Saturday, September 10, 2016

ZAIDI YA WATU 10 WAFARIKI KWENYE TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, RAIS MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MKUU WA MKOA WA KAGERA, SALUM KIJUU






NA K-VIS MEDIA
ZAIDI ya watu 10 wanaripotiwa kupoteza maisha leo Septemba 10, 2016 kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 5.7 lililokumba maeneo yanayozunguka ukanda wa Ziwa Victoria, huku Mkoa wa Kagera ukiwa umeathirika zaidi.
Tayari Rais John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Salum Kijuu, kufuatia tetemeko hilo ambalo licha ya kusababisha vifo, lakini pia limeacha nyumba kadhaa zikianguka na zingine kupata nyufa.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa usiku hii imesema, Rais amehuzunishwa sana na maafa hayo na anaungana na wana familia waliopoteza wapendwa wao na kuwatakia walioumia Mungu awaponye haraka.
Mamia ya watu walipelekwa kwenye hospitali ya mkoa wa Kagera kwa ajili ya kupatiwa matibabu huku nyumba kadhaa zikiwa zimeanguka kufuatia tetemeko hilo ambalo kwa mujibu wa kituo cha wanasayansi ya ardhi cha Marekani U.S.G.S, tetemeko hilo ambalo pia limekumba maeneo mengine huko Uganda, lilikwenda umbali wa kilomita 10 chini ya ardhi.
Mji wa Bukoba kwa sasa hauna umeme, ambapo kwa mujibu wa shuhuda mmoja alisema, Tetemeko hilo limepelekea mji mzima kukosa umeme. 

 Mkazi huyu wa Bukoba, akiendesha pikipiki yake mbele ya nyumba iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi lililoukumba mji huo na viunga vyake leo Septemba 10, 2016
Uharibifu wa nyumba uliosababishwa na tetemeko hilo

MKOA WA KAGERA WAKUMBWA NA TETEMEKO LA ARDHI

Watu kadhaa wameripotiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi kupiga katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera hii leo. 

Kufuatia tetemeko hilo, nyumba kadhaa zilibomoka na kuwafukia watu waliokuwa ndani yake huku wengine wakijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali kwa matibabu.
Muonekano wa moja ya barabara mkoani Kagera iliyoharibika kufuatia tetemeko hilo la ardhi. 

Pia imeripotiwa mikoa ya jirani na Kagera ukiwemo mkoa wa Mwanza kukumbwa na tetemeko hilo japo taarifa za madhara bado hazijapatikana.
SOMA ZAIDI »

 Hudson Stanley Kamoga
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala, na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri  akiwemo Muongoza kipindi cha asubuhi cha 360 cha Clouds FM, Bw. Husdon Stanley Kamoga. Akitangaza uteuzi huo Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, amesema Makaibu Tawala, wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa, wakati wakurugenzi walioteuliwa, wanatakiwa kuripoti ofini ya TAMISEMI iliyoko mkoani Dodoma Jumanne Septemba 13, 2016 ili kupatiwa maelekezo zaidi. Taarifa kamili ya Ikulu hiyo hapo chini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Kitema I wilayani Tandahimba waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili kwenye wilaya hiyo ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa kwa burudani ya ngoma wakati akiwasili kwenye makao makuu ya wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa wilaya ya Tandahimba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kiwanda cha kubangua korosho cha AMAMA kilichopo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi na Mdhibiti wa ubora wa bidhaa Bw. Karim Hassan (kushoto) ya hatua mbali mbali ambazo korosho hupitia wakati wa kubanguliwa kwenye kiwanda cha AMAMA kilichopo Tandahimba mkoani Mtwara.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI



Katika kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj siku ya Jumatatu Septemba 12, 2016, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, ametoa msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi laki saba na elfu themanini (780,000), kwa ajili ya Kituo cha kulelea Wazee na Walemavu wasiojiweza cha Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Akikabidhi msaada huo jana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliuhimiza uongozi wa kituo hicho kusimamia vyema ugawaji wa vyakula hivyo li kuwafikia walengwa, ikizingatiwa kwamba kumekuwa kukiibuka malalamiko kutoka kwa wazee wanaoishi katika kituo hicho kwamba misaada ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali imekuwa haiwafikii yote.

