Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais mstaafu wa
awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye wakati wa utawala wake alifahamka
sana na watanzania kama “Mzee Rukhsa”, Ikulu jijini Dar es Salaam. (PICHA NA
IKULU)
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu
wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais
mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga amewataka maofisa
Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini kufanya kazi kwa uzalendo
ili Tanzania iweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) ifikapo
mwaka 2030 kama ilivyokusudiwa.
Kauli
hiyo aliitoa mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa warsha ya malengo
endelevu kwa maafisa hao kutoka kanda ya Ziwa ambayo imeandaliwa na
Wizara ya Fedha na Mipango .
Alisema
uhamasishaji kuhusu malengo haya ni matokeo ya Nchi wanachama wa Umoja
wa Mataifa kukamilisha utekelezaji wa Malengo ya Milenia yaliyokamilika
mwaka 2015.
Alisema
Mpango wa maendeleo endelevu utatekelezwa kati ya mwaka 2015 hadi 2030,
hivyo pia na unajulikana kama agenda 2030 na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa pia iliridhia utekelezaji
wa malengo hayo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Fedha na Mipango, Servus Sagday akielezea madhumuni ya
warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa
Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini iliyofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kufungua warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa
mikutano Hazina ndogo.
Alisema katika utekelezaji wa mpango huo lazima maafisa hao wawe na uzalendo kwa kufanya kazi kwa maadili.
“Bila
kubadili fikra zao malengo hayo hayataweza kufikiwa, tufanye kazi kwa
bidii ili ifikapo mwaka 2030 tuweze kujipima na kuweza
kushangilia kwa kufikia malengo ya maendeleo endelevu 17 ambayo yamejikita kwenye sekta mbalimbali,”alisema Mmbaga.
Alisema
changamoto iliyopo kwasasa ni namna ya kufikia malengo hayo, hivyo ni
lazima kuwa tayari kubadilika katika kufanya kazi na kutafsiri mambo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akifungua warsha
ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa
Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini inayoendelea katika ukumbi
wa mikutano Hazina ndogo mjini Dodoma chini ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
“Tutakuwa
tunavutana, tunaangushana na itatupotezea muda wa kufikia kwenye
malengo haya lakini kikubwa ni lazima tukubali malengo ni ya kwetu na
yapo kwa ajili yetu sisi wenyewe ili mwisho wa siku tuweze
kuyafikia,”alisema.
Aliwahimiza
kuwa na moyo wa uzalendo ili kufikia malengo hayo katika utatuzi wa
changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo miundombinu.
“Lazima
tutambue watumishi wa umma ni jeshi ambalo linatakiwa kupigana na
maadui wale ambao wanatuathiri kijamii na kiuchumi na tuna maadui watatu
ujinga, maradhi na umaskini, wakati wanapopigana na maadui waliopo
kwenye malengo hayo na sisi tuunganishe na hawa maadui watatu,”alisema.
Alisema
inawezekana ikapangwa mipango mbalimbali lakini kama hawatabadili fikra
zao na hawapo tayari kufanya kazi ili kufikia malengo hayo kazi itakuwa
ni ngumu.
Alibainisha
tayari miongozo ya bajeti imeshatumwa kwenye mikoa hivyo kwa mujibu wa
miongozo hiyo waangalie namna ya kupanga shughuli, miradi ambayo
itajikita kufikia maelngo endelevu 17 ya Kitaifa na kidunia.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) -Idara ya Uchumi, Dr. Wilhelm
Ngasamiaku akitoa mada kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) na
mchakato wake katika warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango
nchini inayoendelea katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo mjini Dodoma
chini ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkufunzi
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi, Dr. Joel
Silas akitoa mada kuhusu uhusiano wa Maendeleo Endelevu (SDG's) na
mpango wa maendeleo wa miaka mitano kwenye warsha ya siku tatu ya
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na
Maofisa Mipango nchini inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa
mikutano Hazina ndogo chini ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP).
Afisa
kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Eva Ruhago
akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha ya siku tatu ya Malengo ya
Maendeleo Endelevu (SDG's) inayoendelea katika ukumbi wa Hazina ndogo
mjini Dodoma chini ya ufadhili wa UNDP.
Pichani
juu na chini sehemu ya washiriki wakitoa maoni wakati wa majadiliano
katika warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa
Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini inayoendelea mjini
Dodoma katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo chini ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Pichani
juu na chini ni sehemu ya Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango
kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya Kagera, Kigoma, Mara,
Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza wanaoishiriki warsha hiyo ya siku
tatu yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi ili kutimiza
kaulimbiu ya Malengo hayo isemayo "Hakuna atakayeachwa nyuma" inayolenga
kujenga msingi wa malengo shirikishi yanayodhamiria kuleta maendeleo
chanya kwa wote.
Mgeni
rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga
(walioketi katikati) katika picha ya pamoja na Maofisa Maendeleo ya
Jamii na Maofisa Mipango kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya
Kagera, Kigoma, Mara, Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza wanaoshiriki
warsha hiyo ya siku tatu inayoendelea mjini Dodoma chini ufadhili wa
UNDP
November
25th is the International Day for the elimination of Violence against
women in the world. The 16 days up to December 10th the Human Rights Day
is a period of global activism dedicated to fight gender violence in
all settings.
UZIKWASA,
an organization based in Pangani, Tanzania has become known for its
innovative interventions that encourage a voice among rural communities
and the development of capable grass roots leaders who are committed to
fight gender rights violations in Pangani.
