Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kumuaga Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakati akipunga
mkono kwenye ndege yake taryari kwa kuanza safari ya kuelekea nyumbani katika
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam
Oktoba 27, 2016. (PICHA NA IKULU).
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mfalme wa Morocco
Mohamed VI mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfalme wa
Morocco Mohamed VI kabla ya kuagana nae katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mfalme wa
Morocco Mohamed VI wakiangalia bendi ya matarumbeta iliyokuwa ikitumbuiza
katika ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
AKAUNTI ZA LAKE FM MWANZA NA WAFANYAKAZI WAKE ZATOWEKA HEWANI.
Ikiwa yamebaki masaa machache kuelekea
kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na Lake Fm redio ya
Jijini Mwanza, akaunti ya Instagram ya redio hiyo imevamiwa na watu
wanaosadikika kuwa ni wahuni wa mtandaoni.
"Siku hizi mitandao ya kijamii ina nguvu
sana hususani kwenye kusambaza habari, hivyo nadhani wameamua kuingilia
akaunti yetu baada ya kuona namna ambavyo tunaitangaza show ya Usiku wa
Mshike Mshike inayofanyika leo". Uongozi wa Lake Fm umefafanua na
kuongeza;
"Tunapenda kuwaambia Wananzengo wetu
kwamba show hiyo itafanyika kama kawaida na tayari Khadija Omar Kopa
amewasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kuwapa burudani hivyo wasishtuke
kutoona posts zetu kwenye mtandao wa Instagram kwani tunapatikana
Facebook na Twitter @lakefmmwanza".
Mbali na akaunti ya redio kuibiwa, pia
akaunti za Instagram za wafanyakazi wa redio hiyo pamoja na wasikilizaji
wake waliokuwa wakipost kuhusu show ya Mshike Mshike zimeibiwa.
Show ya Mshike Mshike inafanyika leo
alhamisi Oktoba 27,2016 katika kiwanja cha nyumbani Villa Park Rerort
kuanzia saa moja jioni kwa kiingilio cha shilingi 7,000 kabla ya saa
tano usiku na shilingi elfu kumi baada ya saa tano usiku ambapo bendi ya
Ogopa Kopa Classic pamoja na wasanii mbalimbali akiwemo Fatina Khamis
kutoka bendi ya Big Star watakuwepo.
Na BMG
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi
Baadhi ya Wasanii wa kundi la Dar Creators
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwenye tamasha la muziki wa asili lililopewa jina ’Marahaba Swahili Music Festival’ lililofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Biafra na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Dar waliopata burudani mbalimbali za muziki wa ngoma za asili na nyimbo mbalimbali zilizoimbwa (Live).
Mmoja wa Waratibu wa tamasha hilo,Karola Kinasha alieleza lengo lake ni kukuza vipaji vya wasanii chipukizi wanaoimba na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki wa asili,na piia kuutangaza muziki wetu wa asili.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwenye tamasha la muziki wa asili lililopewa jina ’Marahaba Swahili Music Festival’ lililofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Biafra na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Dar waliopata burudani mbalimbali za muziki wa ngoma za asili na nyimbo mbalimbali zilizoimbwa (Live).
Mmoja wa Waratibu wa tamasha hilo,Karola Kinasha alieleza lengo lake ni kukuza vipaji vya wasanii chipukizi wanaoimba na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki wa asili,na piia kuutangaza muziki wetu wa asili.
UONGOZI wa kampuni ya DIRA NEWSPAPER COMPANY LTD wachapishaji
wa gazeti DIRA YA MTANZANIA unamwomba
radhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi na jeshi la wananchi wa
Tanzania kwa ujumla kwa habari iliyochapishwa kwa bahati mbaya katika gazeti
letu; toleo Na.424 la
Juni,20-26 ,2016 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “KIFARU CHA KIVITA
CHA JWTZ CHAIBWA”.</
span>
Tunapenda kueleza kwa
masikitiko kuwa habari hiyo ilichapishwa kwa bahati mbaya baada ya mtayarishaji
wa kurasa (graphic designer) kuipanga habari ambayo ilikuwa haijakamilika
kiuchunguzi na kuiacha iliyotakiwa ichapishwe siku hiyo.
