Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwapungia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wakati akiwasili tayari kuhutubia wakazi wa kijiji hicho. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwasili Nansio wilayani Ukerewe kwa meli ya MV. Nyehunge II
ambapo alikuwa na kazi za kuweka jiwe la msinggi kwenye mradi wa maji wa
Nebuye pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chumba cha
Upasuaji kituo cha Afya Kagunguli na kuhutubia wananchi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwapungia wananchi wa Nansio wilayani Ukerewe waliojitokeza
kumpokea ambapo aliwasili kutokea Mwanza mjini kwa meli ya MV. Nyehunge
II
ambapo alikuwa na kazi za kuweka jiwe la msinggi kwenye mradi wa maji wa
Nebuye pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chumba cha
Upasuaji kituo cha Afya Kagunguli na kuhutubia wananchi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiambatana
na viongozi mbali mbali katika kukagua mradi mkubwa wa maji wa Nebuye
wilayani Ukerewe mkoa wa Mwaza
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakazi wa kijiji cha Nebuye ambapo aliwasihi kuutunza mradi
wa maji na mazingira kwa ujumla wakati wa kuweka jiwe la msingi katika
mradi wa maji ya Nebuye wilayani Ukerewe mkoa wa Mwaza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisoma
maandishi yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la mradi mkubwa wa maji wa
Nebuye wilayani Ukerewe mkoa wa Mwaza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
akiwapungia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wakati akiwasili tayari
kuhutubia wakazi wa kijiji hicho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akihutubia
wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe na kusisitiza serikali
ya awamu ya tano ni ya kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya
Tanzania.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasalimia
wakazi wa Nansio waliojitokeza kwa wingi kutaka kumsalimia na kuwakilisha kero
zao wakati wa ziara yake katika wilaya ya Ukerewe
..................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la
msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye mji Nansio katika kisiwa cha Ukerewe
mkoani Mwanza mradi ambao utahudumia wananchi elfu 61.
Makamu wa
Rais ambaye amesafiri kwa takribani masaa Matatu na meli ya MV Nyehunge II katika
Ziwa Victoria kwenda kisiwa Ukerewe kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa
huo,amewahimiza wananchi hao wautunze mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi
kikubwa kuondoa tatizo na uhaba wa maji safi na salama katika kisiwa hicho.
Mradi huo ambao
unaojumuisha kazi za uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unatekelezwa
chini ya umefadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania katika miji ya Sengerema,Geita na
Nansio – Ukerewe kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 30.4 ambapo serikali
ya Tanzania imechangia mradi huo Dola za Kimarekani milioni nne.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amewaahidi wananchi kuwa serikali ya awamu ya Tano unamikakati
mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia
muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu
mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa
vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Afisa
wa IRI, Tony Alfred akizungumza jambo wakakati wa mafunzo ya mchakato
wa mabadiliko ya Katiba kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Chamwino wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba.
Katibu Mtendaji wa TYVA Saddam Khalfan akitoa ufafanuzi kuhusu shirika hilo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu
mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na changamoto zake kwa vijana wa
wilaya ya Tanga Mjini mkoani Tanga.
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Kijana
mwenye ulemavu wa ngozi akisoma katiba ya Tanzania kwa makini sana
wakati wa mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika
Mjini Tanga.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo yaliyofanyika Tanga wakifuatilia mada
Na Mwandishi Wetu
Asasi
Ya Vijana, Tanzania Youth Vision Association kwa Kushirikiana Na
International Republican Institute zimetoa mafunzo ya kuboresha Uwezo wa
Vijana kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini katika Mikoa
mitatu ilijumuisha Wilaya Nne, ikiwemo Kinondoni, Dodoma Mjini, Chamwino
Na Tanga Mjini.
Mafunzo hayo yameweza kufikia vijana 500 kwa njia ya Warsha na Vijana aa wananchi zaidi ya 100,000 kupitia mitandao ya kijamii.
Lengo
kuu la Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na ushiriki wa Vijana katika
mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Katika ufunguzi wa mafunzo hayo,
Katibu Mtendaji wa TYVA ndugu Saddam Khalfan alisema, TYVA inaamini
Katiba ni Sheria mama na mwongozo ambao una uhusiano wa moja kwa moja na
maisha yetu ya kila siku.
