Na mahmoud Ahmad Arusha
MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha,
imetoa muda wa siku kumi kwa upande wa utetezi wa kesi ya kumyima
dhamana mbunge waArusha, Godbless Lema, kuwasilisha kusudio la kuomba
kuongezewa muda wa kukata rufaa ili aweze kupewadhamana.
Uamuzi huo umetolewa leo na jaji Dakta Modesta Opiyo wakati akiamua hatima ya mbune huyo kupata dhamana au la
Jaji Opiyo amesema hoja za Upande wa serikali zilizowasilishwa na
Wakili Hashim Ngole za kudai waleta maombi hayo walikuwa wazembe na walichelewa siku nne kuwasilisha Notisi baada ya rufaa yao kuondolewa na Jaji Fatuma Masengi Desemba 2 hazina mashiko.
Jaji Opiyo, amesema siku nne zinazolalamikiwa kuwa
walichelewa kutoa maombi hayo, mahakama inaona hoja hizo hazina mashiko
sababu siku mbili kati ya hizo zilikuwa siku za mapumziko jumamosi na
Jumapili, hivyo walitumia siku mbili kuandaa nyaraka na kupeleka maombi
hayo.Wakili Hashim Ngole za kudai waleta maombi hayo walikuwa wazembe na walichelewa siku nne kuwasilisha Notisi baada ya rufaa yao kuondolewa na Jaji Fatuma Masengi Desemba 2 hazina mashiko.
Akiwasilisha hoja za maombi ya
kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi hiyo ili rufaa hiyo iweze
kusikilizwa Wakili Mfinanga alidai
mahakamani hapo kuwa maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo chini ya kifungu 361(2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Alidai kuwa maamuzi wanayotarajia kukatia rufaa ni uamuzi uliotolewa
Novemba 11 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hakimu Desderi Kamugisha, ambapo Lema anakabiliwa na kesi namba 440 na 441 za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

No comments :
Post a Comment