Thursday, September 22, 2016

WAZIRI WA UJENZI PROFESA MBARAWA ATAKA WADAU WA UJENZI WALA RUSHWA WAFUTIWE LESENI ZAO



Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akihutubia wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Ambwene Mwakyusa akizungumza katika semina hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akipeana mkono na Msaji wa Bodi hiyo Jehad Jehad baada ya kumaliza kutoa hutuba yake.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Taswira meza kuu katika semina hiyo.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mbarawa.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi, Waziri Mbarawa (aliyekaa katikati), Wengine kutoka kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Profesa Mhandisi William Nshana, Mwenyekiti wa Bodi, Ambwene Mwakyusa, Msajili wa Bodi, Jehad Jehad na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili, Dk.Adelina Kikwasi.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa, ameitaka Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuwafutia leseni wadau wa sekta ya ujenzi  watakao bainika kuomba au kupokea rushwa.
Katika hatua nyingine Profesa  Mbarawa ameitaka  Bodi hiyo kuandaa  orodha ya wakadiriaji majenzi na wabunifu  majengo wasiyofuta maadili ya kazi zao ili iwekwe hadharani na wasipate tenda za kufanya kazi popote.
Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo na kueleza kazi yoyote iwe nzuri na bora ni lazima kuepuka rushwa na kufuata  maadili na kanuni za kazi.
“Napenda niwagize bodi kuanzia sasa nataka wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo na wadau wote wa sekta ya ujenzi ambao ni wara rushwa muwafutie leseni zao  ili wasiweze kupata tenda au kutoa tenda.Maadili katika kazi zenu ni jambo la msingi na si vinginevyo,”alisema Profesa Mbarawa.
Mbarawa aliigiza bodi hiyo kuandaa orodha ya watakao kuwa  si waadilifu ili kuonyesha katika jamii kuwa hawa hawasitahili kupewa tenda ya aina yoyote. 

Alisema baada ya kuandaa orodha hiyo  ni vizuri ikatangazwe hata katika vyombo vya habari ili iwe fundisho kwa wengine wenye vitendo hivyo.
Mbarawa aliwataka wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo nchini kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika serikali ya Awamu ya Tano ili kuweza kjiongezea mitaji.
“Kuna mradi wa ujenzi wa Reli ya kiwango cha kisasa unakuja na serikali imetenga Sh. Trilioni 1, lazima kutakuwa na ujenzi wa majengo hiyo ni fursa mbayo mnaweza kuitumia kujiongezea uwezo, lakini kama mtafanya kazi kwa kuungana njia hiyo inaweza kuwasaidia kupata tenda hizo.” alisema.
Awali, akizungumza katika semina hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa, alisema semina hizo zimekuwa na faida kwa wakadiriji majenzi na wabunifu, kwani zinawaongezea uwezo wa kujua mambo mbalimbali na kwamba zimekuwa zikifanyika kila mwaka mara mbili na zimewanufaisha wadau wa sekta ya ujenzi 5,328. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akishuhudia Dereva wa Basi la Tahmeed (kulia) akipimwa kilevi na Trafiki Nuru Mvungi kabla ya Basi lake kuruhusiwa na safari. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akielekea Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani Ubungo, jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria katika Stendi hiyo pamoja na Stendi ya Kibaha mkoani Pwani. Masauni alilizuia Basi la Shambarai lenye namba za usajili T419 BUF na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza kuhatarisha maisha ya abiria. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwauliza abiria wa Basi la Harambee linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, maswali mbalimbali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wakati wanaposafiri. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua mikanda katika Basi la Shambalai wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akioneshwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, tairi la Basi la Shambalai ambalo halina ubora kwa ajili ya kusafirisha abiria. Hata hivyo Masauni aliagiza basi hilo lizuiwe kufanya safari na pia kuchukuliwa hatua kali kwa Mmiliki wa basi hilo pamoja na Dereva. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akizungumza na madereva wa Basi ya mikoani pamoja na wa magari madogo ya mizigo yanayopaki Stendi Kuu Ubungo, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani. Hata hivyo, madereva hao walilalamika kuwa hawana mikataba ya kazi zao. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi hiyo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari, Picha ya Ndege Kibaha, Pwani, mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua mabasi mabovu na usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akihoji usalama wa mtoto baada ya kugundua siti moja kukaa watoto wawili jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MKURUGENZI WA AFRIKA AKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA NCHINI KUZUNGUMZIA USHIRIKIANO

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo kushoto akizungumza katika kikao na Mabalozi wanao ziwakilisha nchi za Afrika hapa nchini. Mazungumzo yao yalijikita katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na nchi zao. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Slipway iliyopo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Septemba, 2016
Sehemu ya Mabalozi kutoka nchi za Afrika wakiwa kwenye Mkutano. Kutoka kulia ni Balozi wa Uganda hapa nchini, Mhe. Doroth Samali Hyuha, akifuatiwa na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Yasser El shawaf na Balozi wa Msumbiji, Mhe. Monica Patricio Mussa
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Bw. Suleiman Saleh wakati wa mkutano kati ya Wizara na Mabalozi wa Afrika waliopo nchini
Mkutano ukiendelea

OFISI YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ YAPOKEA MTAMBO MAALUM WA MAWASILIANO YA NDANI

Meneja Mkuu wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nd. Ali Ibrahim Kilupi kushoto akimkabidhi msaada wa mtambo maalum wa mawasiliano ya Simu za ndani { Inter call } Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza kwa ajili ya Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam. Wa kwanza kutoka Kulia anayeshuhudia tukio la makabidhiano hayo ni Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam Ndugu Issa Mlingoti Ali.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Meza akiuwasilisha msaada huo wa Mtambo wa mawasiliano ya Simu kwa mlengwa Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam Ndugu Mlingoti.
                                                                                         Picha na – OMPR – ZNZ.
 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza alisema jamii na hasa wananchi Wazalendo wenye uwezo wanapaswa kuendelea kujenga tabia ya kusaidia nguvu katika kupambana na changamoto zinazoikabili serikali pamoja na wananchi katika maeneo mbali mbali nchini.

Alisema mfumo uliozoeleza kwa kipindi kirefu sasa katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo ni ule uliotegemewa zaidi wa kupokea misaada kutoka Mashirika, taasisi na mataifa ya nje ya nchi.

Ndugu Joseph Abdulla Meza alitoa kauli hiyo wakati akipokea msaada wa mtambo maalum wa mawasiliano ya ndani { Inter call }kwa ajili ya Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam uliotolewa na Uongozi wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi hafla iliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema wakati umefika kwa wananchi wenyewe kurejesha ari iliyowahi kutekelezwa miaka ya nyuma katika nia ya kujenga nchi kwa kushirikiana kwenye Nyanja zote zinazohusika za kujenga Taifa lenye nguvu za Kiuchumi, maendeleo na ustawi wa Jamii.

{ Tumezoea kupokea misaada kutoka nje ya nchi lakini ni vyema tukapaswa kujenga tabia ya Wananchi wenyewe kusaidia changamoto zinazotukabili sisi pamoja na Serikali yetu “. Alisema Nd. Meza.

Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushukuru Uongozi wa Hoteli ya Kendwa Rocks kwa uamuzi wake wa kusaidia nguvu za kiuwezeshaji changamoto zinazozikabili baadhi ya Taasisi za Umma Nchini.

Mapema Meneja Mkuu wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nd. Ali Ibrahim Kilupi alisema Taasisi yake imeamua kutoa Mtambo huo ili kuwasaidia watendaji wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi

No comments :

Post a Comment