Alibainisha
watu wengi wamekua wakisoma au kuisikia Katiba, na wengine wakidhani
Katiba ni maalumu kwa ajili ya wanasheria au wasomi tu. Kuna uhusiano
mkubwa kati ya Katiba bora ya Nchi, Demokrasia na Maendeleo ya Jamii.
Mwanaharakati
Na Mtetezi wa HAKI za Binadamu ndugu Deus Kibamba alipata kuwaelezea
washiriki wa mafunzo hayo historia ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba,
Ushiriki wa wananchi katika mchakato wa Katiba, hatua muhimu katika
Mchakato wa utengenezaji Katiba, Mambo ya Msingi yaliyomo katika Katiba
inayopendekezwa na Mambo muhimu kuelekea kura ya Maoni ya Katiba
Inayopendekezwa.
Alidokeza
pia, katika mchakato wa Katiba, hasa katika hatua ya Bunge la Katiba
ulikosa maridhiano ya Kitaifa. kuna haja ya kuwepo mkutano wa kitaifa
utajaowaleta wadau na jopo la wataalamu mbalimbali kwa ajili ya
kunyambua yale mambo yanayoendelea kuleta ukakasi linapaswa kufanyika.
Ndugu
Dickson Kamala ambaye ni Mtetezi wa HAKI za vijana na Makamu Mwenyekiti
Wa TYVA aliwasilisha mada ya umuhimu wa Vijana kushiriki na
kushirikiana katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili kupata Katiba
itayojali maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla.
Afisa
kutoka IRI, Tony Alfred aliwatarifu Vijana washiriki kusoma kuhusu
Katiba na wanaweza kupata habari na taarifa zaidi kuhusu Katiba kwa
kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutuma Neno "Katiba yetu" Kwenda
0684996494.
Afisa
Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la
‘The Foundation For Civil Society’ Nasim
Losai, akitoa mada wakati wa ufungaji wa Tamasha la Tano la Watu wenye
Ulemavu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo
Plaza jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limefungwa hii leo hayo.
Mkufunzi
Mwelekezi, Salma Maoulid, akisimamia zoezi la maswali na majibu wakati wa kufunga Tamasha la
Tano la Watu wenye Ulemavu lililoanza jana kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo
Plaza jijini Dar es Salaam.
Afisa Uchumi Mwandamizi, Mchambuzi na Mipango, Andrea Aloyce, akitoa
mada kwa washiriki wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemabu
lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini
Dar es Salaam.
Mshereheshaji akiendelea kuongoza Tamasha hilo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Governance & Economic Policy Centre, Moses
Kulaba, akitoa mada kwa washiriki wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu
wenye Ulemabu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl – Ubungo
Plaza jijini Dar es Salaam.
Mkarimani akiwatafsiria walemavu Viziwi kila kilichokuwa kikizungumzwa ukumbini hapo
Mshereheshaji
akiendelea kuwachangamsha washiriki, ''Abunuasi aliwauliza Je mnajua
lichowaitia?? wakajibu hapana, akwaambia basi kama hamjui basi rudini
nyumbani, wakaru, Siku yapili Je mnajua nilichowaitia?? wakajibu
Ndiyooo,akawaambi basi kama mnajua basi rudini nyumbani kwa sababu
mnajua ninachotaka kuzungumza nanyi, ikabidi waondoke, Siku ya Tatu
wakaja tena alipo wauliza Je mnajua nilichowaitia??? siku hiyo
wakakubaliana kujigawa wengine wakasema Ndiyoooo, na wengine wakajibu
Hapanaaaa, akawaambia basi sasa itabidi nyie mnaojua muwaambie hao
wasiojua kile ninachotaka kuzungumza, kisha mrudi nyumbani'' kila mmoja
akaguna na kuondoka mahala hapo kwa hasira....
Mshiriki akiongozwa kuingia ukumbini.
Waratibu wa Tamasha hilo wakiwa bize kuratibu yaliyokuwa yakiendelea
ukumbini hapo wakati wa kufunga Tamasha hilo.
Mshiriki akiuliza swali.
Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea
ukumbini hapo.
No comments :
Post a Comment