George Michael Mtaalam kutoka
kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus
akionyesha moja ya kifaa cha kuzima moto kinachoweza kufungwa katika
mitambo mbalimbali chenye uwezo wa kuzima moto katika
hatua za awali kabisa kabla ya kuwa mkubwa wakati alipokuwa akielezea
ubora wa vifaa hivyo katika kupambana na majanga ya moto kwenye uzinduzi
ulifanyika Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishono mwa
wiki.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza
George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima
moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa
hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi
uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, wa
pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Junaco Group Campanies na wa tatu ni Fikili S. Salla Kamishna wa
Divisheni ya Usalama dhidi ya moto Jeshi la Zimamoto.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza
George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima
moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa
hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi
uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, wa
pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Junaco Group Campanies
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza
George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima
moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa
hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi
uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam , wa
pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Junaco Group
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimpongeza George
Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto
FirePro ya Cyprus mara baada ya kumaliza kutoa maelezo yake mbele ya
wageni waalikwa wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi
Oysterbay jijini Dar es salaam, katikati ni Justin Lambert Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
Biashara wa Kampuni ya JUNACO Group Of Companies Limited Bw. Anic
Kashashaakizungimza katika uzinduzi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa
uzinduzi wa kifaa hicho cha Firepro mwishoni mwa wiki.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya , Justin Lambert Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na George Michael
Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya
Cyprus wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo

……………………………………………………………………..
Kampuni ya JUNACO Group of
Companies mwishoni mwa wiki ilizindua kifaa cha kisasa kinachotumika
kuzima moto kwenye makazi ya watu na mitambo kinachofahamika kama
‘FirePro’ ikiwa ni uvumbuzi unaolenga kukabiliana na janga hilo hatari.
Akizungumza wakati wa hafla
maalum ya uzinduzi wa kifaa hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki na kuhuduriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mambao ya Ndani Balozi Hassani Simba Yahya, Mwenyekiti na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo ya nchini hapa nchini , Bw Justine Lambert
alisema matumizi ya kifaa hicho miongoni mwa watanzania yatasaidia
kutaondoa athari za uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo na majanga ya
moto kwenye makazi ya watu.
“Uvumbuzi na ujio wa kifaa hiki
ni ishara kwamba athari zitokazo na majanga ya moto ambayo yamekuwa
yakiripotiwa kupoteza maisha ya watanzania na kusababisha umasikini
kutoka na uharibifu wa mali sasa linakwenda kwisha,’’ alisema Bw Lambert
huku akiongeza kuwa wao kama sekta binafsi wana wajibu wa kuisaidia
serikali kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi wake.
Alisema mbali na suala la
kuhakikisha usalama wa watanzania, uwepo wa kifaa hicho pia utaongeza
ajira kwa wadau wote watakaohusika kwa namna moja au nyingine katika
mauzo ya kifaa hicho hapa nchini.
“ Ndani ya miaka minne ijayo
Junaco Group of Companies tunarajia kutengeneza ajira zipatazo 780
zitakazohusisha wauzaji, wasambazaji na wataalamu wa kufunga kifaa hiki
kote nchini,’’ alisema.
Kwa upande wake balozi Simba
ambae alimuwakilisha waziri wa wizara hiyo Bw Mwigulu Nchemba alisema
serikali imekuwa ikiridhishwa sana hasa pale inapopokea taarifa za uwepo
wa teknolojia mpya zinazolenga kutatua changamoto zinazowakibili
wananchi wake kuisalama kama hiyo ya uzinduzi wa kifaa cha ‘FirePro’
huku akitoa wito kwa kampuni hiyo kutumia fursa za kiuwekezaji kuanzisha
kiwanda cha kutengeneza vifaa kama hivyo hapa nchini.
“Ujio wa kifaa hiki hapa nchini
ni wazi kuwa utakuwa na matokeo chanya kijamii na kiuchumi kwasababu
mbali na kulinda usalama wa wananchi na mali zao lakini pia utazalisha
ajira zaidi ya 800… hongereni sana naimani mtafikiria pia kuanzisha
kiwanda kitakachowezesha uzalishaji wa vifaa hivi hapa nchini,’’
alisema.
Kwa mujibu wa Meneja Maendeleo wa
Mradi huo Bw, George Michael, teknolijia iliyotumika kutengeza kifaa
hicho ni bora zaidi kwa nchi zinazoendelea na ni rafiki pia kwa
mazingira.
No comments :
Post a Comment