UZIKWASA’s multimedia work that has addressed violence against women and girls (VAWG) includes:
-Pangani FM radio programs
*Leadership that Touches (UongoziwaMguso)
*Womens’ Voice (Sauti ya Mwanamke)
-Feature films
*Fimboya Baba (Father’s Stick: Early and forced marriage)
*Chukua Pipi (Sweet deceit, sexual abuse of school children)
*AISHA (Gang rape)
-Comic books
* Varangati
*Halafu series
*AISHA book
-Forum Theatre and Theatre for Development
-A series of TV spots
On
December 2 UZIKWASA will participate in the 16 days of activism by
launching theMinna Dada Day, abig bang event to create awareness on
VAWGin Pangani District.The campaign is designed to start a deep
reflection process among the Pangani people and their leaders about
atrocities committed against women and girls including Intimate Partner
violence.
Minna dada introductory TV Spot
The
following four “Minna Dada” TV spots paint a picture of how intimate
partner violence affects the lives of local Pangani women. Cinema Zetu
of AZAM TV will broadcast the four spots during the next four months.
1.Economic exploitation of women by their male partners
2. Rape in marriage
3.Male partners hindering women to access leadership position
4.Emotional violence through public humiliation
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Baraza la katiba Zanzibar, Profesa Abdul Shariff
akizungumza kuhusu umuhimu wa asasi za kiraia kutoa elimu juu ya Katiba
Pendekezwa katika kongamano lililofanyika Unguja lililoandaliwa na
Taasisi ya Vijana ya TYVA pamoja na IRI.
Mbunge
wa Viti maalum Pemba-Zanzibar, Mheshimiwa Zainabu Mussa Bakari
akizungumzia Haki na Wajibu wa mwananchi Kikatiba wakati wa ufunguzi wa
Kongamano lililowashirikisha vijana mbalimbali kutoka kisiwani Pemba ili
kujadili katiba mpya lililoandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA pamoja na IRI.
Baadhi
ya vijana wakipitia katiba wakati wa kongamano lililowakutanisha vijana
hao ili kujadili haki na wajibu wa wananachi katika katiba mpya.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada
Baadhi ya vijana wakichangia mada
Mtaalam
wa Katiba, Ndugu Khamisi akizungumzia msingi na muktadha juu ya katika
katika kongamano lililofanyaika Unguja uliowakutanisha vijana.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia kongamano lililowakutanisha ili kujadili haki na wajibu wa vijana katika katiba mpya.
Na Mwandishi Wetu
Asasi
Ya Vijana, Tanzania Youth Vision Association kwa Kushirikiana Na
International Republican Institute zimetoa mafunzo ya kuboresha Uwezo wa
Vijana kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini katika visiwa vya
Unguja na Pemba, Zanzibar.
Mafunzo hayo yameweza kufikia vijana 250 kwa njia ya Warsha na Vijana na wananchi zaidi ya 200,000 kupitia mitandao ya kijamii.
Ndugu
Nasser Mtengera (Mkuu wa Idara ya Habari na Utafiti, TYVA) alielezea
Lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na ushiriki wa Vijana
katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Katika ufunguzi wa mafunzo hayo
Chake chake, Pemba Mheshimiwa Zainab Mussa Bakari (Mbunge) alibainisha
kuwa wananchi wana haki ya kikatiba ya kushirikishwa katika mchakato wa
katiba mpya na kusema nini wanachotaka kiwemo ndani ya katiba.
Mwanaharakati
Na Mtetezi wa HAKI za Binadamu ndugu Deus Kibamba (Mwenyekiti - Jukwaa
la Katiba Tanzania) alipata kuwaelezea washiriki wa mafunzo hayo
historia ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, Ushiriki wa wananchi
katika mchakato wa Katiba, hatua muhimu katika Mchakato wa utengenezaji
Katiba, Mambo ya Msingi yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa na Mambo
muhimu kuelekea kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
Alidokeza
pia, katika mchakato wa Katiba, hasa katika hatua ya Bunge la Katiba
ulikosa maridhiano ya Kitaifa. kuna haja ya kuwepo mkutano wa kitaifa
utajaowaleta wadau na jopo la wataalamu mbalimbali kwa ajili ya
kunyambua yale mambo yanayoendelea kuleta ukakasi linapaswa kufanyika.
Alidokeza pia Mchakato wa katiba ulitegemewa kuwa kimbilio la kutatua
kero za Muungano.
Afisa
kutoka IRI, Tony Alfred aliwatarifu Vijana washiriki kusoma kuhusu
Katiba na wanaweza kupata habari na taarifa zaidi kuhusu Katiba kupitia
ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutuma Neno "katibayetu" Kwenda
0684996494.
Ndugu
Saddam Khalfan (Katibu Mtendaji wa TYVA) aliwashukuru vijana na wadau
mbalimbali kwa kuhudhuria na kufanikisha mikutano ya Unguja na Pemba
huku akihimiza Mkakati wa ushiriki wa vijana ni mahsusi kwa ajili
ya kuhakikisha kuboresha maendeleo ya vijana kwa Tanzania ya sasa na
baadae. Tanzania ambayo inatamaniwa na kundi la vijana lakini sambamba
na makundi mengine yote.
Vijana
wajasiliamali wakiwa katika mafunzo ya kutengeneza urembo wa Shanga
baada ya kupata somo kutoka kwa Mkufunzi Peninnah katika mafunzo hayo
Biashara kwa Vijana kuelekea Soko la AFrika Mashariki yanayoendelea
kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Picha na
Mafoto Blog
Vijana wakichangamkia bidhaa kuanza kutengeza Shanga
Vijana wajasiliamali wakirefresh kwa kucheza mchezo wa kujichangamsha..........
Mkufunzi akitoa maelekezo ya mchezo huo..
No comments :
Post a Comment