Hata hivyo Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Georgina Kwesigabo, alitanabaisha kwamba vyakula na misaana ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali kituoni hapo, yote imekuwa ikiwafikia walengwa wote isipokuwa kuna changamoto ya baadhi yao kuuza misaada wanayopatiwa ikiwemo vyakula, jambo ambalo linaulazimu uongozi wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kusimamia misaada hiyo hususani kuwapikia chakula wanaoishi kituoni hapo badala ya kuwagawia chakula ili wajipikie wenyewe.

Wazee wanaoishi kituoni hapo waliishukuru serikali kwa msaada huo ambapo walisema wanaendelea kumuombea Rais Magufuli na Serikali yake ili iendelee kuboresha kituo hicho ikiweo kuwekewa uzio ili kuondokana na hofu ya kiusalama waliyonayo kwani wakati mwingine wamekuwa wakiibiwa mali zao ikiwemo kuku ambazo wamekuwa wakizifuga.

Vyakula vilitolewa na Mhe.Rais Magufuli ni, mchele gunia sita (kila gunia kilo 50), mafuta ya kupikia madumu manne (kila dumu lita 20) pamoja na mbuzi wawili.
Baadhi ya wazee wanaoishi kwenye Kituo cha Bukumbi, wakifurahia mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya Rais Magufuli kuwapatia msaada wa vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj, itakayofanyika kesho kutwa jumatatu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (mwenye kofia), akimsikiliza mmoja wa wazee katika Kituo cha Wazee Bukumbi.
Mmoja wa akina mama kwenye Kituo cha Bukumbi akiishukuru Serikali kwa msaada wa chakula ilioutoa kituoni hapo
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Sweda (kulia), akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula uliotolewa na Mhe.Rais Magufuli katika Kituo cha Wazee Bukumbi wilayani humo. Alisema Serikali inawajali Wazee wanaoishi katika kituo hicho na kwamba ina upendo kwao ndiyo maana inaendelea kuwahudumia.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Georgina Kwesigabo, alitanabaisha kwamba vyakula na misaana ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhiri mbalimbali kituoni hapo, yote imekuwa ikiwafikia walengwa wote isipokuwa kuna changamoto ya baadhi yao kuuza misaada wanayopatiwa ikiwemo vyakula, jambo ambalo linaulazimu uongozi wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kusimamia misaada hiyo hususani kuwapikia chakula wanaoishi kituoni hapo badala ya kuwagawia chakula ili wajipikie wenyewe.
Vyakula vilivyotolewa na Mhe.Rais Magufuli kwa ajili ya Makao ya Wazee na walemavu wasiojiweza Bukumbi, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Huyu mbuzi, tehe tehe tehe!!
Makao ya Wazee na walemavu wasiojiweza Bukumbi, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BMG


Ofisi za Mikaela Professional Tailors zinapatikana Ghana Green View, barabara ya Airpot Jijini Mwanza. Wapigie kwa nambari 0767 68 28 88 ili wakuhudumie kwa wakati na kwa ubora.

Tofauti na ilivyo katika majiji mengine nchini kama vile Jijini Dar es salaam, Jiji la Mwanza halina mwamko mkubwa katika ubunifu wa mavazi.


Ni kutokana na hali hiyo, Wataalamu na Mabingwa wa Ushonaji wa mavazi ya aina mbalimbali (Kike na Kiume) Jijini Mwanza, Mikalela Professional Tailors, wameahidi kulitambulisha Jiji hilo katika ubunifu wa mavazi ili kuendana na kasi iliyopo katika majiji mengine.

"Awali nilikuwa nateseka sana. Nguo zangu nilikuwa nikishea Jijini Dar au Arusha na nikizivaa watu wengi wakawa wanauliza niliposhonea na kutamani niwapeleke. Nikaona kumbe Mwanza kuna uhitaji mkubwa wa ubunifu na ushonaji wa mavazi hivyo nikaamua kuanzisha kampuni ya ubunifu na ushonaji wa mavazi ya Mikaela Professional Tailor ili kukata kiu hiyo

No comments :

Post a Comment