Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Brad Gordon
akizungumza kuhusu uwekezaji wa kampuni yake hiyo, nchini pamoja na
uzalishaji pia utekelezaji wa miradi ya kijamii kwenye maeneo ya migodi
ya kampuni hiyo, wakati wa mkutano huo wa uwekezaji katika sekta za
maliasili za mafuta na gesi, uchimbaji madini kilimo na maendeleo ya
mifugo, uliotayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Kampuni
ya Montage ya jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim
Mbarouk-www.bayana blogspot.com)
Baadhi
ya wawekezaji na washiriki wa mkutano huo, wakifuatilia maelezo
mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya watendaji wa kampuni
zilizowekeza vitega uchumi nchini katika sekta za maliasili za mafuta na
gesi, uchimbaji madini kilimo na maendeleo ya mifugo, uliotayarishwa na
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Kampuni ya Montage ya jijini Dar
es Salaam leo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Anglogold Ashanti, Srinivasan
Venkatakrishnan, akizungumza kuhusu uwekezaji wa kampuni yake hiyo
nchini pamoja na uzalishaji pia utekelezaji wa miradi ya kijamii kwenye
maeneo ya migodi ya kampuni hiyo, wakati wa mkutano huo wa uwekezaji
katika sekta za maliasili za mafuta na gesi, uchimbaji madini kilimo na
maendeleo ya mifugo, uliotayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) na Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Anglogold Ashanti, Srinivasan
Venkatakrishnan, akizungumza katika mkutano huo, wa uwekezaji katika
sekta za maliasili za mafuta na gesi, uchimbaji madini kilimo na
maendeleo ya mifugo, uliotayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) na Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya wawekezaji na washiriki wa mkutano huo, wakifuatilia mada mbalimbali
pamoja na maelezo kuhusu kampuni zilizowekeza katika sekta za maliasili
za mafuta na gesi, uchimbaji madini kilimo na maendeleo ya mifugo,
uliotayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Kampuni ya
Montage ya jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakiwa na washiriki wa mkutano huo, wakifuatilia
mada mbalimbali pamoja na maelezo kuhusu kampuni zilizowekeza katika
sekta za maliasili za mafuta na gesi, uchimbaji madini kilimo na
maendeleo ya mifugo, uliotayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) na Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya wawekezaji na washiriki wa mkutano huo, wakifuatilia kwa makini mada
mbalimbali pamoja na maelezo ya watendaji wa kampuni zilizowekeza
nchini katika sekta za maliasili za mafuta na gesi, uchimbaji madini
kilimo na maendeleo ya mifugo, uliotayarishwa na Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC) na Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya washiriki wakiwa katika mkutano huo, wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwasilishwa na watendaji wa kampuni zilizowekeza nchini
katika sekta za maliasili za mafuta na gesi, uchimbaji madini kilimo na
maendeleo ya mifugo, uliotayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) na Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini Tanzani, Dk. Samuel Nyantahe,
akizungumza katika mkutano huo wa uwekezaji kuhusu ushiriki wa
shirikisho hilo katika kukuza uwekezaji nchini.
Mkurugenzi
wa Huduma za Uwanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),
Louis Accaro, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF,
Godfrey Simbeye, wakati wa mkutano huo.
Baadhi
ya washiriki wakiwa katika mkutano huo, uliotayarishwa na Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Montage ya jijini Dar es
Salaam leo.
Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi na Nishati (TCME), Balozi Ami Mpungwe, akizungumza wakati wa mkutano huo, wa uwekezaji nchini.
Baadhi
ya washiriki wakiangalia vijarida na machapisho yaliyokuwa na maelezo
mbalimbali kuhusu uwekezaji wakati wa mkutano huo, uliotayarishwa na
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Kampuni ya Montage ya jijini Dar
es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Montage, Teddy Mapundi, washirika katika kuandaa
mkutano huo pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), akiwa katika
mkutano huo.
Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ally Samaje, akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Uwanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),
Louis Accaro, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taasisi hiyo,
ilivyojipanga katika kuinua uwekezaji nchini.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke,
Hashimu Komba (katikati), akikata utepe kwa niaba ya mkuu wa wilaya
hiyo, kuashiria kupokea madawati 80 yaliyotolewa na Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) kwa Shule ya Msingi ya Kibasila Dar es Salaam
jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Msaidizi wa Mkuu wa wilaya hiyo,
Betha Minga, Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo na
Mwakilishi wa Meneja wa TFS Kanda ya Mashariki, Mohamed Lyandama
Ofisa Mistu wa Wilaya ya Temeke, Fredrick Umilla (kulia), akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati.
Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo (kulia), akitoa taarifa kwa mgeni rasmi.Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo (wa pili kulia), akimkabidhi mgeni rasmi, Hashim Komba hati ya makabidhiano wa madawati hayo. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga na Mwakilishi wa Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TFS, Mohamed Lyandama.
Mgeni rasmi Hashim Komba akipanda mti wa
kumbukumbu mbele ya ofisi ya TFS Wilaya ya Temeke iliyopo Chang'ombe
Veta jijini Dar es Salaam.
Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Temeke, Bakari Mrondwa akipanda mti.
Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga
akishiriki kupanda mti.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes wakishiriki kupanda mti. Kulia ni Masha Hassan na Yahaya Hamza.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja
na maofisa wa TFS Wilaya ya Temeke pamoja na wanafunzi wa Shule ya
Msingi Wailes waliopokea madawati hayo kwa niaba ya wenzao.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYAKAZI wa Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Temeke wametakiwa kuendelea kuwa
waadilifu katika kazi zao za kila siku ili kujiepusha na vitendo vya
rushwa kutoka kwa watu wanaojihusisha na uharamia wa mali asili ya nchi.
Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana
na Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba kwa niaba ya mkuu wa
wilaya hiyo wakati akipokea madawati 80 yenye thamani ya sh. 6,370, 000
yaliyotolewa na TFS wilaya ya Temeke kwa ajili ya kukabiliana na uhaba
wa madawati wilayani humo.
"Kwa hali halisi ninayoiona hapa ofisini
kwenu najua ninyi ni waadilifu mnaviepuka vitendo vya rushwa endeleeni
kusimamia kazi yenu ili kulinda mali asili ya taifa" alisema Komba.
Komba alisema kuwepo kwa magunia ya mkaa
na mbao katika ofisi hiyo zilizokamatwa na kielelezo tosha kuwa hakuna
vitendo vya rushwa vinavyofanywa na maofisa wa ofisi hiyo.
Komba amewaomba TFS kuendelea kuchangia madawati ili kumuunga mkono
Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure na katika mazingira bora ikiwemo kukaa kwenye madawati.
Akitoa taarifa fupi wakati wa kukabidhi
madawati hayo Meneja Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya Tanzania (TFS)
Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo alisema wakala tangu kuanzishwa kwake
wamepata mafanikio makubwa kupitia utekelezaji wa mpango mkakati wa
kwanza wa miaka mitatu 2011 -2014 ambapo sasa wanaelekeza nguvu katika
kutekeleza mpango mkakati wa pili wa miaka mitatu 2014 hadi 2016.
Alisema katika kutekeleza majukumu yake
wakala imepata changamoto za uvamizi wa maeneo ya misitu kwa ajili ya
kilimo, ufugaji, makazi, ukataji miti, uchimbaji madini na uchomaji moto
misitu.
Alisema ili kukabiliana na changamoto
hizo inatakiwa kuongeza watumishi na vitendea kazi na kujenga vituo
katika kila msitu wa hifadhi na kuweka mabango ya tahadhari.
Kiondo alisema kuwa wakala umetayarisha
mpango bora wa usimamizi wa uhifadhi wa misitu na moja ya mikakati
iliyopo kwenye mpango huo ni kupanda hekta 185,000 za miti kwa mwaka kwa
kushirikiana na wadau ili kuziba pengo la mita za ujazo 19.5 milioni
kwa mwaka za timbao hadi kufikia miaka 2030.
No comments :
Post a Comment