Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa
TANESCO wa mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu (katikati) wakati
alipotembelea Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2,
2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa kutoka kwa Meneja wa TANESCO wa
Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu (kushoto) kuhusu hali ya
upatikanaji wa umeme kwenye makao makuu ya nchi Dodoma wakati alipotembelea
Kituo cha Umeme cha TANESCO cha Dodoma Oktoba 2, 2016. Wengine
Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama,
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Christina
Mndeme.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
wafanayakazi na viongozi wa kiwanda cha Gypsum cha Premalt cha Dodoma wakati
alipokitembelea mjini Dodoma Oktoba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uzalishaji katika
kiwanda cha Gypsum cha Premalt cha mjini Dodoma wakati alipokitembelea
Oktoba 2, 2016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akipokea kutoka kwa mkurugenzi wa kiwanda cha Magodoro Dodma, Haidary Gulamali,
magodoro 200 yenye thamani ya shilingi milioni 10 ukiwa ni msaada kwa
waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo
yalifanyika baada ya Waziri Mkuu kutembelea kiwanda hicho Oktoba 2, 2016.
Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Spring zinazotumika kutengeneza magoro
wakati aliopotembelea kiwanda cha Magodoro Dodoma Oktoba 2, 2016. Kushoto
ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Haidary Gulamali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi
wa kiwanda cha Magodoro Dodoma baada ya kutembelea kiwanda hicho Oktoba 2,
2016. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Haidary Gulamali na
kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana na wapili kulia kwake
ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses
Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na
Yanga na Serikali kufikia uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja
wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao
iliyofanyika Oktoba Mosi 2016. (PICHA NA
PICHA NA RAYMOND MUSHUMBUSI)
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses
Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na
Yanga na Serikali kufikia uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja
wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao
iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
NA K-VIS BLOG
SERIKALI
imetangaza kuzifungia timu za soka za Yanga na Simba kuutumia uwanja huo,
wakati zinapokutana kwenye michezo ya soka.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza leoOktoba 2,
2016 alipofika kwenye uwanja huo kujionea uharibifu uliofanywa na mashabiki wa
Simba, kwenye pambano la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara lililopigwa jana
Oktoba 1, 2016, ambapo baadhi ya mashabiki wa Simba wenye hasira, waling’oa
viti kufuatia bao la Amisi Tambwe, lililolalamikiwa kuwa lilifungwa baada ya
mchezaji huyo kuutuliza mpira wa Kross kwa mkono.
“Nimetembelea
uwanja wa Taifa na kukagua uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba katika mechi
dhidi ya Yanga hapo jana. Yafuatayo ni maamuzi yaliyochukuliwa na Serikali,”
Ameandika Waziri Nape kwenye ukurasa Wizara ya Habari ulio kwenye Facebook.
Kwa
mujibu wa Waziri Nape, maamuzi hayo ni pamoja na:-
1)Simba
na Yanga hazitoruhusiwa kutumia uwanja wa taifa hadi hapo itakapo amualiwa vinginevyo.
2)Simba itatakiwa kulipia hasara iliyotokana na uharibifu huu.
3)Simba haitopata mgao wake wa mechi ya jana.
4)Kamera za CCTV zitafungwa uwanja mzima kufuatilia mienendo ya mashabiki wanapokuwa uwanjani ili kuweza kuwatambua watu wote watakao jihusisha na vitendo vya fujo.

Tayari
uongozi wa Simba umetoa tamkola kuomba radhi kutokana na hatua ya
washabiki wake, lakini ikatupia lawama maamuzi mabovu ya waamuzi wa
pambano hilo ikiwa ni pamoja na kuruhusu bao "haramu' alilofunga Amisi
Tambwe, kwa vile alipokea pasi kwa mkono kabla ya kufunga, Hali
kadhalika taarifa hiyo ya Simba, imesema, mwamuzi huyo pia alikataa bao
la mshambuliaji wake Ajib, kwa maelezo kuwa mfungaji alikuwa ameotea
kitu ambacho washabiki wengiwa Simba wanadai haikuwa sahihi. Katika
pambano hilo la ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba licha ya
kucheza wakia pungufu kwa muda mrefu, walifanikiwa kusawazisha bao hilo
kwenye dakika za mwisho mwisho na hivyo pambano hilo kuwa sare ya bao
1-1.
Nape akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea uwanja huo leo Oktoba 2, 2016
Waziri Nape akikagua viti vilivyoharibiwa
NA ARON MSIGWA - NEC.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaendelea kutoa elimu ya Mpiga Kura kote nchini ili kuwajengea wananchi uelewa sahihi juu majukumu ya Tume na chaguzi zinazofanyika nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Jaji Lubuva amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakishindwa kutimiza Haki yao ya Kikatiba ya kupiga Kura kuwachagua viongozi wananowapenda kwa sababu ya kukosa uelewa juu ya Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia Uchaguzi .
Amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 inaipa NEC jukumu la kusimamia na kuendesha Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa upande wa Tanzania Bara na kubainisha kuwa ili jukumu hilo lifanywe kwa ufanisi wananchi waliotimiza vigezo vya kupiga kura na wale wanaotarajia kupiga kura miaka ijayo lazima wapatiwe elimu sahihi ya Mpiga Kura.
Amefafanua kuwa baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, NEC ilianza kutekeleza programu mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya Mpiga Kura kuwafikia wananchi moja kwa moja kupitia mikutano mikubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, maonesho ya Sabasaba na Nane Nane , kutoa elimu ya Mpiga kura kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na kuzitembelea baadhi ya shule za Sekondari za mkoa wa Singida na Mara.
" Moja ya shughuli za Tume ni kuendesha na kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani nchi nzima kwa upande wa Tanzania Bara, ili shughuli hii tuifanye vizuri ni muhimu sana tuwapatie wananchi elimu sahihi juu ya upigaji wa kura, tutafanya jambo hili tukishirikiana na wadau na Asasi nyingine ambazo tutazipa kibali cha kutoa elimu hii" Amesisitiza Jaji Lubuva.
Jaji Lubuva amebainisha kwamba utoaji wa elimu hiyo utaongeza idadi ya wapiga kura kwenye chaguzi zijazo akitoa mfano wa idadi pungufu ya wapiga waliojitokeza kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na ule uliofanyika Oktoba 25 , 2015 ambapo baadhi ya wananchi walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la Wapiga Kura na kupewa vitambulisho hawakujitokeza kupiga kura.
" Tunalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia umuhimu wa wananchi kushiriki Kupiga Kura, baadhi ya wananchi wamekuwa wakijitokeza ili wapate vitambulisho jambo ambalo sio sahihi, mfano mwaka 2010 wananchi milioni 15 walijiandikisha kupiga kura lakini waliojitokeza kupiga kura ni milioni 8.626 hii ni idadi ya chini, pia mwaka 2015 wananchi waliojiandikisha walikuwa milioni 23,161,440 lakini waliojitokeza Kupiga Kura ni watu milioni 15,589,639 hapa kuna ongezeko, tunaamini tukiwapatia elimu wengi zaidi watajitokeza kuwachagua viongozi wanaowapenda " Amesitiza Jaji Lubuva.
Amesema katika kuendelea kupanua wigo wa utoaji wa elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi wengi zaidi NEC itashiriki Kongamano na maonesho ya Wiki ya Vijana yatakayoambatana na Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2016 Oktoba 7 hadi 14, 2016 mkoani Simiyu ambapo pamoja na Mambo mengine watendaji na Maafisa wa Tume watatoa elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi na kutembelea shule za Sekondari za mkoa huo.
Aidha, ili kuboresha chaguzi zijazo ametoa wito kwa wananchi waendelee kushirikiana na Tume kwa kujitokeza kwa wingi kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa hoja mbalimbali katika maeneo ambayo watendaji wa NEC watafika kutoa elimu ya Mpiga Kura
Amiri
Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa, wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani Septemba 30, 2016.(PICHA NA IKULU) |
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John
Pombe Magufuli na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa
kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo
Septemba 30, 2016

Meli za kivita,
Vifaru vikiwa katika zoezi la Amphibious Landing katika kilele cha maadhimisho
ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini,
Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
Ndege vita
katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kufunga maadhimisho hayo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Baatini ili kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' na kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi kabla ya kwenda kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' na kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kabla ya kuelekea kwenda kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya Askari mbalimbali wa JWTZ walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakati akielekea kwenye bendi ya Jeshi ya Mwenge iliyokuwa ikitumbuiza viwanjani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati bendi ya Jeshi ya Mwenge Jazz ilipokuwa ikitumbuiza kabla ya kufunga rasmi maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani jana. Pembeni yake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimpigia makofi.
Askari mbalimbali wa JWTZ walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia.

wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haji Omar Kheir akilakiwa na makamanda. Nyuma
yake ni Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ Dkt. Abulhamid Yahya Mzee
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akiongea na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Robert Mboma
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiwasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya
kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na
adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya
JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange
alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini
kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na
adui (Amphibous Landing) ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini,
Wilayani Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipowasili kufunga mafunzo
ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa
eneo lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani
Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng.
John Kijazi alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua
ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na
adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya
JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa Dkt Modestus Kipilimba alipowasili kufunga mafunzo ya
medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo
lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani
Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest
Mangu alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua
ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na
adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya
JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Magereza nchini Afande John Casmir Minja alipowasili kufunga mafunzo
ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa
eneo lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani
Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Valentino Mlowola
alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka
ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibious
Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika
kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kaimu Kamishna Mkuu wa Idara ya
Uhamiaji Mama Victoria Lembeli alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya
Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo
lililokaliwa na adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea saluti toka kwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Venance Mabeyo
alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya
kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na
adui (Amphibious Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya
JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Venance Mabeyo
alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini
kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo lililokaliwa na adui (Amphibous
Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika
kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi
mstaafu, Jenerali Robert Mboma alipowasili kufunga mafunzo ya medani ya
Kijeshi ya kutua ardhini kutoka ndani ya maji na kukomboa eneo
lililokaliwa na adui (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Katiba na Sheria Mama Suzana Mlawi
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Majenerali wa JWTZ
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hizo Meja
Jenerali James Mwakibolwa
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuweka saini katika kitabu cha wageni
akishuhudiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiongea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine akisikiliza muhtasari wa zoezi
hilo
Wanadhimu wa zoezi
Sehemu ya wasimamizi wa zoezi hilo
Mkurugenzi Mkuu wa zoezi hizo Meja Jenerali James Mwakibolwa akisoma taarifa
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine akisikiliza muhtasari wa zoezi
hili

Pombe Joseph Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Mstaafu
Jenerali Robert Mboma
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange
kabla ya kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies
Mwamunyange kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la Medani
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi kuelekea kwenye uwanja wa zoezi la
Medani
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na kuelekea kwenye uwanja wa zoezi
la Medani
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa akiwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein

Shein, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange (kulia) na Mkurugenzi
Mkuu wa zoezi hilo Meja Jenerali James Mwakibolwa (kushoto)
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi
(kulia) na mmoja wa washereheshaji Meja BMP Mlunga wakipiga saluti
wakati wa wimbo wa Taifa
Brass band ya JWTZ ikiwa tayari tayari
Mcheza
ngoma hodari wa kikundi cha sanaa cha JWTZ Private Juma Abdulrahman
Juma akikaribishwa jukwaa kuu kupewa zawadi kwa burudani nzuri
iliyooneshwa na kikundi chake
Mcheza
ngoma hodari wa kikundi cha sanaa cha JWTZ Private Juma Abdulrahman
Juma akiendelea kutoa burdani baada ya kukaribishwa jukwaa kuu kupewa
zawadi kwa kazi nzuri iliyooneshwa na kikundi chake
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akimtuza Private Juma Abdulrahman Juma kwa niaba
ya wenzie kwa burudani nzuri.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akimpongexza kwa burudani nzuri Private Juma
Abdulrahman Juma kwa niaba ya wenzie
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein akimtuza Private Juma Abdulrahman Juma kwa niaba ya wenzie
Makamanda wakipiga bastola za miali kuashiria kuanza kwa zoezi hilo la medani
Kazi imeanza....
