Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha ya mfano wa
Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan
na kupita baharini hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa
Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya
mazungumzo. Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo
kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni
mwakani. (PICHA NA IKULU)
Rais akiagana na balozi huyo wa Korea baada ya mazungumzo yao
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Balozi wa Russia hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo, leo Septemba 22, 2016 |
.

Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo (wa nne kutoka kulia)
akiongoza kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu,
katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo (wa nne kutoka kulia) na
viongozi wengine pamoja na wajumbe wakipata picha ya pamoja baada ya kikao cha
kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa
Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
JONAS
KAMALEKI- MAELEZO
JAJI
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jacob Mwambejele amemkabidhi Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ripoti ya uchunguzi baada
kukamilika kwa uchunguzi huo.
Tukio
hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo ripoti iliyohusu uchunguzi wa
Mgogoro wa muda mrefu kuhusu kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani, Kilosa,
mkoani Morogoro.
Katika
makabidhiano hayo Jaji Mwambejele amesema kwa kushirikiana na timu yake, Wizara
ya Ardhi, Vijiji vya wilayani Kilosa na uongozi wa Mkoa wa Morogoro
wamekamilisha ripoti hiyo ndani ya siku 60 kama adidu za rejea zilivyowataka.
Jaji
Jacob Mwambejele amesema uchunguzi huo uliangalia baadhi ya mambo ikiwemo kama
uanzishwaji wa kijiji cha Mabwegere ulianzishwa kisheria na sheria zilifuatwa
katika uanzishwaji huo, kama ulikuwepo usahihi wa kisheria katika upimaji wa
eneo hilo na kama wanavijiji walishirikishwa, alisema Lukuvi.
Jaji
huyo ameyataja maeneo mengine ya uchunguzi huu kuwa yalikuwa pamoja na
kuchunguza kama upimaji ulizingatia mipaka, kuchunguza maeneo mengine yenye
migogoro na kuchunguza jambo jingine lolote ambalo litasaidia katika kuleta
suluhu ya mgogoro huo.
Kwa
upande wake, Waziri Lukuvi ametoa shukrani zake kwa Jaji Mwambejele na timu
yake, waziri Lukuvi amesema ripoti hiyo imekalika kwa wakati na inataraji
kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 25.
“Mapendekezo
yaliyotolewa ndani ya ripoti ya Jaji, tutayafanyia kazi haraka iwezekanavyo ili
kumaliza mgogoro wa Mabwegere ambao umedumu kwa miaka mingi,” alisema Lukuvi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi mapema mwaka huu
alimteua kwa mamlaka yake chini ya
kifungu 18 (1) cha Sheria ya Ardhi sura 113 Jaji Jacob Mwambejele wa Mahakama
Kuu- Kitengo cha Biashara kuchunguza mgogoro wa Kijiji cha Mabwegere na vijiji
jirani vya Mfuru, Mbigiri, Mandengwa, Dumila , Matongolo na Maboiga vilivyopo
Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro ili kupata suluhisho la kudumu la mgogoro
huo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa
wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita (kulia), akizungumza
katika na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya mtaa
huo iliyofanyika Hoteli ya Best Western Plus Dar es Salaam leo asubuhi.
Kushoto ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta.
Mwenyekiti wa Mtaa
wa Serikali ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita,
akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya tovuti hiyo.
Katibu Tarafa ya Magomeni, Fullgence
Sakafu (katikati), akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya
Kionondoni, aliyekuwa mgeni rasmi, kuashiria uzinduzi rasmi wa tovuti
hiyo. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta,
Mwenyekiti wa mtaa huo, Kimweri Mhita, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Masaki, Richard Mwakyulu na Mjumbe wa Kamati ya Mtaa huo, Rose
Mkisi.
Mkutano na wanahabari ukiendelea kabla ya uzinduzi huo.
Wajumbe wa kamati ya mtaa huo wakishiriki kwenye uzinduzi huo.
Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Peter Mkongereze akizungumza kwenye hafla hiyo.
Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
Mmoja wa waendeshaji wa tovuti hiyo,
Benjamin Chaula (kulia), akielezea jinsi itakavyokuwa ikifanya
kazi.Kushoto ni Norbert Baranyikwa.
Makofi yakipigwa baada ya uzinduzi wa tovuti hiyo.
Katibu Tarafa ya Magomeni, Fullgence Sakafu (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es
Salaam imezindua tovuti yake ili kurahisisha mawasiliano na shughuli za
maendeleo kwa wananchi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa
tovuti hiyo Dar es Salaam leo asubuhi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Masaki, Kimweri Mhita alisema tovuti hiyo imeanzishwa kwa lengo la
kuwasiliana na kuwashirikisha katika shughuli za maendeleo raia wa
kigeni wanaoishi katika mtaa huo.
"Kutokana na jiografia ya eneo letu
kulikuwa na changamoto kuwa ya kuwashirikisha wenzetu katika masuala
mbalimbali kutokana na kutokuwa na mawasiliano tukaona tuanzishe tovuti
yetu itakayosaidia kuondoa changamoto hiyo" alisema Mhita.
Alisema kupitia tovuti hiyo itasaidia
kuwatambua wafanyabiashara waliopo katika mtaa huo ambao wameanza
kujisajili pamoja na wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Tarafa
wa Kata ya Magomeni, Fullgence Sakafu alisema kuanzishwa kwa tovuti
hiyo katika wilaya hoyo wilaya hiyo mtaa huo umeonesha njia hivyo
akaomba mitaa mingine kuiga mfano huo.
Alisema tovuti hiyo itasaidia kuweka
wazi mipango ya maendeleo katika mtaa huo pamoja na kuhimizana kwenye
kampeni ya kufanya usafi inayoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda na kuwa.
Alhaji Adam Kimbisa
NA K-VIS BLOG
MWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya vyombo vya habari vya Chama
Cha Mapinduzi, (CCM), Al-Hajj Adam Kimbisa, amejiuzulu wadhifa wake.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa chama hicho, Christopher Ole
Sendeka na kusambazwa kwa vyombo vya habari leo Septemba 22, 2016, imesema
pamoja na Kimbisa, pia bodi nzima nayo imejiuzulu.
Kimbisa na bodi hiyo, wamechukua uamuzi huo ikiwa ni siku chache
baada ya Rais John Pombe Magufuli, kufanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za
magazeti ya Uhuru na Mzalendo, ambapo pamoja na mambo mengine alikumbana na malalamiko
mengi kubwa ni kuwepo kwa maslahi duni na kushuka kwa morali ya kufanya kazi
ambapo, wafantakazi wa makagazeti hayo, walimueleza Rais Magufuli ambaye pia ni
Mwenyekiti wa chama hicho, kuwa hawajalipwa mishahara kwa zaidi ya miezi
mitano.
Hakuna sababu zaidi zilizotolewa za kujiuzulu kwa mwanasiasa
huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, na Mbunge wa Bunge la
Afrika Mashariki akishika nafasi ya kuwa mwenyekiti wa Wabunge wa bunge hilo
wanaotoka Tanzania.










No comments :
Post a Comment