Thursday, November 24, 2016

Profesa Museru: Wauguzi Toeni Huduma Bora kwa Wagonjwa

waug1
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru akizungumza  na wauguzi  wa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika mkutano  uliofanyika leo  hospitali  hapo.
waug2
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH  Profesa Museru  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi mara baada ya kufunga mkutano huo uliofanyika mapema leo.
………………………………………………………………………
Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili- MNH,  Profesa   Lawrence Museru amewataka wauguzi kufanya kazi kwa bidii  na kuzingatia maadili  ya Uuguzi ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma  katika hospitali hiyo .
Profesa Museru  ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam  katika  mkutano  wa wauguzi  Tawi la Muhimbili  uliolenga kumpongeza  kwa kuteuliwa  kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo .
Profesa Museru  amesema  licha ya  wauguzi hao kukabiliwa changamoto mbalimbali  lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha upendo kwa wagonjwa  ili kukabiliana na ushindani na kutoa huduma  bora.
“ Hii ni hospitali ya Taifa inatoa huduma za kibingwa hivyo ni lazima huduma zitolewe kwa kiwango cha juu kulingana na hadhi yake” amesema Profesa Museru.
Akisoma Risala kwa niaba ya wauguzi  Katibu wa TANNA  Taifa  Sebastian Luziga   amesema wauguzi wa MNH  wanamshukuru Profesa Museru kwa jinsi anavyojitoa kuwasaidia katika mambo mbalimbali  na kwamba  hali hiyo inaonyesha anathamini taaluma ya uuguzi.

No comments :

Post a Comment