Ndege vita zikiwa katika fomesheni
Sehemu ya ndege vita
Mpiga picha mwandamizi wa magazeti ya Daily News na Habari Leo Mroki Mroki akiwa kazini kurekodi zoezi hilo
NA K-VIS BLOG
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu
wa Serikali kuhamia Dodoma tangu
nchi hii ipate Uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita, jana Oktoba1, 2016
alifanya ziara kwenye maeneo
mbalimbali ya Manispaa hiyo, ziara ambayo wachambuzi wa mambo
wameelezea ni kujifunza jinsi wakazi wenzake wanavyopambana kuendesha
maisha ili hatimaye aweze kwenda nao sambamba. Maeneo aliyozuru Waziri
Mkuu ni pamoja na sehemu za huduma za jamii kama soko kuu la Majengo,
Hospitali ya Rudaa ya Mkoa, miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu (CDA). Awali kabla ya kufanya ziara hiyo,
Waziri Mkuu alifanya mkutano na viongozi wote wa Manispaa hivyo na
kuwaeleza mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiandaa kupokea watu
zaidi watakaohitaji kuja kuwekeza kwenye Manispaa hiyo. Mapema mwaka
huu, Rais wa
Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dakta John Pombe Magufuli, akitoa
shukrani kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, aliahidi serikali yake
nzima kuhamia Dodoma katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano ili
kuupa hadhi mkoahuo wa kuwa Makao Makuu ya nchi. Kufuatia ahadi hiyo,
Waziri Mkuu alianza kwa vitendo kutekeleza ahadi ya Rais, na kusema yeye
atakuwa kiongozi wa kwanza kuhamia Dodoma. Pichani, Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitembelea moja ya
mabucha ya nyama alipozuru soko kuu la Majengo la Manispaa ya Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu akitembeela soko laMajengo
Kama kawaida ya watanzania wengi siku hizi suala la matumizi ya mbango
kama njia ya kuwasilisha ujumbe wao kwa viongozi wafanyabiashara
hawakuzubaa wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea soko
kuu la manispaa ya Dodoma la majengo Oktoba 1, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelekezo ya kuboresha usafi wa
mazingira ya hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakati alipoitembelea hospitali
hiyo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Bi. Fatuma Yassin wa Swaswa
Dodoma wakati alipotebelea hospitali ya mkoa wa Dodoma Oktoba 1, 2016.
Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma wakishangilia wakati Waziri
Mkuu akitoa hotuba
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma wakishangilia wakati Waziri
Mkuu akitoa hotuba
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akizungumza na watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma baada ya kutembelea
hospitali hiyo Oktoba 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan
Rugimbana
Waziri Mkuu, akitembelea Hospitaliya Rufaa ya Manispaa ya Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wafanyabiashara wa soko Kuu la
manispaa ya Dodoma la Majengo
Waziri Mkuu akitembelea soko kuu la Majengo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana akimkaribisha Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa kuzungumza na wafanyabiashara wa soko kuu la Manispaa ya Dodoma
la Majengo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko kuu
la Dodoma la Majengo
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa skisalimiana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Paskas Mulagili baada ya kuwasili kwenye
nyumba za CDA za Kikuyu.
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akisalimiana na watumishi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu
(CDA) wakati alipokagua ukarabati wa nyumba za CDA za Kikuyu
Nyumba za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) za Kikuyu
zinazokarabatiwa ili zitumiwe na maofisa wa serikali watakaohamia
Dodoma

JOZI LOUNGE YADHAMINI MISS TANZANIA 2016
Club maarufu
kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jijini Dar Es Salaam, imejitokeza hivi
karibuni kujiunga na moja katika kampuni na taasisi zilizokwisha kujitokeza
kudhamini zoezi zima la kutafuta mrembo wa tanzania atakayepeperusha na
kuitangaza Tanzania katika anga za kimataifa katika Nyanja mbalimbali yakiwemo
utalii na huduma ya jamii yenye mahitaji maalum.
Akizungumza
na warembo kutoka mikoa yote Tanzania ambao wanatarajia kuchuana vikali
mwishoni mwa mwezi wa kumi huko jijini Mwanza na hatimaye kumpata mshindi wa
Miss Tanzania 2016, Mkurugenzi wa Jozi Lounge Bw.Dismas Massawe amesema Jozi
Lounge itawadhamini warembo hao kwa kuwapatia malazi, chakula na mahitaji
mengine muhimu kwa kipindi cha siku tatu ambapo jana ilikuwa uzinduzi na leo ni
siku ya semina mbalimbali na siku ya jumapili itakuwa siku ya kusherehekea
ushindi wa mikoa tayari kuelekea katika mapambano ya ngazi ya Taifa.
Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika moja ya pozi jana mara
baada ya kuwasili Jozi Lounge, ambapo watakuwa hapo kwa siku tatu
mfululizo. Jozi lounge ni mojawapo wa wadhamini wa mashindano ya miss
tanzania mwaka huu 2016
Wakipata vinywaji kwa pamoja huku wakifurahia utulivu mwanana ndani ya Jozi Club
Baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016,ambapo jana wameingia kambini pia walipata muda wa kuserebuka ndani ya Club maarufu
kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jiji Dar EsSalaam.
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakiserubuka ndani ya Jozi Club kwa raha zao
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi(kulia), akimkabidhi moja
ya meza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu.(Mwenye suti nyeusi),
kwa ajili ya shule ya sekondari Ikoma iliyoko wilayani huko. TPB imetoa
madawati 50, ikiwa ni pamoja na viti na meza kama msaada wa benki
kusaidia sekta ya elimu nchini. Msaada huo una thamani ya shilingi
milioni 4.
Mkuu wa wilaya. Nurdin Babu, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madawati.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba
Moshingi, akikaribushwa na Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu
kwenye shule ya sekondari Ikoma, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa
madawati.
TPB yachangia madawati Serengeti
Benki
ya Posta Tanzania (TPB) imetoa mchango wa madawati na viti 50 vyote
vikiwa na thamani ya shilingi Milioni Nane kwa Shule ya Sekondari ya
Ikoma, iliyopo Wilayani Serengeti Mkoani Mara. Mchango huo wa madawati
ulikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu na Afisa
Mtendaji Mkuu wa (TPB) Sabasaba Moshingi, kwenye hafla fupi iliyofanyika
shuleni hapo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Sabasaba Moshingi alisema kuwa benki yake
imeamua kutoa viti pamoja na madawati hayo ili kuhakikisha kuwa
wanafunzi wote watakaoanza kutumia shule hiyo hapo mwakani watakaa
kwenye mazingira mazuri yanayofaa. Pia alitoa pongezi nyingi kwa uongozi
wa Kijiji hicho cha Ikoma kwa bidii zao zilizohakikisha kuwa
wanakamilisha ujenzi wa madarasa pamoja na maabara, tayari kwa kupokea
wanafunzi mwaka ujao. Aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi
huo ili kuweza kukabiliana na changamoto nyingine kama vile uhaba wa
nyumba za waalimu na mabweni zinazoendelea kuikabili shule hiyo.
