Thursday, November 17, 2016

MAKONDA "AMLIPUA" KAMANDA SIRRO, NI KUHUSU UVUTAJI SHISHA JIJINI DAR ES SALAAM




Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa, (kulia), akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda, (kushoto), baada ya Makonda kutoa salam za mkoa wa Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa Mradi wa Ubireshaji Huduma za Umeme jijini Dar es Salaam uliofanyika Mikocheni jijini Dar es Salaam, Novemba 16, 2016. Katikati ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.


NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, “amemlipua” Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuwa nini uvutaji wa SHISHA umerejea kwa kasi jijini Dar es Salaam, hususan wilayani Kionondoni licha ya polisi kujua kuwa ni marufuku.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, Shisha inawaingizia mamilioni ya fedha wanaofanya biashara hiyo, tena hawazidi watu 10, hivi karibuni walikuja watu hao ofisini kwangu na kunieleza kuwa hupata faida ya shilingi milioni 30 hadi 40 kwa mwezi kwa kila mmoja, hivyo wakanieleza watanipa shilingi milioni 5 kila mwezi kwa kila mmoja sawa na shilingi milioni 50,   Alisema Makonda. Wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa uboreshaji huduma za umeme jijini Dar es Salaam, kwenye kituo cha TANESCO Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Lakini jambo la kusikitisha, baada ya hapo, uvutaji wa Shisha umerejea kwa kasi, nilimuagiza Kamishna Sirro lakini naona kama ana kigugumizi vile, sijui ile milioni 5 imempitia, na huyu kamanda wa polisi Kino ndoni, nilimuona hapa, naye naona kama anakigugumizi, sijui na yeye zilimpitia hizo milioni 5?
 alisema Makonda mbele ya Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha Rais Dlt. John Pombe Magufuli kwenye uzinduzi huo uliofanyika Novemba 16, 2016.
Makonda alisema, tayari ametoa maagizo kwa wakuu wote wa Wilaya, kulishughulikia suala hilo, na atakayeshindwa, atamuwajibisha. “Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunatekeleza maagizo yako, ambayo ni wewe uliyatoa, lakini sasa hali ndiyo hiyo.” Alisema Makonda.
Hata hivyo, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, aliurejesha “mpira” huo kwa Makonda mwenyewe kwa kumwambia, “Mh Makonda umesema hapa kuwa uvutaji wa Shisha umerejea jijini Dar es Salaam, haya ni maagizo tuliyatoa na alifanya kazi nzuri sana, yeye ndiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, na amesema hapa tayari amewaagiza wakuu wa wilaya kuchukua hatua na wakishindwa atawawajibisha, na mimi namwambia akishindwa nitamuwajibisha, sasa utaona protoko inarudi pale pale." Alifafanua Waziri Mkuu na hadhira kuangua kicheko.

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro
Kamanda wa Pilisi mkoa wa kipolisi, Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP), Salome Kaganda

No comments :

Post a Comment