Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakigonga 'cheers' ya
kutakiana kheri na afya njema katika hafla mchapalo ya kusheherekea
miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es
Salaam.
TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI MOI MUHIMBILI JIJINI DAR
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi akifungua rasmi sherehe za
kuadhimisha siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi
Duniani,ambapo alisema wanakazi kubwa ya kutoa matibabu kwa watoto wenye
matatizo ya mtindio wa ubongo na mifupa na mpaka sasa watoto takribani
202 wameshafanyiwa upasuaji na zoezi linaendelea Nchi nzima.
Mwenyekiti
wa chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
Bw. Hakim ambaye nae mtoto wake anamatatizo kama hayo akielezea kuwa
kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa kuwa watu wengi wanahusisha tatizo hilo
na imani potofu, aliongeza kuwa watoto waliofanyiwa upasuaji mkoa wa
Mbeya ni 18, Morogoro 12, Mwanza 50, na Izazi 14. na wamefanikiwa kuokoa
Maisha ya watoto 185 katika mikoa 16 Tanzania.
Meneja wa Nakiete akitoa neno wakati wa Maadhimisho hayo
Mmoja wa wazazi akiwa na Mwanae mwenye tatizo la Kichwa kikubwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi (Kushoto) akipokea Msaada kutoka Duka la madawa la Nakiete
Madam Sophia Mbeyela (Kulia) akitoa msaada kwa watoto hao
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao wenye vichwa vikubwa
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi wapili kutoka kushoto akipokea
Msaada viti 15 vya kutembelea 'wheel chair' watoto kutoka kwa Mohamed
Punjan Foundation
Baadhi ya wauguzi wakiwa katika maadhimisho hayo
Baadhi ya wazazi na walezi na wazazi wenye kichwa kikubwa na Mgongo wazi wakiwa katika maadhimisho hayo.
Picha zote na Fredy Njeje
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo,
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Usafirishaji wa
mbolea kwa njia ya Reli TRL, Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye Ofisi
za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani.
Azungumzia uzinduzi huo Mkurugenzi huyo alisema kuwa YARA kwa
kushirikiana na TRL na SAGCOT, wameamua kuzindua njia hiyo ya
usafirishaji ili kupunguza gharama za usafirishaji kwa kutumia barabara
na maji ili kuwafikia walengwa kwa wakati na kwa gharama nafuu, ambapo
awali kusafirisha Tani moja kutoka Viwandani Ulaya hadi jijini Dar es
Salaam, ilikuwa ni Dola za Kimarekani 40, kwa Tani moja na Dar es Salaam
hadi Tabora ni Dola za Kimarekani 100 kwa Tani moja kwa njia ya
barabara.
Aidha Macedo, alisema kuwa kuamua kutumia usafiri wa Treni sasa usafiri utashuka kwa asilimia 3
Mfalme
Mohammed wa Morocco akibusu Masahaf kabla ya kumkabidhi Waziri Mkuu
Kasim Majaliwa katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi
wa msikiti kwenye eneo la BAKWATA Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba
25, 2016. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abukary Zubeir. Jumla ya
Masahaf 10000 zilikabidhiwa na Mfalme huyo.(Picha n Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Mfalme
Mhammed wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakishuhudia
wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeir (kulia) akitia saini
Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni
jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine
Shigella(Julia), akiwa na ujumbe wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao
hapa Tanzania, walipotembelea Bandari ya Tanga na kujionea fursa za
uwekezaji hapa nchini.
Kaimu Meneja Bandari Tanga, Hendry Arika, akiwafahamisha mabalozi wa nchi za Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchini wakati walipotembelea Bandari ya Tanga kuangalia fursa za uwekezaji kufuatia ujio wa mradi wa bomba la mafuta Tanga.

Meneja wa Bandari ya Tanga, Hendry Arika akizungumza na waandishi wa
habari leo eneo litakalojengwa bomba la mafuta kijiji cha Chongoleani
Tanga wakati wa ziara ya mabalozi 12 kutoka Jumuiya ya Ulaya
wanaowakilisha nchini zai nchini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Tanga, Daudi Mayeji, akiwaonyesha mabalozi wa nchi 12 za Ulaya wanaoziwakilisha nchini zao nchini ramani ya eneo litakapojengwa bomba la mafuta kijiji cha Chongoleani Tanga ziara waliyoifanya leo.
Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu, Wateja Tigo Pesa kuvuna 6.04bn/- (dola 2,763,636) gawio la kumi la robo mwaka. Kulia ni Meneja Masoko na Usambazaji Huduma za Kifedha wa Tigo, Catherine Rutenge.
Meneja Masoko na Usambazaji Huduma za Kifedha wa Tigo, Catherine Rutenge (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha
ya kidijitali Tigo imetangaza gawio jingine la robo mwaka la shilingi
bilioni 6.04 (sawa na dola za Marekani 2,763,636) kwa watumiaji wa
Tigo Pesa ikiwa ni mara ya kumi katika mfululizo wa kampuni hiyo ya
simu kugawa faida hiyo kwa watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa njia ya
simu.
NA MWANDISHI MAALUM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na India ambayo yamedumu kwa muda mrefu hasa katika sekta mbalimbali ikiwemo za elimu,afya na biashara.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo 25-Oct-2016 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Sandeep Arya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais amesema mahusiano kati ya Tanzania na India yamesaidia kunufaisha wananchi wa nchini mbili hasa katika masuala ya kibiashara,miradi ya maendeleo na hivyo mahusiano hayo ni muhimu yakaendelezwa na kudumishwa.
Makamu wa Rais katika mazungumzo na balozi huyo wa India hapa nchini Sandeep Arya pia ameiomba serikali kuisaidia Tanzania katika mpango utakaosaidia wakulima kupata taarifa mbalimbali zinazohusu kilimo na masoko ya bidhaa zao kupitia simu za mkononi ili kuondoa usumbufu mkubwa wanaopata wakulima kwa sasa hasa kuhusu masoko.
Kwa upande wake, Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya amemhakikishia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan serikali yake itakuwa bega kwa bega na Tanzania katika kuhakikisha wananchi wa pande Mbili wananufaika na mahusiano yaliyopo.
Balozi Sandeep Arya amesisitiza kuwa serikali ya India itaendelea kuisaidia Tanzania katika uimarishaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na miradi ya maendeleo na uimarishaji wa shughuli za kiuchumi.
Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sudan nchini Tanzania Mahgoub Sharfi mazungumzo yaliyolenga pamoja na mambo mengine kuhusu namna ya kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Sudan.

Pichani Makamuwa Rais, akiwa na mazungumzo na Baloziwa Indianchini Tanzania, Sandeep Arya, Ikulu jijini Dar es Salaam, Oktoba 25, 2016. (PICHA NA VPO)
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kushoto)
akipewa ushauri na Mtaalam wa magonjwa ya Saratani ya matiti wa hospitali
ya AAR Dkt. Zacharia Kabona wakati wa zoezi la kuwapima ugonjwa huo wafanyakazi
wa kampuni hiyo uliofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City leo Oktoba 25, 2016
jijinji Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa saratani ya
matiti duniani.
Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania wakipewa ushauri na Mtaalam wa magonjwa ya Saratani ya
matiti wa hospitali ya AAR Dkt. Zacharia Kabona,(kulia) wakati wa zoezi
la upimaji wa ugonjwa huo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo
uliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City leo jijinji Dar es Salaam,
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa saratani ya matiti duniani.
Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania , wakimsikiliza kwa makini Meneja wa mauzo Happiness Shuma
alipokuwa akitoa mada kuhusiana na elimu ya ugonjwa wa saratani ya matiti,
wakati wa zoezi la kuwapima wafanyakazi wa kampuni hiyo lililofanyika makao
makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani city jijini Dar es Salaam,ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa saratani duniani.
Meneja wa mauzo Happiness Shuma akitoa mada kuhusiana na elimu ya ugonjwa wa saratani ya matiti,
wakati wa zoezi la kuwapima wafanyakazi wa kampuni hiyo lililofanyika makao
makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani city jijini Dar es Salaam,ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa saratani duniani.
No comments :
Post a Comment