Naye
mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo Mhe. Nurdin Babu aliishukuru Benki ya
Posta kwa msaada huo uliofika wakati muafaka, ambapo shule hiyo
inajiandaa kupokea wanafunzi wapya. Alisema kuwa ni wajibu wa kila
Mtanzania mwenye mapenzi mema kuhakikisha kuwa anatoa kipaumbele kwa
sekta ya elimu ili kuwawezesha watoto wetu kupata elimu kwenye mazingira
mazuri. Alitoa wito kwa taasisi nyingine kuendelea
kuchangia sekta ya elimu hususan shule hiyo, ili waweze kutatua changamoto nyingi zinazoikabili shule hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la JKT Mgulani ambapo
shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam
zilifanyika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Baada ya
kuzindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ambaye aliambatana
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba
na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya
kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan
Mwinyi itakayotumika kumwagilia miti iliyopandwa pamoja na kuongeza na wananchi
walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Gymkana.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka udongo katika mti alioupanda eneo la JKT Mgulani Barabara ya
kilwa wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiunga
na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure
kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
....................................................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 Oktoba 2016 ameongoza mamia ya wakazi wa
mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti
inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam.
Akihutubia
mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya
Kilwa – Kurasini katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es
Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe
vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa
inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora
katika utunzaji wa Manzingira.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini
Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa
asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.
Amesema kuwa
jitihada za kupanda miti nchini zinatakiwa kuimarishwa maradufu kwani zitasaidia
katika uhifadhi wa mazingira hususani katika suala zima la kupambana na athari
za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Makamu wa
Rais katika hotuba yake ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuongezeka hewa
ya ukaa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi
kuwa ya watu hivyo jitihada za pamoja kati ya serikali,taasisi binafsi,asasi za
kiraia na wananchi zinahitajika katika kutunza mazingira na kupanda miti.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia amepongeza
jitihada za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji na uimarishaji
wa mifumo ya maji katika barabara itakayosaidia kurahisisha umwagiliaji wa miti
iliyopandwa.
Amesema anafaraja
na matumaini makubwa kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa
endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio
na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa
Mkutano wa Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la
Mwanza na Geita, unaofanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini
Mwanza.
Mongella
amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa uwazi masuala ya maadili
kwa watumishi wa umma na kwamba yawe ajenda ya kudumu katika ngazi
mbalimbali za utendaji serikalini hususani katika ngazi ya mahakama.
Amesisitiza
mkutano huo kutoka na maadhimio yanayohimiza mahakama kutenda haki na
kuleta manufaa kwa wananchi na kuondokana na malalamiko kwamba mahakama
hazitendi haki katika maamuzi yake.
Mwenyekiti
wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi
Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, chama hicho kinahakikisha
watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa
kutenda haki na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa chombo hicho
katika utoaji wa haki.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.
Na BMG
Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe.Robert Makaramba, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza,
Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe
mkoani Mwanza, akizungumza na wanahabari nje ya mkutano huo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi mkoani
Mwanza, Mhe.Wilbert Martin Chuma, akizungumza kwenye mkutano wa robo
Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu mikoa ya Mwanza na Geita,
unaofanyika leo Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii NSSF mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa mkuatno huo
Katibu wa JMAT
ambaye pia ni Hakimu Mkazi mkoani Mwanza, Bittony Mwakisu (kulia) akiwa
pamoja na Domician Mlashani, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo wilayani
Sengerema na mjumbe wa Kamati tendaji JMAT (kushoto).
Picha ya pamoja
Viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.
Baadhi ya warembo
wakiwasili kwenye Duka na Mgahawa wa Kampuni ya Tomoni Farm, la 'The
Farm Fresh Market', maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam kujionea
shughuli mbalimbali zifanywazo na kampuni hiyo, pia kujipatia chakula
cha mchana.
Mkurugenzi
wa Lino Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundega
akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo mara baada ya idadi
kubwa ya warembo hao kuwasili tayari kuanza kambi rasmi. Kushoto ni Mkuu
wa Itifaki Albert Makoye na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Miss Tanzania,
Deo Captain.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula
na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla, akiwapatia maelezo warembo
hao walipotembelea duka la kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Warembo watakaoshiriki shindano la Miss Tanzania, 2016, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula
na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), nje ya duka la The Farm Fresh Market, Victoria jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), akiwapatia maelezo warembo hao, wakati akiwambeza kwenye sehemu mbalimbali za kampuni hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya warembo wa Miss Tanzania wakiangalia Menu walipofika Mgahawa wa
Kampuni ya Tomoni Farms, Victoria jijini Dar es Salaam.
Washiriki
hao ambao ni washindi kutoka Kanda 9 na mikoa mbalimbali Tanzania
watapokelewa katika Hotel ya Regency Park iliyopo Mikocheni D’salaam, na
baadae watapiga kambi ya siku 4 katika Hotel ya Jozi Lounge iliyopo
Msasani jijini D’salaam.
Mara
baada ya kuingia kambini washiriki hao 30 pamoja na Wasimamizi wao
watakuwa na Semina ya pamoja ambapo watafundishwa masuala mbalimbali
yahusuyo mashindano pamoja na kambi kwa ujumla.
Wakiwa
kambini washiriki hao watafanya ziara katika mikoa ya Dodoma, Singida,
Arusha, Geita na Mwanza kwa shughuli mbalimbali za kijamii.
Kauli
mbiu ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 ni Urembo na Mazingira Safi,
hivyo washiriki wote watafanya kazi mbalimbali kijamii ikiwa ni pamoja
na usafi wa mazingira, kutunza mazingira na pia kushiriki katika
kampeni ya kupanda miti itakayofanyika tarehe 1 Oktoba 2016 nchini pote.
Mashindano
ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 yamekuwa na changamoto kubwa
ya kupata wadhamini wachache waliojitokeza kudhamini mashindano haya
katika mikoa na sehemu mbalimbali.
Tunachukua
fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Wadhamini wote waliojitokeza na
kuchangia kwa njia mbalimbali katika kufanikisha mashindano ya mwaka
huu.
Tunawashukuru
pia washiriki wote katika ngazi zote waliojitokeza kushiriki na pia
shukrani kwa wazazi na walezi walioruhusu watoto wao kushiriki
mashindano ya urembo ya miss Tanzania 2016.
Ni
matarajio yetu kwamba wadau wote wa tasnia hii ya urembo nchini
mtajitokeza kwa wingi katika Fainali za Shindano la Miss Tanzania 2016
linalo tarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2016.
