Monday, November 21, 2016

WAZIRI WA UTAMADUNI NA SANAA WA AFRIKA YA KUSINI ATEMBELEA MAZIMBU CAMPUS MKOANI MOROGORO NA KUTEMBELEA MAKABURI YA WAPIGANIA UHURU WA AFRIKA YA KUSINI



Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa (aliyenyoosha mkono) akiangalia moja ya makaburi ya waliopigania uhuru wa nchi yake yaliyopo Mazimbu Campus Mkoani Morogoro.

Mkurugenzi wa SUA Solomon Mazimbu Campus Prof.Yasinta Muzanila(kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(kushoto) kuhusu Mazimbu campus na kumbukumbu zilizopo  wakati Waziri huyo alipotembelea eneo hilo liliopo Mkoani Morogoro ambalo wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini walilitumia katika harakati za kupigania uhuru wao na ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla.



Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akisalimiana na Mkurugenzi wa SUA Solomon Mazimbu Campus Prof.Yasinta Muzanila alipowasili kutembelea eneo lililopo Mkoani Morogoro ambalo wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini walilitumia katika harakati za kupigania uhuru wao na ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla

Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiwa katika eneo lililowekwa sanamu ya Rais wa kwanza Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela kama ukumbusho wa wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini Mazimbu Mkoani Morogoro.


Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, ambapo aliwaasa wananchi kuchukua uamuzi wa  kupima afya zao na kupatiwa matibatu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dk. Hedwiga Swai. 

No comments :

Post a Comment