Tanga, WANAFUNZI wa Vilabu vya
Umoja wa Mataifa kutoka vyuo Vikuu na Shule za Sekondari na Msingi
kutoka Mikoa mbalimbali nchini wamekutana Tanga kujadili mambo mbali
mbali yahusuyo shughuli za Umoja wa Mataifa.
Wanafunzi hao walijadili mambo
hayo yakiwemo Demokrasia na Utawala bora Barani Afrika pamoja na
changamoto za Raia katika nchi zenye machafuko.
Pia walijadili uchafuzi wa
mazingira kwa nchi zenye viwanda na uharibifu wa mazingira ya bahari kwa
baadhi ya viwanda kumwaga sumu baharini.
Akizungumza katika kongamano hilo,
Mlezi wa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransiss Shelutete, amezitaka
Serikali nchi za Afrika kuwachukulia hatua kali uchafuzi wa mazingira .
Wanachama wa vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakifuatilia kongamano lililohusisha wanafunzi wa vyuoni na Shule za Sekondari na Msingi na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga
Mratibu wa klabu ya Umoja wa Mataifa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransisis Shelutete, akizungumza kwenye kongamano la Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka Mikoa mbalimbali nchini na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga
Blog ya kijamii tangakumekuchablog 0655 902929
No comments :
Post a Comment