ORODHA YA WAREMBO WA MISS TANZANIA 2016
JINA
|
MKOA/ KITUO
|
KANDA
|
|
DAR CITY CENTRE
UKONGA
TABATA
DAR CITY CENTRE
|
KANDA YA ILALA
|
|
UBUNGO
DAR INDIAN OCEAN
SINZA
SINZA
|
KANDA YA KINONDONI
|
|
LINDI
MOROGORO
MOROGORO
MTWARA
|
KANDA YA MASHARIKI
|
|
DODOMA
SINGIDA
SINGIDA
|
KANDA YA KATI
|
|
IRINGA UNIVERSITY
|
KANDA YA ELIMU YA JUU
|
|
GEITA
MWANZA
GEITA
|
KANDA YA ZIWA
|
|
ARUSHA
KILIMANJARO
TANGA
MANYARA
|
KANDA YA KASKAZINI
|
|
IRINGA
IRINGA
RUVUMA
MBEYA
|
KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
|
.
|
MBAGALA
KIGAMBONI
MBAGALA
|
KANDA YA TEMEKE
|
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waumini
wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya katika Mkutano wa 47 wa jumuiya hiyo nchini
unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha
Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu
awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, anayefuata ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo
nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni katika hotuba yake aliitaka
Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii
kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao
kiroho. (PICHA
NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).
Rais
Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati katika Mkutano wa
47 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa
Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood
Chaudhry. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika
hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika
jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili
yao kiroho
Kiongozi
Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akitoa
hotuba yake katika Mkutano huo wa 47 wa Jumuiya hiyo
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Rais
Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakiwapungia waumini wa Jumuiya ya
Waislamu wa Ahmadiyya (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanawasili katika
Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya
Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masaunia ambaye alikuwa mgeni maalum
katika mkutano huo wa 47 wa jumuiya hiyo nchini, aliitaka Jumuiya hiyo pamoja
na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza
kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu
na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood
Chaudhry
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokea
zawadi ya vitabu vya dini kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa
Ahmadiyya nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry
Sehemu
ya Waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
Taasisi ya
Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, imebainisha kwamba kukosekana
kwa uwajibikaji miongoni mwa baadhi ya viongozi, kunasababisha maendeleo
duni kwenye baadhi ya maeneo/vijiji yenye wawekezaji ikiwemo migodi.
Mkurugenzi wa
taasisi hiyo, Jimmy Luhende, ameyasema hayo leo kwenye mdahalo wa kila
mwezi unaoendeshwa na taasisi hiyo kujadili masuala mbalimbali
yanayohusu rasilimali asilia ikiwemo madini, gesi na mafuta.
Amesema katika
tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo katika vijiji mbalimbali
vinavyozungukwa na migodi katika mikoa ya kanda ya ziwa, wamebaini
kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo zahanati, shule,
miundombinu bora ya barabara pamoja na maji safi na salama.
Amesema taasisi
hiyo imeanzisha midahalo mbalimbali inayowahusisha wananchi pamoja na
viongozi katika vijiji 147 vya mikoa minne ya kanda ya ziwa yenye
uwekezaji wa madini ili kuwajengea uwezo wananchi kutumia uwekezaji ulio
kwenye maeneo yao kurahishisha maendeleo.
Afisa Miradi
(Sheria na Mikataba) kutoka taasisi ya ADLG, Carolina Tizeba, amesema
katika tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo kwenye Vijiji vinne vya
Nyenze, Ikonongo, Songwa na Maganzo katika Wilaya ya Kishapu mkoani
Shinyanga, umebaini kuwepo kwa ushiriki mdogo wa wananchi pamoja na
uwajibikaji wa viongozi wao katika masuala ya uwekezaji wa madini jambo
ambalo linasababisha kushindwa kufuatilia manufaa ya uwekezaji katika
vijiji vyao na hivyo kuchangia kuwepo kwa huduma duni za kijamii katika
vijiji hivyo ambavyo kuna wawekezaji wa madini.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, akizungumza jambo kwenye mdahalo huo uliofanyika Isamilo Jijini Mwanza.
Nicholaus Ngelea ambaye ni Afisa Miradi ADLD, akiwasilisha mada kwenye mdahalo huo uliofanyika Isamilo Jijini Mwanza.
Carolina Tizeba ambaye
ni Afisa Miradi (Sheria na Mikataba) ADLG, akiwasilisha taarifa ya
utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kwenye vijiji vinavyozungukwa na
migodi mkoani Shinyanga.
Washiriki mbalimbali wakiwemo
Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti
mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo
Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti
mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Mshiriki akichangia mada

Washiriki wa mdahalo huo

Bonyeza HAPA Kwa Mdahalo uliopita. Imeandaliwa na BMG.
Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba,
(kushoto), akimkabidhi mfano wa funguo, Waziri Mkuu KassimMajaliwa, ikiwa
niishara ya kumkaribisha Dodoma kama mkazi wa Manispaa hiyo, alipowasili kwenye
makazi yake mjini humo Septemba 30, 2016.Waziri Mkuu ametimiza ahadi yake ya kuhamia Dodoma aliyoitoa bungeni ifikapo mwishoni mwa mwezihuu. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu akionyesha funguo hiyo yamfano baada ya kukabidhiwa
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma
baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30, 2016
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa
kimira na wanawake wa Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika
Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016
Viongozi wa Manispaa na wananchi wakishangilia ujio wa Waziri Mkuu |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokewa na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba na viongozi wengine wa mkoa huo
Waziri
Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake
mjini Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu akiwapungia viongozi na
wananchi wa mkoa wa Dodoma alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma
leo Septemba 30, 3016
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya
Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa Makazi ya Waziri
Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Septemba 30, 2016.
Baadhi
ya Washiriki watakaowania Taji la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika
picha pamoja muda mfupi baada ya kuwasili kambini. Jumla ya Washiriki 30
kutoka kanda mbalimbali nchini wameingia Kambini leo Septemba 30, 2016
tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni
mwa Mwezi ujao.
Mrembo
anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazima
akizungumza na Warembo alipokutana nao leo Septemba 30, 2016 kwenye
Hoteli ya Regency, Jijini Dar es salaam. ambapo jumla ya Washiriki 30
wameingia kambini leo tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo
linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.
Baadhi
ya Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakimsikiliza kwa makini Mrembo
anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazim.
