Tuesday, December 6, 2016

MAJALIWA ATAKA PEMBE ZA FARU ALIYEKUFA 2015 ZIPELEKWE OFISINI KWAKE KESHO DESEMBA 8



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenye ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo Desemba 6, 2016. Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa hifadhi ya Ngorongoro kupeleka pembe za faru aliyekufa kwa maradhi mwaka 2015 zipelekwe ofisini kwake Desemba 8, ni baada ya kugundua hujuma za kumuhamisha faru huyo kumpeleka kwenye hoteli ya kitalii kwenye hifadhi moja ya hifadhi za taifa.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Baadhi ya watumishi wa Mamlka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo Desemba 6, 2016



Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu wawili wa JWTZ kuwa Meja Jenerali kuanzia tarehe 03 Disemba 2016.Maafisa Wakuu hao ni;
Brigedia Jenerali George William Ingram ambaye ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga, (pichani kulia), na Brigedia Jenerali Michael Wambura Isamuhyo, (pichani kushoto),  ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.

Taarifa ya Makao Makuu ya JWTZ iliyotolewa jana Desemba 6 imesema, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Adolf Mwamunyange kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu anawapongeza na kuwatakia kheri katika vyeo vyao vipya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.

No comments :

Post a Comment