Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimjulia hali Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela aliyelazwa katika wodi ya Sewahaji
Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.Kwa taarifa zilizopo hali ya
Mhe. Shigela inaendelea vizuri.(PICHA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WHUSM)
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wenzao kutoka Taasisi ya Open Heart
International (OHI) ya Nchini Australia wakitoa huduma ya matibabu ya
moyo bila ya kupasua kifua (Catheterization) kwa mgonjwa, kwenye taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. (PICHA NA ANNA NKINDA-JKCI)
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wenzao kutoka Taasisi ya Open Heart
International (OHI) ya Nchini Australia wakitoa huduma ya matibabu ya
moyo bila ya kupasua kifua (Catheterization) kwa mgonjwa. Kushoto ni Afisa
Muuguzi Ayoub Mchau, akifuatiwa na Dkt. Daniel Maclennan na kulia ni Dkt. Peter
Kisenge.
Waziri
Mkuu, Kaasim Majaliwa akiteta na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo
Pinda wakati alipokwenda kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kumjulia hali
Mzee Xavery Kayanza Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Novemba
22, 2016. Mzee Pinda amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matibabu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati
alipokwenda kwenye hospitali ya Mkoa wa Dodoma kumjulia hali baba mzazi wa
Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Xavery Kayanza Pinda Novemba 22, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
baada ya kuwasili kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako alikwenda kumjulia
hali baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Xavery Kayanza Pinda Novemba 22,
2016. Kulia ni Paroko wa Kanisa Kuu Katoliki la Dodoma , Padri Wisi Onesmo na
wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya
Simu ya Tigo, Shavkat Berdiev (kulia), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kutangaza ofa
ya Krismas ya Smartphone. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William
Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imetangaza
kuzindua ofa mpya ya Tecno Y3+ Music Smartphone ambayo imejengewa
ndani yake zana kubwa ya kuchezesha ambayo inatoa nafasi ya
kutiririsha kupitia mtandao na hivyo kuwawezesha wateja kufurahia na kusherehekea na wapendwa wao wakati wa kipindi hiki cha kipekee kinachohusiana na Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
No comments :
Post a Comment