Warembo wakifanyiwa Usaili na viongozi wa Miss Tanzania.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni tano kutoka kwa Mbunge
wa Afrika ya Mashariki ShyroseBhanj ukiwa ni mchango wa waathiri wa tetemeko,
Ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016.Kulia ni Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji , CharlesMwijage.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Hajjat Amina Masenza kwa mchango wa wana Iringa
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi 18,681,000/= kutoka kwa Mkuu
wa mkoa wa Iringa, Hajjat Amina Masenza ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la
ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu
jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Charles Mwijage.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya
sh. 415,800,000/= kutoka Chama cha Waagizaji wakubwa wa
mafuta nchini (TAUMA ) ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la
ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu
jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Tasisi ya Aga khan nchini, Amin Kurji (kulia) ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na wapili kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 80 kutoka kwa Balozi wa Pakistan nchini, Amir Khan (wapili kushoto ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hoteli ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. |
Baadhi
ya watu walioshiki katika tukio la kukabidhi jumla ya shilingi 190
ukiwa ni mchngo wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani
Kagera kutoka kwa balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi
wa China Mhe. Gou Haodong na Taasisi ya Aga Khan wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa alipozungumza baada ya kupokea mchngo huo kwenye hoteli ya
Hyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya upatikanaji wa tiketi za
kieletroniki kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa jadi
Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kushoto ni
Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom Tanzania Bw. Gallius Runyeta.
NA RAYMOND
MUSHUMBUSI WHUS
Mashabiki wa soka nchini wameondolewa wasiwasi kuhusu
upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani
wa Jadi Yanga na Simba na kuhakikishiwa kuwa mfumo wa upatikanaji tiketi uko
vizuri na mpaka sasa tiketi zinaendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali.
Wasiwasi
huo umetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam
kuhusu matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania
Bara kati ya Yanga na Simba.
Waziri
Nape amesema kuwa kuna kuna taarifa kutoka mitaani kuwa kuna uwezekano wa mfumo
huu kutofanya kazi katika mechi hii na malalamiko ya watu wengi
kulalamika kukosa tiketi za mchezo wa kesho.
“kwa
kila anayetaka kwenda uwanjani kesho kadi zinapatikana nimewaagiza Selcom
wahakikishe wanazungusha magari yao mtaani kuangalia mahali
penye upungufu na yawe na watu wenye kadi hizo aidha, watu
waongezwe kwenye vituo ambayo vina idadi kubwa ya wateja wanaohitaji kadi”
Alisema Mhe Nnauye.
Aidha
Waziri Nape Nnauye amewahakikishia watanzania kuwa atausimamia mfumo huu
kikamilifu na kwa gharama yoyote na atahakikisha hautakuwa na
mapungufu na endapo yatajotokeza yatashughulikiwa na wataalamu ili
kuufanya mfumo huu kufanya kazi ipasavyo kama ulivyokusudiwa.
Kwa
upande wake Meneja Mradi kutoka Selcom Tanzania Galius Runyeta amefafanua
kuwa mfumo huu uko wazi kabisa kwa wadau wote wanaohusika na mapato ya uwanjani
na utakuwa njia mbadala ya kudhibiti mapato yatokanayo na mechi.
“ Kwa
mfumo huu hakuna njia ya mkato kila kitu kiko wazi na kwa kila dakika utaona
mabadiliko ya idadi ya tiketi zinazonunuliwa na mpaka sasa zaidi ya tiketi
10,000 zimenunuliwa na zinazidi kununuliwa” Alisema Runyeta.
Kwa
miaka mingi kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa soka nchini kuwepo kwa
upotevu wa mapato katika mechi za ligi na kimataifa katika viwanja vya soka
nchini kwa kuliona hilo Serikali iliamua kuanzisha mfumo utakaomaliza tatizo
hilo na kukomesha mianya yote ya ulaji iliyokuwepo katika mfumo uliopita.
Meneja
Mradi kutoka kampuni ya Selcom Tanzania Bw. Gallius Runyeta akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiendelea na kazi
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini
TANESCO YAFANYA KIKAO CHA UJIRANI MWEMA NA VIONGOZI WA JAMII INAYOZUNGUKA VITUO VYA KUFUA UMEME WA GESI VYA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM
Meneja wa Kituo cha kufua umeme
kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge, akifungua kikao cha ujirani mwema
kati ya TANESCO, TPDC na viongozi wa jamii inayozunguka Vituo vya kufua
umeme wa Gesi vya Kineterezi jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama, TANESCO Makao makuu, Misana Gamba
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme nchini TANESCO na viongozi wa dini, vyombo vya dola na viongozi wa
Serikali za Mitaa sita inayozungu vituo vya kufua umeme wa Gesi asili vya
Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja
kuhakikisha jamii inashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.
Makubaliano
hayo yamefikiwa leo Septemba 30, 2016, kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya
TANESCO, TPDC, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na vyombo vya
dola ili kujadili namna bora ya kulinda miundombinu ya umeme kwenye vituo
hivyo.
“Umeme
wa Gesi ni umeme salama kabisa, hata hivyo ni wajibu wetu kushirikiana pamoja
kuhakikisha miundombinu ya umeme huu wa Gesi inatunzwa na kulindwa,”, Meneja wa
Kituo cha Umeme Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge alianza kwa kusema wakati
akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho.
Tumeona
tuitane hapa leo ili tujadiliane pamoja namna bora ya kuhakikisha umeme huu
utokanao na Gesi ambao Serikali imeiingia gharama kubwa, miundombinu yake
inalindwa na nyinyi viongozi mnao wajibu mkubwa wa kuwafikishia ujumbe wananchi
wanaoishi maeneo yanayozunguka mitambo hii. Alisema Mhandisi Busunge.
Akitoa
mada juu ya Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme wa
Gesi na hasara inayoweza kulikumba taifa na jamii kwa ujumla, Mkuu wa Usalama
wa TANESCO makao makuu, Misana Gamba alisema, “Lazima tutambue kuwa Serikali
imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa vituo hivi na fedha hizi ni za walipa
kodi wa Tanzania, kwa hivyo ni wajibu wetu sote na sio TANESCO pekee
kuhakikisha tunalinda miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,”
alisema Gamba
Akifafanua
zaidi, Mkuu huyo wa usalama alibainisha mambo ambayo jamii inapaswa kuelewa kuwa
ni hatari dhidi ya miundombinu ya umeme ambayo ni pamoja na kuwasha moto,
kulima au kuchimba mchanga, mmomonyoko wa udongo, wezi wa vyuma, uvuvi haramu, kujenga,
kufanya biashara au kuendesha magari makubwa sehemu ambayo miundombinu hiyo ya
umeme wa Gesi inapita.
