwezi ambazo
mwanachama hulipa kadri awezavyo.
Naye
Afisa Masoko PPF, Evance Baguma, amesema lengo la mfuko huo kuanzisha
huduma ya Wote Scheme kwa wajasiriamali ni kuondoa dhama potofu kwa
baadhi ya wananchi kwamba anayeweza kunufaika na huduma za mifuko ya
hifadhi za jamii ni lazima awe mtumishi wa taasisi binafsi ama serikali.
Wadau
wengi wa filamu mkoani Mara wamefurahishwa na ufafanuzi wa mfuko huo
ambapo wamebainisha kwamba awali walikosa fursa mbalimbali za mifuko ya
hifadhi za jamii ikiwemo PPF kutokana ufahamu duni waliokuwa nao.
Tazama picha zaidi HAPA
No comments :
Post a Comment