Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari akizungumza katika kongamano la siku tatu la wanachama wa Chama cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA) ambalo limeanza Leo jijini Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari akizumgumza katika mkutano huo leo.
…………………………………………………………
Mganga
Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari amewataka watoa huduma za afya
nchini kufanya kazi kwa bidii ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Profesa
Bakari ametoa kauli hiyo Leo wakati akifungua kongamano la siku tatu la
Chama cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA) ambalo linafanyika jijini Dar
es Salaam.
Mganga
Mkuu amewataka kuzingatia maadili ya kazi kwani serikali ya sasa
inawataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuongeza
uzalishaji na kutoa huduma bora katika maeneo yao ya kazi.
“Mnatakiwa
kuwa na nidhamu na kuwahudumia vizuri wagonjwa. Fanyeni kazi kwa bidii
kwani ndani ya nchi kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji,” amesema
Profesa Bakari.
Kongamano
hilo limewakutanisha wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Kilimanjaro Christian Medical Centre KCMC) na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
No comments :
Post a Comment