Na Christian Gaya
Rasilimali halisi yaani
thamani ya mfuko wa NSSF imeongezeka kutoka shilingi bilioni 2,582.92 Juni 2014
mpaka kufikia shilingi bilioni 2,933.97 mpaka Juni 2015, ikiwa ni ongezeko la
asilimia 13.60 kwa mwaka.
Kulingana na Mwenyekiti wa
Bodi wa mfuko wa NSSF Profesa Samwel Wangwe anasema tathimini ya uimara wa mfuko
kwa kipindi kinachoishia Juni 2013 inaonesha mfuko utakuwa imara kwa miaka
mingi ijayo.
Anasema michango ilifikia shilingi
milioni 605.09 mwaka 2014/2015 ukilinganisha na shilingi milioni 548.47 mwaka
2013/2014. Ongezeka hili likuwa ni
asilimia 10.32.
Malipo ya mafao kwa mwaka
2014/2015 yalifikia bilioni 357.67 ukilinganisha na shilingi bilioni 344.79 mwaka
2013/2014. Ongezeko likiwa ni shilingi bilioni 12.88 sawa na asilimia 3.74.
“Pato kutokana na vitega
uchumi kwa mwaka 2014/2015 lilifikia shilingi bilioni 209.68 ukilinganisha na
shilingi milioni 222.16 kwa mwaka 2013/2014, upungufu ukiwa sawa na asilimia
5.6. Prof. anasema.
Anataja ya kuwa mapato
kutokana na kampuni tanzu yameongezeka kutokana na kampuni hizo kufanya vizuri
kwa kipindi cha mwaka ulioishia June 2015. Aidha gawio ya hisa limeshuka
kutokana na kuuzwa kwa baadhi ya hisa kampuni za Simba, TBL na TCC.
Anasema mapato mengine kwa
mwaka 2014/2015 yalifikia bilioni 41.62 ukilinganisha na shilingi bilioni 9.74
kwa mwaka 2013/2014 ongezeko likiwa ni asilimia 327.
Gharama za uendeshaji kwa
mwaka 2014/2015 zilifikia shilingi milioni 110.260 ukilinganisha na shilingi
milioni 105.224 kwa mwaka 2013/2014. Ongezeko ni shilingi milioni 5.036 ambazo
ni sawa na asilimia 4.79.
Wakati gharama za uendeshaji
kwa mwaka 2014/2015 ilikuwa ni asilimia 93.33 ya bajeti ya shilingi milioni
118.123.43. Uwiano huu ni chini ya kiwango cha asilimia 15 kama ilivyoanishwa
kwenye sheria ya NSSF Na 28 ya mwaka 1997 kifungu namba 61 (4)
Anasema kiasi kilichotengwa
kwa ajili ya mafao ya kustaafu ya wafanyakazi wa NSSF kwa mwaka 2014/2015
ilikuwa ni shilingi bilioni 12.32 ukilinganisha na shilingi milioni 12.22 kwa
mwaka 2013/2014
“Tengo la madeni yenye
mashaka/kuchelewa kwa mwaka 2014/2015 ilifikia shilingi bilioni 39.63
ukilinganisha na shilingi bilioni 135 mwaka 2013/2015. Madeni haya yamepungua
kwa shilingi bilioni 96.32. Kupungua kwa madeni haya kumetokana na kulipwa kwa
madeni yaliyocheleweshwa kulipwa kwa mwaka 2013/2014” Mwenyekiti wa bodi
anasema
Anasema kodi ya mapato lilifikia
shilingi bilioni 40.22 kwa mwaka 2014/2015 ukilinganisha na shilingi bilioni
0.51 kwa mwaka 2013/2014.
Wakati mapato mengine
yanayotokana na uthaminishaji rasilimali yalifikia bilioni 63.35 kwa mwaka
2014/2015 kulinganisha na bilioni 29.49 kwa mwaka 2013/2014 ikiwa ni asilimia
114.81.
