Kampuni moja ya simu imetambulisha
karatasi laini za chooni 'toilet paper' za kufutia simu za kisasa
smartphone kwenye vyoo vya Uwanja wa Kimataifa wa Narita Jijini Tokyo
nchini Japan.
Vyoo katika uwanja huo vimewekewa
karatasi hizo laini za kufutia simu, ambazo mtumiaji akiingia chooni
anaweza kuchukua kufuta kioo cha simu yake ili kuua vijidudu.
Gharama za toilet paper za simu,
zimegharamiwa na kampuni kubwa ya simu ya NTT Docomo, ambapo karatasi
hizo pia zinataarifa za maeneo ya kupata Wi-Fi na app ya wasafiri.
No comments :
Post a Comment