Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh (kulia) akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi
kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa
Wateja wa kampuni hiyo, Bw. Gaspa Ngowi. Katika kuadhimisha wiki hiyo
StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST
Bollywood na FOX Life.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni
hiyo, Gaspa Ngowi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Kulia ni Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh. Katika kuadhimisha
wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood
Africa, ST Bollywood na FOX Life.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni
hiyo, Gaspa Ngowi akizungumza na wateja walipotembelea kitengo cha
huduma kwa wateja wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa
wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya
tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
Meneja wa Ufundi wa StarTimes Tanzania,
Yusuph Baracha (kushoto) akiwaelekeza wateja walipotembelea chumba cha
kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana kupitia
king’amuzi cha kampuni hiyo wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya
huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua
chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX
Life.
Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes
Kitengo cha Huduma kwa Wateja wakiwahudumia wateja kupitia njia ya simu.
Wateja wa StarTimes pamoja na waandishi wa habari walipata fursa ya
kutembelea kitengo hicho pamoja na cha kurushia matangazo ya chaneli
mbalimbali zinazopatikana kupitia king’amuzi cha kampuni hiyo wakati wa
hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha
wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood
Africa, ST Bollywood na FOX Lif
Na Dotto Mwaibale
KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa
wateja inayosherehekewa duniani kote na makampuni na taasisi mbalimbali
katika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba, StarTimes wamewaletea wateja wake
chaneli mpya ambazo zitanogesha zaidi burudani.
Akizungumza wakati wa hafla fupi
iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh amebainisha
kuwa wanafanya jitihada za kutosha kuhakikisha mkoa yote nchini
inafikiwa na huduma zake.
“StarTimes inajivunia kuwa kinara katika
huduma za matangazo ya dijitali nchini ikiwa na wateja zaidi ya milioni
moja nchi nzima. Mpaka hivi sasa tumekwishaifikia mikoa takribani 17
ambapo hivi karibuni tumezindua huduma zetu mkoani Kigoma na tukiwa
mbioni kuzindua na Mtwara pia.
Mbali na mikoa hiyo lengo kuu ni
kuhakikisha kuwa nchi nzima inafikiwa na huduma zetu ambapo
tutahakikisha tunasambaza maduka na ofisi zetu. Zote hizi ni jitihada za
dhati ambazo kampuni iliahidi katika kuhakikisha kila nyumba ya
mtanzania inafikiwa na huduma za matangazo ya dijitali. Hivyo basi
tumekuwa tukijitahidi kukamilisha dhamira hiyo huduma na bidhaa zetu
zinapatikana kwa bei nafuu ambayo hata mtanzania wa kipato cha chini
anaweza kumudu.” Alisema Luoh
“StarTimes inajivunia kuwa na watoa
huduma takribani 300 ambao wapo tayari kuwahudumia wateja muda wote
kupitia nambari 0764 700 800. Mbali na watoa huduma hao pia kupitia
ofisi zetu na za mawakala wetu wateja pia wanahudumiwa katika ubora ule
ule katika mikoa yote tunayopatikana. Pia tunayohuduma ya baada ya mauzo
ambapo tunao mafundi waliotapakaa katika mitaa mbalimbali ya jiji la
Dar es Salaam kuwafuata wateja walipo. Hii yote inadhihirisha na kwa
namna gani tunavyowajali wateja wetu.” Alihitimisha Mkurugenzi huyo wa
Uendeshaji
Naye kwa upande wake Meneja wa Huduma
kwa Wateja wa kampuni hiyo Gaspa Ngowi ameongezea kuwa ndani ya mwezi
huu wamewaletea wateja wao chaneli mpya ambazo ni ST Bollywood, ST
Bolyywood Africa na FOX Life huku nyinginezo zikiwa njiani kuja rasmi.
