Wednesday, October 26, 2016

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU YATOA ORODHA MPYA YA WAFAIDIKA 2016/2017






Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:
 I. Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya  Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo                                                 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo                                             118
o Wadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja                                      3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali                     87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele                      6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine                                  9,867
Jumla                                                                                             20,183
Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akipokea Luninga kutoka kwa Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Bw Gao Wei wakati wa makabidhiano ya. Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China  nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo , kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa  Bibi Leah Kihimbi


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China  nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo ,kushoto ni Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw.Gao Wei, na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa  Bibi Leah Kihimbi.

NA SHAMIMU NYAKI-WHUSM.
UBALOZI wa China nchini umeipatia Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo vifaa vya ofisi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 ikiwa ni kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Serikali hizo mbili.
Hatua hiyo imekuja ikiwa na lengo la kusaidia katika kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa ambayo katika mpango wa miaka mitano ya maendeleo ya Serikiali inatakiwa kuongeza ajira pamoja na pato la taifa kupitia kazi mbalimbali za sanaa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo  leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu aliushukuru  Ubalozi huo kwa mchango wao wa kuhakikisha sekta ya sanaa inakuwa na kuleta mabadiliko nchini.
 “Tunashukuru Ubalozi wa China kwa kutupatia vifaa hivi ambavyo vitasaidia sana utendaji katika Sekta ya Sanaa ambayo inaendelea kukua kwa kasi hapa chini na kusaidia kuimarisha ushirikiano mzuri baina ya Serikali yetu na China”Alisema Bw. Petro Lyatuu.
Naye Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi huo Bw Gao Wei amesema kwamba China itaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kuendeleza Sanaa kwa kutoa misaada mbalimbali  kwa kadri itakavyohitajika.
“Tutaendelea na ushirikiano  huu sio tu kwa kutoa msaada wa vifaa bali pia kubadilishana uzoefu na taaluma ya Sanaa ili Sekta hii ikue na kuheshimika na kutambulika rasmi kama ajira ”Alisema Bw Gao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi amesema kuwa vifaa hivyo vitaimarisha utendaji kazi wa Sekta ya Sanaa ukizingatia kuwa ni Sekta ambayo imebeba dhamana kubwa ya kutangaza Sanaa ndani na nje ya  nchi.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu  wa kwanza kushoto akiangalia “honing machine” inayotumika kituoni hapo, kulia kwake ni ndugu Firmin Lyaruu na Meneja wa TEMESA Kilimanjaro Mhandisi Alfred Ng’hwani.

NA THERESIA MWAMI- TEMESA KILIMANJARO.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watendaji kuziba mianya ya uvujaji wa mapato, ili kuhakikisha Wakala unakusanya mapato iliyokusudia na kufanya matumizi stahiki kwa maendeleo ya Wakala.
Amesema hayo wakati akizungumza na  na watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanajaro alipotembelea na kujionea hali ilivyo katika kituo hicho na kuwahimiza watumishi wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na kutoa huduma zenye ubora. 
“Nawaomba muwe na  mbinu mbadala yakuzuia mianya ya uputevu wa mapato na  mzibane Taasisi mnazozidai  walipe madeni ili mapato yatakayokusanywa yasaidie kuboresha zaidi karakana zetu.” Alisisitiza Dkt. Mgwatu. 
Nao watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanjaro kwa nyakati tofauti, wamemuahakikishia mtendaji huyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzidi kupambana kuipeleka mbele TEMESA ingawa kumekuwapo na  ukosefu wa vitendea kazi  kulingana na taaluma mbali mbali zilizopo kwenye kituo hicho.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huo.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akipata maelezo ya utendaji kutoka kwa Meneja wa TEMESA Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Ng’hwani alipotembelea kituoni hapo.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wakwanza kulia), akiongea na watumishi wa TEMESA Kilimanjaro alipotembelea kituoni hapo

POLISI ARUSHA YATOA ONYO JUU YA WAHUSIKA WA BIASHARA YA BANGI

NI KINYUME CHA SHERIA KUMUWEKA MTU NDANI KWA ZAIDI YA MASAA 24

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani linalofanyika mjini Dodoma.

KITENDO cha jeshi la polisi kuwaweka ndani mahabusu zaidi ya saa 24 bila kuwapeleka mahakamani au kuwapa dhamana ni ukiukwaji wa sheria na uvunjifu wa ,katiba ya nchi.

Hayo yalisemwana leo Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa alipokuwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

“Ni kinyume cha sheria kuweka watu ndani zaidi ya muda uliwekwa kisheria. Lakini watanzania wengi hawajua hili…hii inatokana na uelewa finyu wa naswala ya kisheria,” alisema Mchemgerwa, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo liloandaliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF).

Alisema wapo watu ambao wanakutana na matatizo mbalimbali pamoja na kuwekwa ndani bila ya makosa kutokana na kutokujua sheria.

Mchengerwa alisema watu wengi hawajui kama kuna dhamana ya polisi ambapo mtuhumiwa hatakiwi kukaa mahabusu zaidi ya saa 24 bila kupelekwa mahakamani au kupewa dhamana.

Katika kongamano hilo,Mchengerwa alisema watoa msaada wa kisheria wanatakiwa kutoa msaada huo katika kila wilaya hususani maeneo ya mjini na vijijini.

“Wapo watu ambao wako gerezani na hawana kosa lakini kutokana na tatizo la uelewa mdogo wa kisheria wamekuwa wakifungwa.
Abdullkarim Saidi, mmoja watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar akizungumza kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria wa visiwani Zanzibar
“Jamii bado haijui kama kuna dhamana ya polisi pia ni kosa la kisheria kumweka mahabusu mtuhumiwa zaidi ya saa24 bila kumpeleka mahakamani au kumpatia dhamana”alieleza.

Aliwataja wasaidizi wa kisheria kama nguzo muhimu ya kuwasaidia kuelemisha watanzania kuhusu maswala haya ya kisheria na jinsi ya kupata haki zao pindi wanapopatwa na matatizo mbalimbali ya kisheria.

Kwa upande wake mmoja wa watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar, Abdullkarim Saidi alisema licha ya kazi kubwa wanayofanya ya kutoa msaada wa kisheria, wasaidizi wa kisheria nchini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi.
Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Wasaidizi wa Kisheria walioshiriki kongamano hilo linalomalizika mjini Dodoma leo.

Alisema changamoto hizo ni pamoja na kukosekana kwa usafiri pamoja na fedha za kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, na kuongeza kuwa “tunafanya kazi katika mazingira ambayo si rafiki kutokana na kutembea kwa umbali mrefu.”

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa LSF Bw. Kees Groenendijk amesema shirika lake limeweka mikakati madhubuti ya kuwasaidiza wasaidizi wa kisheria waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kifedha na kitaaluma ili waweze kuwasaidia na kuwafikia watanzania wengi zaidi wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.

Kwa mujibu wa Kees, mpaka sasa shirika la LSF limeshatoa zaidi ya shilingi billion 20 kwa mashirika mbalimbali yanajishughulisha na utoaji wa huduma za kisheria—lengo kuu likiwa ni kuwasaidia watanzania 
kupata haki zao.

No comments :

Post a Comment