Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar
Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akiwa na mgeni wake Ndg Wilfred
Moshi wakiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani
Zanzibar, kutembelea na kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Ndg Wilfred Moshi ni Mtanzania wa Kwanza kupanda
Mlima Mkubwa Duniani wa Evarest ukiwa na Mita 8,848, Mtanzania huyo Ndg
Wilfred Moshi amepanda mlima huo mwaka 2012. akiwa ni Mwaafrika wa Tatu
kupanda mlima huo na mwafrika wa Pili mweusi kupanda mlima huo Duniani
kwa ukubwa.
Ndg Wilfred Moshi akiwa Zanzibar kwa
matembezi na kuangalia Utalii wa Zanzibar na kupata nafasi kutembelea
Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa mualiko wa Mhe Mwakilishi wa
Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Ndg Wilfred Moshi akitambulishwa kwa
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwa Mgeni wa Mwakilishi wa
Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akisalimia
Wajumbe wa Baraza wakati wa kutambulishwa kwake.
Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima
Evarest Ndg Wifred Moshi akiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said. akiwa
katika sehemu ya wageni katika ukumbi huo wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar
Mhe Simai Mohammed Said, akimtambulisha Mgeni wake Ndg Wilfred Moshi kwa
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid, alipofika
kutembelea na kujionea shughuli za Baraza la Wawakilishi wakati wa
Mkutano wake leo asubuhi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mtanzania wa Kwanza na Muafrika wa
Tatu Duniani kupanda Mlima wa Evarest Ndg Wilfred Moshi alipofika katika
jengo la Baraza la wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai
Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya mgeni wake Ndg
Wilfred Moshi ambae ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Evarest..
Ndg Wilfred Moshi akitowa historia yake
kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika
katika majengo ya Baraza la Wawakilishi kwa mualiko wa Mhe. Simai
Mohammed Said Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar. akitowa historia yake ya
kufanikiwa kupanda mlima huo mkubwa duniani na kuelezea tayari
ameshapanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 100.
Ndg Wilfred Moshi akiwa katika picha ya
pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa
ajili ya kumbukumbu yake alipofika kutembelea Baraza la Wawakilishi
Chukwani Zanzibar leo. 29-11-2016 akiwa mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la
Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa
katika picha ya pamoja na Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa
Duniani wa Evarest Ndg Wilfred Moshi alipofika katika jengo la Baraza la
Wawakilishi Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
othmanmaulid@gmail.com
Bukoba, Novemba
29, 2016-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)
leo imetoa msaada mifuko ya saruji 500 yenye thamani ya shilingi
milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera.
Msaada huo ni kuitikia wito wa serikali kwa mashirika, watu
binafsi na watu wenye mapenzi mema wa kujitoa kusaidia wahanga wa
tukio hilo.
Akizungumza
katika tukio la kukabidhi msaada huo katika Ofisi ya Mkuuu wa Mkoa wa Kagera
mjini Bukoba, Meneja Usalama wa SBL, Sebastian Kalugulu aliwapa
pole wahanga wa tetemeko hilo kwa kuwahakikishia kwamba
SBL kila mara iko tayari kusaidia pindi inapohitajiwa na
jamii.
“”Tunatoa
pole ya dhati na masikitiko yetu kwa wahanga wa tetemeko la
ardhi na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka,” alisema Kalugulu,
na kuongeza kwamba SBL inaungana na watu wengine wenye mapenzi mema
kutoa msaada wa kibinadamu kwa ajili ya kuwasaidia kuhimili kadhia
iliyowapata na kurudi katika shughuli zao kawaida.
Kalugulu
alithibitisha tena kwamba kampuni hiyo ya bia imejikita katika
kuunga mkono serikali na watu binafsi wenye mapenzi mema,
mashirika na makampuni katika kuisaidia jamii katika
maeneo SBL inapoendesha shughuli zake.
“Ni
matumaini yetu kwamba msaada huu utachangia katika
michango iliyokwishatolewa na wasamaria wengine na kwamba
itawawezesha wahanga hao kujenga miundombinu
iliyoharibika na hata kuboresha maisha yao.”
Akizungumzia
mchango uliotolewa na SBL, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum
Kijuu alisema kwamba msaada huo unachangia katika
michango mingine kutoka kwa watu wenye mapenzi
mema kutoka ndani, mikoani na kimataifa ambao kmwa
ukarimu waliitikia wito wa serikali wa kusaidia.