Tunapenda JWTZ na
watanzania wote kwa ujumla kuwa wafahamu kuwa gazeti la DIRA YA MTANZANIA
halikulenga kuchafua Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama ambavyo baadhi
ya watu walivyofikiria. </
span>
Tunafahamu mchango mkubwa
wa jeshi la wananchi wa Tanzania kwa taifa letu na namna jeshi hilo
linavyoshirikiana kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari hasa utoaji wa taarifa
mbalimbali na kamwe jeshi hili tokea kuanzishwa kwake halijawahi kukwaruzana na
vyombo vya habari jambo ambalo ni heshima kubwa kwetu na taifa kwa ujumla.</ div>
Hivyo uongozi wa gazeti
hili umeonelea kuomba radhi kwa Mkuu wa majeshi (CDF), askari wote wa JWTZ na
watanzania wote walioshitushwa na habari hiyo na hasa mkuu wa kikosi cha 83 KJ
cha Kiluvya mkoani Pwani ambaye kikosi chake kilitajwa kama chanzo cha habari
hiyo.
Na tunaomba ifahamike kuwa
tumeomba radhi kwa ridhaa yetu na tunaamini kuwa “kuomba radhi” ni kitendo cha
kiungwana kwa utamaduni wa waafrika na hasa watanzania tuliokulia katika
misingi ya amani, upendo na utulivu na pia tunaamini kuomba kwetu radhi
kutazidisha mahusiano mema na ya karibu kati yetu na JWTZ.
Tunatanguliza
shukrani zetu.</ div>
Musiba
Esaba …………………………..</ div>
Meneja
utawala na Fedha.RPC Salome Kaganda |
Na Dotto Mwaibale
WAMILIKI wa magari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuzima na kufunga milango magari yao pale wanaposimama kwa dharura kupata mahitaji mbalimbali ili kuyanusuru kuibwa.
Mwito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salome Kaganda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu tukio la kuibwa kwa gari la Kapteni Innocent Dallu maeneo ya Mbezi Juu huku akiwemo mtoto wake Lightness.
"Napenda kutumia fursa hii kuwaomba wamiliki wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari ya kuzima magari yao na kufunga milango wanaposimama maeneo yoyote kupata mahitaji yao kwani si rahisi kumbaini mhalifu kwani wapo kila sehemu" alisema Kaganda.
Alisema katika tukio la kuibwa kwa gari la kampteni Dallu alikuwa amesimama maeneo ya Mbezi Juu bila ya kulizima akinunua mahitaji ambapo walitokea vijana wakaondoka na gari hilo aina ya Toyota Harrier baada ya kumtelemsha mmoja wa watoto aliyekuwemo ndani ya gari hilo aitwaye Philip huku wakiondoka na mdogo wake Lightness.
Alisema watuhumiwa hao walimtelekeza mtoto huyo maeneo ya Golden Bridge katika baa moja na kisha kuondoka na gari hilo ambalo lilipatikana baada kukamatwa na polisi Kiwangwa mkoani Pwani ambapo kijana mmoja Ezekiel Daud anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Alisema ni vizuri wamiliki wa magari kuzingatia jambo hilo ili kuepusha matukio kama hayo ambayo yanapoteza muda mwingi wa kuyatafuta kwani tukio kama hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kinondoni ambapo wahalifu waliweza kuiba gari aina ya Noah lililosimamishwa bila ya kuzimwa na kuondoka nalo na alijapatikana mpaka leo hii.
Baada ya kukamilisha zoezi la
Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe
11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo.
Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa utoaji wa
mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu
sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:
I. Vipaumbele vya
kitaifa vinavyoendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha
wataalamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo
ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
i. Uhitaji wa waombaji hususani
wenye mahitaji maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa viungo 118
o Wadahiliwa wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali 87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine 9,867
Jumla 20,183
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa viungo 118
o Wadahiliwa wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali 87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine 9,867
Jumla 20,183
Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
IMETOLEWA
NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
WIZARA YA HABARI YAPOKEA VIFAA VYENYE THAMANI ZAIDI YA SH.MILIONI 20 KUTOKA UBALOZI WA CHINA NCHINI.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akipokea Luninga kutoka kwa
Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Bw Gao Wei
wakati wa makabidhiano ya. Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20
kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili
ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara
hiyo , kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu,
(katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
makabidhiano ya Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka
Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya
maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara
hiyo ,kushoto ni Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw.Gao
Wei, na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi.
NA
SHAMIMU NYAKI-WHUSM.
UBALOZI
wa China nchini umeipatia Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo vifaa vya
ofisi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 ikiwa ni kuendeleza
ushirikiano uliopo baina ya Serikali hizo mbili.
Hatua
hiyo imekuja ikiwa na lengo la kusaidia katika kukuza na kuendeleza sekta ya
sanaa ambayo katika mpango wa miaka mitano ya maendeleo ya Serikiali inatakiwa
kuongeza ajira pamoja na pato la taifa kupitia kazi mbalimbali za sanaa.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu aliushukuru Ubalozi huo kwa mchango wao wa kuhakikisha
sekta ya sanaa inakuwa na kuleta mabadiliko nchini.
“Tunashukuru Ubalozi wa China kwa kutupatia
vifaa hivi ambavyo vitasaidia sana utendaji katika Sekta ya Sanaa ambayo
inaendelea kukua kwa kasi hapa chini na kusaidia kuimarisha ushirikiano mzuri
baina ya Serikali yetu na China”Alisema Bw. Petro Lyatuu.
Naye
Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi huo Bw Gao Wei amesema kwamba
China itaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kuendeleza Sanaa kwa kutoa
misaada mbalimbali kwa kadri
itakavyohitajika.
“Tutaendelea
na ushirikiano huu sio tu kwa kutoa
msaada wa vifaa bali pia kubadilishana uzoefu na taaluma ya Sanaa ili Sekta hii
ikue na kuheshimika na kutambulika rasmi kama ajira ”Alisema Bw Gao.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi
amesema kuwa vifaa hivyo vitaimarisha utendaji kazi wa Sekta ya Sanaa ukizingatia
kuwa ni Sekta ambayo imebeba dhamana kubwa ya kutangaza Sanaa ndani na nje
ya nchi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu wa kwanza kushoto akiangalia “honing
machine” inayotumika kituoni hapo, kulia kwake ni ndugu Firmin Lyaruu na Meneja
wa TEMESA Kilimanjaro Mhandisi Alfred Ng’hwani.
NA
THERESIA MWAMI- TEMESA KILIMANJARO.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA
Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watendaji kuziba mianya ya uvujaji wa mapato, ili
kuhakikisha Wakala unakusanya mapato iliyokusudia na kufanya matumizi stahiki
kwa maendeleo ya Wakala.
Amesema hayo wakati akizungumza na na
watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanajaro alipotembelea na kujionea hali
ilivyo katika kituo hicho na kuwahimiza watumishi wa kufanya kazi kwa juhudi na
maarifa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na kutoa huduma zenye ubora.
“Nawaomba muwe na mbinu mbadala
yakuzuia mianya ya uputevu wa mapato na mzibane Taasisi
mnazozidai walipe madeni ili mapato yatakayokusanywa yasaidie
kuboresha zaidi karakana zetu.” Alisisitiza Dkt. Mgwatu.
Nao watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanjaro
kwa nyakati tofauti, wamemuahakikishia mtendaji huyo kufanya kazi kwa kujituma
na kuzidi kupambana kuipeleka mbele TEMESA ingawa kumekuwapo na ukosefu
wa vitendea kazi kulingana na taaluma mbali mbali zilizopo kwenye
kituo hicho.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko
katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia
utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi
kwa maendeleo ya Wakala huo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akipata maelezo ya utendaji kutoka kwa Meneja wa
TEMESA Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Ng’hwani alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wakwanza
kulia), akiongea na watumishi wa TEMESA Kilimanjaro alipotembelea kituoni hapo
No comments :
Post a Comment