Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akizungumza na Viongozi wa
Bandari ya Dar es salaam mara baada ya kuwasili Bandarini hapo kwaajiri
ya kufanya ziara.
………………..
NA EVELYN MKOKOI – DAR ES SALAAM
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mzingira Mhe. Luhaga Mpina amefanya ziara ya kushtukiza
katika bandari ya Dar es salaam ili kujionea utaratibu wa Bandari hiyo
wa kuondosha taka zitokanazo na shughuli zake.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina
imetokana na Malalamiko ya wananchi yaliyodai kuwa uchafuzi mwingi
umekuwa ukifanyika katika Bahari na sehemu kubwa ya fukwe ya bandari
imekuwa ikijaa taka za aina mbali mbali.
Kutokana na malalamiko hayo ya
wakazi wa jiji la Dar es Saalam, Naibu Waziri kabla ya kukagua maeneo ya
kutoa na kukusanya taka za aina mbali mbali katika bandari hiyo
zikiwemo taka za mafuta ghafi, alipokea taarifa kutoka kwa uongozi wa
Bandari ambapo ameshangazwa na kile kilicholezwa na Afisa Mazingira wa
bandari Bwana Thobias Sonda kuwa Bandani hiyo kubwa katika kanda ya
Afrika Mashariki haina sehemu ya kupokea taka yaani waste reception facility na haina takwimu za taka zinazoingia na kutoka Bandarini Hapo.
Akishindwa kujibu Baadhi ya
Maswali yaliyoulizwa na Naibu Waziri Mpina Afisa mazingira huyo alieleza
kuwa, Bandari hiyo inazalisha aina mbili kubwa za taka ikiwa ni taka za
aina mbali mbali na taka za maji taka, alisema kuwa taka hizo
zinaondoshwa na wakala ambao wanasajiliwa na Sumatra lakini
haikueleweka wazi kuwa, taka hizo zinatupwa wapi na aliongeza kwa kusema
kuwa, taka nyingi na hali ya uchafu inayoonekana pembezoni mwa Bandari
ya Dar es Salaam inatokana na shughuli za kibinadamu kiwandani hapo, na
kusema kuwa, kuna utaratibu wa kufanya usafi na kuziondosha na kukanusha
kuwepo kwa taarifa za boat na meli zinazofanya safari za kuanzia bandarini hapo kuchafua mazingira ya bandari na Bahari.
Afisa Mazingira huyo, liongeza kwa
kusema kuwa taka za maji taka pamoja na kukosekana kwa takwimu za
uondoshwani na umwagaji, zimekuwa zikikuswanywa a magari yao maalumu na
kumwagwa katika mabwawa yao yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kwa kushangwazwa na hali hiyo,
Mpina kupitia Baraza la taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC
ameutaka uongozi wa Bandari hiyo kujenga mfumo mzuri wa kuhifadhi taka
kwa muda wa miezi sita na kuripoti kwa Baraza za Mazingira kwa miezi
mitatu Mfulizo kuonyesha namna ambavyo uondoshaji wa taka hizo
unafanyika, Pamoja na kuwasilisha ripoti kwa Baraza ya Namna ambavyo
mawakala hao walipatikana.
Aidha Naibu waziri Mpina
ameliagiza baraza kumpelekea ripoti ndani ya siku saba, inayoonyesha
kama hao mawakala wa kukusanya taka bandarini wapo kisheria.
Kwa Upande wake Kaimu Meneja wa
Mamlaka ya Bandari Nchini Bw. Nelson Mlele amesema kuwa amepokea maagizo
ya Mhe kupitia NEMC kwani yanawakumbusha utekelezaji wa majukumu yao na
kwa upande wa Bandari ni changamoto itakayofanyiwa kazi haraka.;
No comments :
Post a Comment