Mkuu huyo wa mkoa
alisema kuwa atahakikisha kuwa msaada huo unaenda kwenye lengo
lililokusudiwa na kutoa wito kwa watu
zaidi kuendelea kuwasaidia wahanga.
Mwisho
Katibu Mtendaji wa Chama cha Afya ya
Jamii Tanzania (TPHA), Fabian Magoma (kulia), akizungumza katika
Kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA)
linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Kushoto ni Mwenyekiti wa TPHA anayemaliza muda wake, Daktari Bingwa
Elihuruma Nangawe.
Dk. Manase Frank akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Profesa Andrew Swai akitoa mada.
Wadau wa sekta ya afya wakifuatilia kwa karibu mada zilizokuwa zikitolewa katika kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Dk. Andronicus Aloyce Rwelamila kutoka
Hospitali ya Tumbi Kibaha (kushoto) na Muuguzi wa Hospitali hiyo, Mary
Gowele wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea
Usikivu katika kongamano hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa TPHA, Dk. Elihuruma Nangawe
Profesa Japhet Kileo (kulia), akiuliza maswali kwenye
kongamano hilo.
Dk. Mwanahamisi Magwangwara (kushoto),
akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta
ya afya katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii
Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es
Salaam leo. Kulia ni mtoa mada, Profesa Andrew Swai.
Dk.Chilolo Edward (katikati), akijibu
maswali kuhusu changamoto ya waendesha bodaboda. Kushoto ni Profesa
Andrew Swai na Dk. Manase Frank.
Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika
Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akielezea changamoto ya
matumizi ya pombe katika Manispaa ya Kinondoni.
Na Dotto Mwaibale
MADAKTARI nchini wametakiwa kufanya mikutano ya kijamii au wananchi ili kuwapa fursa ya kujua magonjwa yanayo wakabili.
Hayo yalielezwa na Dk. Manase Frank
wakati akitoa mada katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya
ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini
Dar es Salaam leo asubuhi.
"Changamoto kubwa tuliyonayo ni wananchi
wengi kutojua magonjwa yanayowasumbua hivyo ni muhimu kwa madakatari
kuitisha mikutano itakayowakutanisha na wananchi ili kuondoa changamoto
hiyo" alisema Dk. Frank.
Alisema wagonjwa wengi wamekuwa wakikata
tamaa kwa kuchangiwa na kauli za baadhi ya madaktari ambao wanashindwa
kujua tatizo la mgonjwa husika hivyo wakati umefika wa madaktari
kushirikiana kwa karibu na jamii, viongozi wa dini ili kuondoa
changamoto hiyo.
Akitolea mfano wa kijana mmoja ambaye
alifiwa na ndugu zake wote wa karibu kutokana na ugonjwa wa ukimwi na
kuishi kwa kunyanyapaliwa lakini baadaye afya yake ilikuja kuimarika
kufuatia ushauri uliotolewa na daktari kwa jamii iliyokuwa ikimzunguka
wakati wa ugonjwa wake.
Mtoa mada mwingine Profesa Andrew Swai
aliomba serikali wakati wa siku ya Jumamosi na Jumapili kufunga baadhi
ya barabara ili zitumike kwa wananchi kufanya mazoezi ya kutembea ili
kujenga afya za miili yako na kuepukana na magonjwa kama kisukari.
Akizungumzia changamoto ya matumizi ya bodaboda Dk.Chilolo
Edward alisema kwa mwaka jana katika Hospitali za mikoa ya Morogoro,
Tumbi Pwani na Shinyanga kulikuwa na ajali 895 huku majeruhi wakiwa
4813.
Alisema majeruhi waliolazwa katika
hospitali hizo walikuwa ni 4525, waliopewa rufaa kwenda hospitali za
Bugando na Muhimbili walikuwa 71 na waliolazwa ni 702.
Alisema vifo vilikuwa 81 hivyo vilitokea baada ya kufikishwa Hospitalini ni 70 na vilivyotokea eneo la ajali vilikuwa 11.
Dk.Chilolo alisema ili kupunguza
changamoto hiyo inapaswa watoa huduma za afya kutoa elimu kwa waendesha
boda boda pale wanapofikishwa mahospitali kuhusu umuhimu wao katika
familia na taifa kwa ujumla hivyo kuwa makini wanapoendesha vyombo hivyo
vya moto badala ya kuacha kazi hiyo kufanywa na polisi au Sumatra.
No comments :
Post a Comment