Imeleezwa
kuwa ili kumwezesha kila mwananchi wa Tanzania kupata maendeleo na
kuondokana na janga la umaskini, Serikali haina budi kutunga sera ambazo
zitamgusa kila mwananchi na kuwa na faida jambo ambalo litawasadia
kukuza uchumi wao binafasi na taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na
mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Kijamii (ESRF), Philemon Luhanjo katika mkutano wa siku moja wa kujadili
sera za kijamii zinavyoweza kusaidia kubadilisha uchumi wa Tanzania,
mkutano ambao uliandaliwa na ESRF.
Luhanjo
alisema ni vyema Serikali inapokuwa inatunga sera ihakikishe zinakuwa
na faida kwa wananchi ili ziweze kuwasaidia kupata maendeleo na
kuboresha maisha yao na hata wakati nchi ikielekea katika uchumi wa kati
kila mwananchi ahusike na mabadiliko hayo.
"Sera
zipo nyingi, zipo za maendeleo ya jumla, elimu, afya, kilimo, viwanda
na kila kitu, sisi tunajaribu kuangalia tunapotengeneza sera mbalimbali
tuhakikishe kwamba sera hizo zitamnufaisha binadamu, kwamba chochote
unachofanya kiwe nikwa faida ya mwanadamu, mipango na malengo yote yawe
yanamlenga binadamu kuondoa matatizo yake,
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akihutubia katika mkutano
wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake
kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya
Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.(PICHA:K-VS
BLOG/KHALFAN SAID).
"Serikali
inapofanya mipango inatakiwa kupanga mipango ambayo inajaribu kujibu
kero za mwananchi, kama ni elimu, kama ni afyaa au kama ni kilimo cha
kisasa, tunapotengeneza sera tuwe tunauwianisha, hizo sera
zikitekelezeka na mteja wa bidhaa awe ameandaliwa ili mkulima asiwe
amepoteza nguvu bure," alisema Luhanjo na kuongeza.
"Tunazungumzia
nchi ya viwanda, viwanda gani? na nchi yetu niya kilimo kwahiyo
tunatarajia viwanda vingi vitakuwa ni vya kilimo, kwahiyo tunataraji
mkulima mdogo aimalishwe ili aweze kuzalisha mazao yanayokwenda
kiwandani ni lazima sera ziwe na uwiano mzuri."
Nae
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema
Serikali inafahamu kuwa nchi haiwezi kupiga hatua bila kuhusisha
mwananchi mmoja mmoja na inachofanya kwa sasa na kuwashawishi watu wenye
viwanda kutumia malighafi ambazo zinazalishwa nchini ili wakulima
nchini wafaidike na uwepo wa viwanda nchini.
"Tunaamini
hatuwezi kuwa na uchumi unaokua kama hali ya kijamii ya wananchi haikui
na hata Rais Magufuli alikuwa akisema tangu akiwa katika kampeni kwamba
Tanzania ya Magufuli niya viwanda, na viwanda hivi ni kwa ajili ya watu
wetu,
Mwenyekiti
wa Bodi ya wadhamini wa ESRF, Philemon Luhanjo, akizungumza katika
mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake
kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na ESRF.
"Kwenye
mpango wetu wa miaka mitano tumesisitiza maendeleo ya viwanda lakini
vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini katika kilimo chetu,
kwahiyo hatuwezi kuwa na viwanda kama kilimo hakijaendelea, hatuwezi
kuwa maendelo ya kijamii kama kilimo chetu hakijaendelea, kilimo ndiyo
uti wa mgongo wa taifa letu, kwahiyo tumejadili hilo ili kuona wananchi
wetu wananufaika vipi," alisema Kijaji. Kwa upande wa Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alizungumza kuhusu mkutano huo ambao
umedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na
kusema,"ESRF kwasasa hivi tupo kwenye mchakato wa kutengeneza Ripoti ya
Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017, "Katika hiyo ripoti tumeweza
kutaharisha ripoti 11 ambazo zitachangia katika utayarishishaji wa hiyo
ripoti na dhumuni kubwa ni kuweza kuzijadili hizo ripoti na kupata
uelewa mpana ni kwa kiasi gani sera za kijamii zina mchango mkubwa
katika kuleta mageuzi ya kiuchumi hapa Tanzania."
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mkutano
huo.
Mkuu
wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon
Manyama akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za
jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.
Mtafiti
mshiriki mwandamizi wa ESRF, na mashauri wa ufundi wa mradi wa THDR
Profesa Marc Wuyts, akiwasilisha mada Situating social policy
transformation: A conceptual framework, kwenye mkutano wa tano wa mwaka
wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya
kiuchumi nchini Tanzania.
Mhadhiri
wa Masuala ya Afrika na Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Edinburgh,
Shule ya Sayansi ya Siasa nchini Uingereza Dk.Hazel Gray, akiwasilisha
mada yake kuhusu mabadiliko katika sera za kijamii kwenye mkutano wa
tano wa mwaka wa ESRF.
Mchokoza
mada kutoka taasisi ya Daima na Mtafiti mwandamizi mshiriki ESRF,
Profesa Samwel Wangwe, akitoa maelezo yake kuhusu mada iliyowasilishwa
mezani kwa wajumbe.
Profesa
wa uchumi DoE, Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Mushi,
akiwasilisha mada kuhusu historia ya sera ya jamii katika mkutano huo.
Mgeni
rasmi Dk. Kijaji, (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk.
Tausi Kida, (wa kwanza kushoto), Bi Anna, na mwenyekiti wa bodi ya
udhamini ya ESRF, Bw Philemon Luhanjo, Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini
na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha (wa pili
kulia) wakipongeza wakati wa mkutano huo.
Wageni
waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali kwa makini katika mkutano wa tano
wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye
mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania
Picha ya pamoja ya washiriki, wakuu ESRF, wakiwa na mgeni wa heshima Dk. Kijaji.
No comments :
Post a Comment