Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro
Marine Transport Bw. Salehe Songoro akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) ripoti ya ukaguzi
wa ujenzi wa meli mbili za mizigo katika bandari ya Itungi ziwa Nyasa.
Kaimu Meneja wa bandari ya
Itungi na Kiwira Eng. Juma Kisavara (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo
kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani
(katikati) kuhusu namna ya kuondoa mchanga katika kingo za ziwa Nyasa
ili kuwezesha meli zinazotengenezwa kuingizwa katika maji kwa urahisi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua Meli ya Mv. Njombe ambayo
ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipanda juu ya Meli ya Mv. Ruvuma
ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99 ili kuona mfumo wa injini
unavyofanya kazi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mfumo wa uendeshaji wa Meli
ya Mv. Njombe ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
Muonekano wa Meli za Mv. Njombe
na Mv.Ruvuma ambazo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, meli hizo
zipo katiaka hatua za majaribio kabla ya kuanza kutoa huduma.
Meneja wa Wakala wa barabara Mkoa
wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipokagua ujenzi wa
barabara ya Kikusya-Ipinda hadi Matema KM 34.6 ambayo inajengwa kwa
kiwango cha lami.
No comments :
Post a Comment