“Wiki hii ni maalumu kwa wateja wetu
hususani katika kuonyesha kuthamini mchango wao katika kuunga mkono
huduma zetu. StarTimes inapenda kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja
kwa kuleta chaneli mpya katika ving’amuzi vyake ambazo ni ST Bollywood,
ST Bolyywood Africa ambazo zinaonyesha filamu kali na mpya za kihindi
huku kukiwa na chaguo kwa mtazamaji kuchagua lugha anayoipenda ikiwemo
Kiswahili; na FOX Life ambayo yenyewe inaonyesha filamu na mfululizo wa
tamthiliya za runinga.” Alisema Ngowi
Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja wa
StarTimes alihitimisha kwa kusema kuwa, “Mbali na chaneli mpya pia
tumewaletea bidhaa za runinga na projekta ambazo ndani yake kuna
ving’amuzi ambapo wanaweza kutazama chaneli na vipindi mbalimbali. Hivyo
basi wateja wakae mkao wa kula ili kujipatia bidhaa hizi ziliunganishwa
na mfumo wa dijitali moja kwa moja.”
Katika kusherehekea wiki hii ya huduma
kwa wateja, StarTimes imeadhimisha kwa kuwakaribisha wateja kutembelea
ofisi zake ili kujionea jinsi wanavyoendesha shughuli zao.
Wateja hao walipata pia fursa ya
kutembelea kitengo cha huduma kwa wateja ambapo waliweza kuonana na
kuzungumza moja kwa moja na watoa huduma hao, pamoja na chumba cha
kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana ndani ya
king’amuzi cha kampuni hiyo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet,
John Corse (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya
Embraer 190 kusafirisha abiria. Kulia ni Ofisa Uhusiano na Masoko wa
kampuni hiyo, Lucy Mbogoro.
Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (katikati), akisisitiza jambo
kwenye mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja,
Christina Kausan.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
WANANCHI wametakiwa kuchangamkia usafiri
wa ndege wa Kampuni ya Fast jet baada ya kampuni hiyo kuanza kutumia
ndege mpya aina ya Embraer 190 ambayo ni nafuu zaidi kwa matumizi.
Mwito huo umetolewa na Dar es Salaam leo
na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse wakati akizungumza na
waandishi wa habari jana kuwa ndege hizo ni rahisi kwa matumizi ya
usafiri hapa nchini.
Alisema kuwa ndege hiyo ina uwezo wa
kubeba abiria 108 aliongeza kuwa zitahudumia kwa miezi 6 huku ikitoa
nafasi kwa mafunzo wa marubani wa Fast jet hapa nchini.
Aliongeza kuwa kwa kuwa Fast jet hapa
nchini imepata hasara kiuendeshaji hivyo ndege hizo kwa kuwa hazitumii
matufa mengi itasaidia kuiimarisha biashara.
" Hii imetokea tu kuwa wakati serikali
imeleta aina ya ndege zisizotumia mafuta mengi na sisi tulikuwa pia
tumeshaanza mchakato huo na hivyo kwa sasa binafsi naona kuwa watanzania
watanufaika zaidi" alisema Corse.
Pia aliipongeza serikali kwa kuleta
ndege mpya aina ya Bombardier 8, Q400 ambazo zinaenda mikoa ya Rukwa,
Mara, Kagera na Dodoma ambapo ndege za Fast jet hazifiki.
Alisema kwa kuwa lengo la Fast jet ni
kuwapatia watanzania huduma nafuu za usafiri wa anga hivyo inafurahia
pale ambapo inaona kuwa ndege za serikali zinafika mikoa ambayo Fast jet
haifiki.
Alisema kuwa kwa kupeleka ndege kwenye
mikoa hiyo ni hatua ambayo inatimiza lengo la Fast jet la kuhakikisha
watanzania wanapata huduma bora za anga kwa bei rahisi na kwa wakati.
Snura Mushi
Msemaji wa Msanii Snura Baraka Nyagenda. akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salamm leo.
