Monday, November 28, 2016

Mkurugenzi Mkuu TBL Group atembelea masoko ya bidhaa za kampuni Mwanza na Mbeya

gro1
Mkurugenzi wa TBL Group,Roberto Jarrin (kushoto) akipata maelezo alipotembelea baa ya Shetemba jijini Mwanza
gro2
Mkurugenzi wa TBL Group,Roberto Jarrin na maofisa waandamizi wa kampuni wakiwa katiba baa ya Changamoto
gro3
Roberto na maafisa wengine waandamizi wa kampuni wakiangalia bidhaa za kampuni zilizopo kwenye masoko
gro4
Mmoja wa maofisa wa kampuni ya TBL akiangalia mpangilio wa bia kwenye jokofu kwenye baa ya Changamoto jijini Mwanza
…………………………………………………………………
Katika kutekeleza majukumu yake kwa Kasi Mpya,Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin, ambaye pia ni Rais wa kitengo cha Masoko cha kampuni mama ya kampuni hiyo ukanda wa Afrika Mashariki,mwishoni mwa wiki alitembelea masoko ya bidhaa za kampuni katika mikoa ya Mwanza na Mbeya.
 
Katika ziara yake hiyo Roberto alifuatana na maofisa waandamizi wa kampuni ya TBL Group ambapo waliweza kutembelea mabaa mbalimbali na kukutana na wamiliki wa mabaa .
 
Ziara hiyo iliwawezesha kujua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye masoko na kuwawezesha kuzitafutia suluhisho ikiwemo kubuni mikakati ya kujiimarisha zaidi kwenye masoko hususani katika kukabiliana na ushindani mkubwa uliopo katika sekta ya uuzaji vinywaji.
 
TBL Group kwa muda mrefu imekuwa na mkakati wa kufanya kazi kwa karibu na wauzaji wa mwisho wa bidhaa zake wanaozifikisha  kwa wateja.
 
Moja ya program ambayo inatekeleza kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano mzuri na wasambazaji hao na kuwawezesha kuwa na biashara imara na endelevu ni kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kupitia mpango unaojulikana kama Retail Development Programme (RDP) ambao umeonyesha kuwa na mafanikio makubwa.

No comments :

Post a Comment