Katibu Mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA,Mhandisi Goodluck Mmary
………………………………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad Arusha
WADAU wa shirika la Umeme nchini Tanesco mkoa wa Arusha wamekataa ombi la Tanesco la kutaka kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.19.na kulitaka shirika hilo lisiwageuze shamba la bibi kwa kulinufaisha kupitia bei ya umeme.
Wakichangia
katika Kikao hicho kilichofanyika Novemba 16 kwenye ukumbi wa benki
kuu,jijini Arusha,Wadau wa TANESCO wamesema kitendo cha kuomba
kuongezewa kiwango cha malipo ya umeme ni kuwakandamiza na kuwaumiza
wananchi, pia ni kuwaongezea mzigo wa maisha.
Hivyo Wadau hao wamepinga vikali hatua ya TANESCO kutaka kupandisha bei ya gharama za umeme kuanzia mwaka 2017 na kuitaka TANESCO isiwatwishe mzigo wa madeni Wadau wake kupitia mkakati wa kuongeza bei za umeme.
Wamesema
wanashangaa Tanesco kuomba kupandisha bei wakati serikali ilishasema
kuwa umeme unazalishwa kwa kutumia gesi hivyo hautapanda lengo ni
kumpatia mwananchi unafuu wa maisha sasa iweje Tanesco wanaomba kuongeza
bei ya umeme.
Kwa
upande wake Baraza la Ushauri la Serikali,GCC, limeelezea kutokubaliana
na Uamuzi wa Shirika la Umeme Tanzania kuamua kupandisha bei ya Umeme
kwa asilimia 18.19 Kuanzia Januari 2017.
Mjumbe wa baraza la Ushauri la serikali GCC,Mafutah Bunini, amesema Baraza limeshangazwa na hatua hiyo ya TANESCO kutaka kupandisha bei ya umeme wakati Serikali ya awamu ya tano inaweka mkazo na msisitizo katika kukuza uchumi
kwa kufufua na kujenga Viwanda ambavyo vitategemea zaidi upatikanaji wa
umeme wa uhakika katika uendeshaji wa shughuli zake za kazi.
Bunini,amesema kuwa kufuatia hatua ya TANESCO kutaka kupandisha bei ya umeme katika kipindi hiki kinaweza kusababisha Wawekezaji katika sekta ya Viwanda kuhofia na baadaye kuhamia nchi nyingine.
Katika Kikao hicho Katibu Mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA,Mhandisi Goodluck Mmary , ameishauri Serikali kuliunda upya Shirika hilo ili liweze kufanya kazi wa tija na ufanisi zaidi katika utoaji wa huduma ili liweze kukabiliana na changamoto ambazo Shirika hilo linakabiliana nazo
Katibu Mtendaji Mhandisi Mmary amesema katika mipango ya Shirika hilo ni kupuguza gharama ili liweze kuwafikia zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania kuweza kupata huduma za umeme.
Baraza lisisitiza kwamba kitendo cha TANESCO kushusha na kupandisha bei za umeme katika kipindi kifupi si sahihi Kiuchumi na hakileti tija
kwa Wananchi na Wafanyabiashara kutokana na kuwepo na bei za umeme
zisizotabirika hali ambayo inaweza kuleta athari kubwa katika uendeshaji
wa Vianda
Mmary,amesema hatua ya TANESCO kutaka kupandisha bei ya umeme katika
kipindi hiki kinaweza kusababisha Wawekezaji katika sekta ya Viwanda
kuhofia na baadaye kuhamia nchi nyingine.limesisitiza Baraza hilo la Ushauri katika Mkutano huo wa Wadau.
Baraza lisisitiza kwamba kitendo cha TANESCO kushusha na kupandisha bei za umeme katika kipindi kifupi si sahihi Kiuchumi na hakileti tija
kwa Wananchi na Wafanyabiashara kutokana na kuwepo na bei za umeme
zisizotabirika hali ambayo inaweza kuleta athari kubwa katika uendeshaji
wa Vianda.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Felix Ngalmgosi amesema hatua ya TANESCO kuomba kupandisha bei ya Umeme kutawakwamisha Wawekezaji katika sekta mbalimbali za Uchumi na Viwanda.
Mhandisi Ngalmgosi ameeleza katika Kikao hicho cha Wadau kwamba kwa mara ya mwisho TANESCO iliwasisha ombo la kurekebisha bei za huduma za umeme February mwaka huu 2016 ikitaka kupunguza bei hizo kwa asilimia 1.1 kwa mwaka 2016
Aidha Mhandisi Ngalmgosi amefafanua kwamba Shirika hilo liliahidi kuendelea kupunguza bei za umeme kwa asilimia 7.9 kuanzia mwaka 2017 hata hivyo EWURA inashangaa kuona TANESCO inaomba kuongeza bei hizo za umeme.
Hivyo EWURA inassitiza kuwa Mamlaka hiyo inazingatia misingi mikuu mitano ya udhibiti kwa
TANESCO kuzingatia Uwazi,Uwajibikaji,liwe na maamuzi
yanayotabirika,Ushirikishwaji Wadau na kufuata Sheria na taratibu
likizingatia gharama halali na halisi za uzalishaji na usambazaji wa hudum za umeme likirejea gharama za Uwekezaji.
Mkurugenzi Msaidizi wa TANESCO anayesimamia kitengo cha Uwekezaji Mhandisi Decklan Paul Mhaiki amesema kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji za Shirika hivi linalazimika kupandisha bei za umeme kwa asilimia 18.19 kutokana na gharama za kuzalisha umeme,kusafirisha na kusambaza umeme
Mhandisi Mhaiki amefafanua kuwa hatua hii imezingatia zaidi gharama za Uwekezaji kwa ajili ya kupunguza upotevu wa umeme,gharama za Uwekezaji kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Wateja Wapya,gharama za mtaji na gharama za uendeshaji na matengenezo.
No comments :
Post a Comment