Msanii Snura Mushi (kulia), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu
kupigwa kwa wimbo wa chura ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui
mazuri ya kitanzania. Kushoto ni Msemaji wake, Baraka Nyagenda.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
N a Dotto Mwaibale
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura wa
msanii Snura Mushi baada ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri
ya kitanzania.
Akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari Dar es Salaam leo, Snura Mushi alisema wimbo wake na video
umeruhusiwa kupigwa baada ya audio ya chura kufanyiwa marekebisho na
kuifanya kuwa katika maudhui ya kitanzania.
Alisema ruhusa hiyo imetolewa kwa barua
iliyoaandikiwa Septemba 26, 2016 yenye kumbukumbu HA.26/375/01'B'/137
ambayo gazeti hili lina nakala yake.
Kupitia mkutano huo msanii Snura Mushi
kwa mara nyingine aliomba radhi kwa watanzania na Serikali kwa ujumla
kwa usumbufu walioupata kwa video yake ya kwanza na kuwaomba waendelee
kuiona video mpya iliyorekebishwa baada ya kuifuta ya kwanza.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitembela Mtaa wa One Way mjini Dodoma Oktoba 5, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea
eneo maarufu la biashara mjini Dodoma la Sabsaba Oktoba 5, 2016. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri mkuu Kassim
Majaliwa ameahidi kukutana na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba mkoani Dodoma
ili kuzungumzia namna ya kulikarabati na kulifanya liwe la kisasa.
Amesema miongoni mwa mambo watakayoyajadili
katika kikao hicho ambacho hakutaja siku ni pamoja na kuboresha mazingira ya
kufanyia biashara hasa kwa wanaouza bidhaa nje ya maduka.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano,
Oktoba 5, 2016) wakati alipotembelea maduka hayo yaliyoko katika barabara ya
One Way inayopita katikati ya barabara ya sita hadi ya 11 pamoja na soko la
Sabasaba akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini
Dodoma.
Amesema Serikali tayari imeshahamia Dodoma hivyo
wafanyabiashara wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuboresha biashara zao ili
waweze kumudu ushindani wa soko.
“Wafanyabiashara lazima mboreshe biashara zenu,
muongeze usafi zaidi na ikiwezekana muimarishe majengo yenu yawe ya kisasa
zaidi kwani haiwezekani maduka ya Makao Makuu ya Nchi yawe katika hali hii,”
amesema.
Pia Waziri Mkuu
amewataka wafanyabiashara hao wasiogope kwenda kukopa katika taasisi mbalimbali
za kifedha kwa lengo la kujiongeza mitaji na kupanua biashara.
Amesema tayari
alishatoa maagizo kwa wamiliki wa benki kuhakikisha wanawawezesha wajasiriamali
wadogo kwa kuwapa mikopo, hivyo aliwataka wasiogope na badala yake wachangamkie
fursa hiyo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mofisa wa Magereza wakati
alipotembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga mjini Dodoma
Oktoba 5, 2016. Wapili kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya Patole,
Auhustine Mrema.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa na Askari Magereza wa
Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga baada ya kulitembelea Oktoba 5,
2016. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Parole Augusine Mrema,
kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma na aliyekaa kushoto ni Mkuu wa
Magereza wa mkoa wa Dodoma, SACP Kirumbi.
Waziri Mkuu akitoka kwenye gereza hilo baada ya kulitembelea.
Askari Magereza wakimsikiliza Waziri mkuu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mofisa wa Magereza wakati
alipotembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga mjini Dodoma
Oktoba 5, 2016. Wapili kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya Patole,
Auhustine Mrema.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa na Askari Magereza wa
Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga baada ya kulitembelea Oktoba 5,
2016. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Parole Augusine Mrema,
kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma na aliyekaa kushoto ni Mkuu wa
Magereza wa mkoa wa Dodoma, SACP Kirumbi.
Waziri Mkuu akitoka kwenye gereza hilo baada ya kulitembelea.
Askari Magereza wakimsikiliza Waziri mkuu
No comments :
Post a Comment