“Ongezeko hili lilitokana na
kuwepo kwa uthamini wa majengo na ardhi yanayomilikiwa na Shirika kwa mwaka
2014/2015. Ongezeko la rasilimali halisi baada ya kodi lilifikia shilingi
bilioni 351.05 kwa mwaka 2014/2015, ukilinganisha na ongezeko la shilingi
milioni 204.85 mwaka 2013/2014. Hili ni ongezeko la asilimia 71.39 na linatokana
na kupungua kwa tengo la madeni yenye mashaka/kuchelewa kulipwa” anasema Prof
Wangwe.
Anasema rasilimali halisi
zilizopo kwa ajili ya mafao zimeongezeka kutoka shilingi milioni 2,582,921 kwa
mwaka 2013/2014 hadi kufikia shilingi
milioni 2,933,972 mwaka 2014/2015
Wakati vitega uchumi
viliongezeka shilingi bilioni 2,403.6 vilivyokuwepo Juni 2014 na kufikia
bilioni 2,728.01 ilipofikia Juni 2015. Ikiwa ni ongezeko la asimilia 13.41
ukilinganisha na mwaka 2013/2014
Anasema kwa ujumla
kumekuwepo na ongezeko la uwezekezaji kwenye Nyanja mbalimbali. Isipokuwa
dhamana za serikali, amana za mabenki ambayo imepungua.
Anasema upungufu mkubwa
katika amana za mabenki unatokana na amana zilizowekezwa mwaka uliopita kuiva
ndani ya mwaka huu, na mwaka huu uwekezaji mdogo umefanyika katika amana za mabenki kutokana na mahitaji
makubwa ya fedha kwa ajili ya uwekezaji kwenye vitega uchumi vya muda mrefu.
“Rasilimali hizi
ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 355.95 June 2014 na kufikia shilingi
bilioni 404.98 June 2015 ongezeko likiwa ni asilimia 13.77. Dhima dhidi ya Shirika
ni pamoja na makadirio ya mafao ya kustaafu ya wafanyakazi wa NSSF kwenye
mkataba wa hiari, fungu la pensheni ya wafanyakazi wa TTCL, na wadai mbalimbali”
Prof Wangwe anataja
Anasema hali ya ukwasi kwa ujumla
mwaka 2013/14 ilikuwa nzuri. Ilipofika june 2014 Shirika lilikuwa na shilingi
milioni 59,890.
Mpango wa Taifa wa hifadhi
ya jamii wa NSSF ulianza kama idara ya serikali mwaka 1964 kabla ya kuanzishwa
kama Shirika la Taifa la Akiba ya Wafanyakazi (NPF) kwa sheria Na 36 ya mwaka
1975.
Shirika hili liliendelea hadi
pale serikali ilipopitisha Sheria Na 28 ya mwaka 1997 iliyoanzisha Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kama mpango kamili wa hifadhi ya jamii
unaozingatia kanuni za kimatifa za hifadhi ya jamii ambapo.
Mabadiliko hayo yameiwezesha
NSSF kutoa mafao mengi na bora mpaka sasa yakiongoza kwa afrika mashariki na
kati zaidi yakiwemo mafao ya pensheni ambapo kabla ya hapo mfumo wa akiba wa
NPF ulikuwa unatoa mafao ya uzeeni kwa njia ya mkupuo. Mafao hayo yalikuwa ni
hafifu na machache sana.
Christian Gaya ni mwanzilishi wa
Kituo cha HakiPensheni Tanzania na mshauri wa masuala ya pensheni. Kwa maelezo
zaidi gayagmc@yahoo.com Au kwa habari
zaidi za kila siku juu ya HakiPensheni unaweza kutembelea tovuti www.hakipensheni.co,tz,
hakipensheni.blogspot.com Simu namba +255 655 13 13 41
No comments :
Post a Comment