Mkuu
huyo wa usalama wa TANESCO alisema, hatari inayoweza kutokea endapo mambo hayo
yatafanywa ni pamoja na kurudisha nyuma jiyihada za Serikali katika kuwaletea
umeme wananchi, lakini pia hatari ya kulipuka kwa mitambo hiyo ambapo madhama
makubwa yanaweza kuwakumba wananchi.
Akichangia
kwenye mazungumzo hayo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, ambaye
ndiye alikuwa muendesha kikao, alisema, Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO,
imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme
kwa faida ya Watanzania wote, na hatua ya kikao hicho ni mwendelezo wa utoaji
elimu na kuwataka viongozi hao kuwa mabalozi katika maeneo yao, kwenye nyumba
za ibada, ili kusudi wananchi wengi waelewe umuhimu wa kuunza miundombinu ya
umeme ambayo kimsingi ni mali ya Watanzania wote.
Naye
afisa mwandamizi wa usalama Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC),
Elias Muganda, alitahadharisha juu ya shughuli za kiuchumi kwenye eneo
linakopita bomba la Gesi na ksuema hiyo ni hatari. “Kwa sasa kuna mabomba
mawili yenye Gesi tayari, ambayo yako umbali wa mita 2 kwenda chini, yakipata
mgandamizo unaosababishwa na magari makubwa kupita juu yake inaweza kupelekea
leakge na kusababisha Gesi kuvuja na matokeo yake kila mtu anayajua ni moto.”
Alifafanua
Akatoalea
mfano wa mabomba yaitwayo Carthodic Protection, ambayo huzuia kutu, lakini
tayari kuna watu wanang’oa vyuma hivyo na hii inaweza kusababisha kutu na
mabomba kutoboka,alitahadharisha, Muganda.
Wakichangia
mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kanga, Shamte Mlanzi Mkali,
alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Mitaa, kila wanapokutana kwenye vikao, moja
ya ajenda ya kuzungumza ni pamoja na usalama wa mitambo ya Gesi.
Hata
hivyo viongozi wengi walionyesha umuhimu wa TANESCO kutoa ajira kwa vijana
waishio maeneo ya jirani na mradi ili waweze kuona manufaa ya moja kwa moja ya
ujio wa mradi huo.
Mambo
yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya Gesi iwe
ni moja ya ajenda za vikao vya Serikali za Mitaa, na iwe marufuku kwa mtu
kupita au kukatiza eneo la Mitambo bila ya kibali maalum, uwepo utaratibu wa
kuwaalika viongozi wa TANESCO/TPDC kwenye vikao vya Serikali za Mitaa kama
itahitajika.
Maazimio
mengine ya kikao hicho kilichomuhusisha pia Mkuu wa upelelezi wa Kituo cha Sitakishari-Ukonga,
SSP, Hassan Okello, ni pamoja na kampuni
za ulinzi kwenye eneo la mitambo zijulikane kwa viongozi wa Serikali za mitaa
yote inayozunguka eneo la mradi.
Mitaa
iliyoshiriki kwenye kikao hicho ni pamona na Mtaa wa Kanga, Kibaga, Kinyerezi,
Kichangani, na Kifura.
Mhandisi Busunge
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila
Muhaji (aliyesimama), akizungumzia umuhimu wa viongozi wa mitaa
kushirikiana na TANESCO katika kuelimisha umma, kutunza miundombinu ya
umeme
Afisa Usalama wa TANESCO makao makuu,
Fidelis Almasi, akielezea namna viongozi wanavyoweza kushiriki katika
kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme na athari za
zitokanazo na uharibifu wa miundombinu hiyo kwa jamii na serikali
Mkuu wa upelelezi, Kituo cha polisi Sitakishari-Ukonga, MrakibuMsaidizi
wa Polisi, (ASP), Hassan Okello, akiwatoa hofu viongzoi hao kuhusu
kutunza siri wanapotoa taarifa za wahalifu na uhalifu na kwamba yeye
binafsi yuko tayari siku zote kuhakikisha usalama kwenye eneo hilo
unazingatiwa
Afisa Usalama Mwandamizi wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Eliasi Muganda, amesema, mabomba
mawili ya gesi tayari yana gesi na yako umbali wa kina cha mita 2 kutoka
uso wa ardji na hivyo hayahitaji mgandamizo kutoka juu kwani ni hatari
yanaeza kupata nyufa na kuvujisha Gesi
Afisa Elimu wa Kata ya Kinyerezi,
Mwalimu Mercy Mtei, (kulia), yeye amesema, atawashirikisha walimu na
wanafunzi kueneza ujumbe kwenye jamii
Sheikh Juma Swaleh wa Msikiti wa Othman Bin-Afan wa Kinyerezi
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Niyukuli Leonard (kulia)
Mchungaji Jacob Msami, akizungumza
Ustaadhi Ally akizungumza
Mchungaji Ariel Mungereja wa Kanisa la EAGT, Kinyerezi
Afisa Usalama wa Kituo cha Kinyerezi I,
Furaha Munisi, akifafanua mambo mbalimbali ya kiusalama ambayo viongozi
hao wanapaswa kuyachukua na kuwaelimisha wananchi
Picha ya pamoja baada ya kikao
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna
Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya
Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni
New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo.
Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.
Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE
wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000
alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya Maendeleo Endelevu aliyopewa na
Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.
Tuzo
hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili
wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al
Khalifa.
Akizungumza
jana Dar es Salaam Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa umoja wa mataifa
umeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambao umekuja kupisha yale
malengo 17 ya mileniam ambayo yote yeye alikuwepo, hivyo aliokuwa
wanatoa tuzo walinona kwa namna alivyoshiriki kwa kiasi kikubwa.
"Tuzo hizi si za kuomba, ni watu wanakaa na kupendekeza mtu wa kupewa,
na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza nilipewa mwaka 2009 nchini
Swideni," alisema na kuongeza.
"Tuzo zinatoka kwa niaba ya jamii inayotoka au kuitumikia na kufanya
nayo kazi, hivyo wamatambua mchango wangu katika kuwatumikia wananchi wa
Muleba," alisema.
Aidha Profesa tibaijuka alitaja sababu zilizpokekea yeye kutochua dola 300,000 za Marekeni za tuzo hiyo.
"Sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta hapo mapema, kulikuwa na
uwezekano wa kuichukua lakini nikasema kwa hali halisi ya nyumbani,
hatuna sheria ya kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi nikaicha
mezani wao wafanye wanayotaka," alisema na kuongeza.
"Unapoona mtu kama mimi nafanya kazi nakwenda kuchafulia kwenye kitu
ambacho siusiki nacho, sasa Unapoipokea hapa utaonekana kama umevunja
maadili au umejinufaisha kwa kuwa ndio mambo ya kwetu, hivyo
nikawaachia," alisema.
Aliongeza kwa sasa umeshapeleka mswada binafsi bungeni wa kuweka sheria
ya michango ili vitu vya hiari kama hivi vinapokuja katika jamii
visimamiwe na si kupotoshwa kisiasa.
"Kwa maana jambo hili halina kificho, yaani huwezi kumzungumzia Anna
Tibaijuka bila kutaja suala la Escro, hayo hayakwepeki kwa sababu
yalitengenezwa yakawa hivyo, mtu asiyehusika anavalishwa joho lisilo
muhusu.
"Lakini kwa sababu jamii haina uwezo wa kuchimba chini, unabaki kuwa
uongo na kushindwa kujua ukweli umesimama wapi, lakini wao (UN) wanajua
hii ni propanda la sivyo nisingesimama hapa na tuzo," alisema.
Aliongeza licha ya yeye kuwa mstaafu wa umoja wa mataifa bado
wanamfuatilia katika shughuli za kimaendeleo ambazo anazifanya akiwa
ndani na nje ya nchi.
"Kama ukijikwaa, ukianguka na kusimama watu wanaangalia kulikoni, na huu
ni utamaduni wao, kwa hiyo pale uongo na fitina havina nafasi," alisema
kwa msisitizo wakati akizungumza na wanahabari.
Diwani wa Kata ya Karambi ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Felix Bwahama ambaye
aliongozana na Profesa Tibaijuka alishukuru UN kwa kumtunuku tuzo hiyo
ambapo alisema ni fahari kwa wanakagera na taifa kwa ujumla licha ya
baadhi ya watu nchini kubeza kazi anazizifanya ambazo zinaonekana
kimataifa.
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna
Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya
Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni
New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo.
Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.
Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE
wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000
alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya Maendeleo Endelevu aliyopewa na
Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.
Tuzo
hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili
wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al
Khalifa.
Akizungumza jana Dar es Salaam Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa umoja
wa mataifa umeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambao umekuja
kupisha yale malengo 17 ya mileniam ambayo yote yeye alikuwepo, hivyo
aliokuwa wanatoa tuzo walinona kwa namna alivyoshiriki kwa kiasi
kikubwa.
"Tuzo hizi si za kuomba, ni watu wanakaa na kupendekeza mtu wa kupewa,
na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza nilipewa mwaka 2009 nchini
Swideni," alisema na kuongeza.
"Tuzo zinatoka kwa niaba ya jamii inayotoka au kuitumikia na kufanya
nayo kazi, hivyo wamatambua mchango wangu katika kuwatumikia wananchi wa
Muleba," alisema.
Aidha Profesa tibaijuka alitaja sababu zilizpokekea yeye kutochua dola 300,000 za Marekeni za tuzo hiyo.
"Sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta hapo mapema, kulikuwa na
uwezekano wa kuichukua lakini nikasema kwa hali halisi ya nyumbani,
hatuna sheria ya kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi nikaicha
mezani wao wafanye wanayotaka," alisema na kuongeza.
"Unapoona mtu kama mimi nafanya kazi nakwenda kuchafulia kwenye kitu
ambacho siusiki nacho, sasa Unapoipokea hapa utaonekana kama umevunja
maadili au umejinufaisha kwa kuwa ndio mambo ya kwetu, hivyo
nikawaachia," alisema.
Aliongeza kwa sasa umeshapeleka mswada binafsi bungeni wa kuweka sheria
ya michango ili vitu vya hiari kama hivi vinapokuja katika jamii
visimamiwe na si kupotoshwa kisiasa.
"Kwa maana jambo hili halina kificho, yaani huwezi kumzungumzia Anna
Tibaijuka bila kutaja suala la Escro, hayo hayakwepeki kwa sababu
yalitengenezwa yakawa hivyo, mtu asiyehusika anavalishwa joho lisilo
muhusu.
"Lakini kwa sababu jamii haina uwezo wa kuchimba chini, unabaki kuwa
uongo na kushindwa kujua ukweli umesimama wapi, lakini wao (UN) wanajua
hii ni propanda la sivyo nisingesimama hapa na tuzo," alisema.
Aliongeza licha ya yeye kuwa mstaafu wa umoja wa mataifa bado
wanamfuatilia katika shughuli za kimaendeleo ambazo anazifanya akiwa
ndani na nje ya nchi.
"Kama ukijikwaa, ukianguka na kusimama watu wanaangalia kulikoni, na huu
ni utamaduni wao, kwa hiyo pale uongo na fitina havina nafasi," alisema
kwa msisitizo wakati akizungumza na wanahabari.
Diwani wa Kata ya Karambi ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Felix Bwahama ambaye
aliongozana na Profesa Tibaijuka alishukuru UN kwa kumtunuku tuzo hiyo
ambapo alisema ni fahari kwa wanakagera na taifa kwa ujumla licha ya
baadhi ya watu nchini kubeza kazi anazizifanya ambazo zinaonekana
kimataifa.
Maafisa watatu wa
serikali akiwa Afisa Tawala mkoa wa Kagera, (RAS), Amantius Msole, Mkurugenzi
wa Manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, na meneja wa benki ya CRDB tawi la
Bukoba wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjiniBukoba leo Septemba
29, 2016wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama kwa kufungua akaunti ya bandia
inayofanana na ile inayotumika kukusanya fedha za waathirika wa tetemeko la
ardhi lililotokea mkoani humo Septemba 10, 2016.
RAS Amantius Msole (katikati), na watuhumiwa wenzake wakisindikizwa na maaskari kanzu kuelekea mahakamani leo
Watuhumiwa wakiwa kwenyechumba chamahakama wakisubiri shauri lao
RAS Amantius Msole, (wakwanza kushoto), akijadiliana jambo na wakili wake
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri
Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa
kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo
Septemba 29, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, (kulia-katikati) akiongoza kikao cha Baraza
la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016
Waziri
Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza
la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016. Kushoto ni Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (PICHA NA IKULU)
No comments :
Post a Comment