Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme Tanzania (TEMESA), Dkt. Mussa Mgwatu akieleza utendaji kazi
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa,
alipotembelea Wakala huo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamini
Sawe-Maelezo)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), alipokagua karakana ya
Wakala huo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamini Sawe-Maelezo)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiteta na mmoja wa madereva wa
Serikali katika karakana ya TEMESA, alipokagua karakana ya Wakala huo,
jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamini Sawe-Maelezo)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme Tanzania (TEMESA), Dkt. Mussa Mgwatu akisisitiza jambo wakati
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa,
alipotembelea Wakala huo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamini
Sawe-Maelezo)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo wakati akiongea
na wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Kanda ya
Dar es Salaam na Pwani (hawapo pichani) alipokutana nao jijini Dar es
Salaam. (Picha na Benjamini Sawe-Maelezo)
Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi
na Umeme Tanzania (TEMESA), Kanda ya Dar es Salaam na Pwani,
wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa (hayupo pichani) alipokutana nao jijini Dar es Salaam kuwaeleza
mikakati ya Serikali kwa Wakala huo.
(Picha na Benjamini Sawe-Maelezo)
……………………………………………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka uongozi wa Wakala wa Ufundi
na Umeme nchini (TEMESA), kuharakisha zoezi la uwekaji wa mifumo
madhubuti ya kieletroniki katika vituo vyake ili kuongeza ufanisi katika
utendaji kazi.
Hayo ameyasema wakati alipokuwa
akizungumza na wafanyakazi wa Wakala huo wa kanda ya Dar es Salaam na
Kibaha ambapo amesema mifumo hiyo ikikamilika itadhibiti na kuongeza
mapato kwa uharaka.
“Kamilisheni haraka hiyo mifumo
ili kuweza kuboresha utendaji kazi wenu na wateja waweze kufurahia
huduma ya uhakika na haraka”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha ameongeza kuwa Wakala
unatakiwa kupunguza idadi ya wafanyakazi wasio na tija na kuajiri
wafanyakazi wachache wenye sifa kulingana na mahitaji halisi
yanayohitajika katika vituo vyao.
“Msilete watumishi kwa sababu
mnawajua, chukueni watu mnaowahitaji kulingana na kazi zenu ili muweze
kuifanya TEMESA iwe na hadhi inayostahili”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wa ongezeko la gharama
za vipuri vya magari zisizoendana na bei ya soko na kupelekea kupunguza
wateja kwa Wakala huo, Prof. Mbarawa ameuagiza uongozi kuwaondoa
wasambazaji wote wanaoongeza gharama hizo ifikapo mwishoni mwa mwaka
huu.
Naye Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Dkt
Mussa Mgwatu amesema Wakala huo utaanza kutumia mfumo wa kitehama kwa
ajili ya kutunza taarifa za matengenezo ya magari na utafanywa kwa awamu
ukianzia karakana ya Dar es Salaam na Kibaha.
Dkt. Mgwatu ameongeza kuwa Mfumo
huo utaweza kufatilia mwenendo wa gari na kutuma ujumbe mfupi kwa njia
ya simu (sms) kwa wateja kuwakumbusha siku za matengenezo ya magari,
wateja kujua mwenendo wa matengenezo na Wakala kutambua madeni yaliyoko
kwa wateja.
Katika kuboresha utendaji kazi na
kuongeza ufanisi amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuunda muundo
mpya ambao utabainisha majukumu ya kila kada kwa uwazi ili kusaidia
kutoingiliana kazi.
No comments :
Post a Comment