Monday, September 5, 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI KUSHIRIKI UANGALIZI WA UCHAGUZI WA WABUNGE KATIKA JAMHURI YA SHELISHELI.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Alix Michel.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akimtambulisha Balozi Innocent Shiyo kwa Rais wa Shelisheli, Alix Michel
Rais wa Shelisheli, Alix Michel akiwa kwenye kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Baloz Dk. Augustine Mahiga nchini Shelisheli.

Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ), katika Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. 

Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8 - 10 Septemba, 2016.

Wajibu huu wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa chaguzi za kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa nchini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga (Mb), alizindua  rasmi misheni hiyo tarehe 2 Septemba, 2016 kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya waangalizi itakua na waangalizi kutoka nchi  za SADC .

Wakati akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix  Michel Rais wa Sheliseli .
 Pia Mheshimia Waziri Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel Morgan,  Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychels na kukutana  na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Seychels.

Imetolewa na :

BALOZI  INNOCENT E. SHIYO

RAIS DKT MAGUFULI ALIPOHUTUBIA WANANCHI UWANJA WA DEMOKRASIA ZANZIBAR JUMAMOSI

Viongozi mbalimbali wakiwa wamejipanga kumsubiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mstahiki Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib alipowasili kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wananchi Uchumi na Ushiriuka.Mhe Haroun Ali Suleiman kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikaribishwa na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuhutubianmkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016

KIMBUNGA HERMINE CHAUWA WATU WAWILI MAREKANI

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY AKUTANA KWA MARA YA KWANZA NA VIONGOZI WA DUNIA

Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa May, amekutana kwa mara ya kwanza na viongozi wa mataifa mbalimbali katika mkutano wa G20, tangu achaguliwe kutwaa wadhifa huo baada ya Uingereza kupiga kura ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo mkutano huo uliibua hisia za machungu kwa Uingereza pale rais, Barack Obama, aliposema Uingereza haitapewa kipaumbele cha kwanza katika makubaliano ya kibiashara na Marekani, kufuatia kujitoa Umoja wa Ulaya.
                 Waziri Mkuu Teresa May akisalimiana na rais Vladimir Putin wa Urusi
                         Waziri Mkuu Teresa May akisalimiana na rais Xi Jinping wa China
    Waziri Mkuu Teresa May pia alikutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Saudi Arabia

No comments :

Post a Comment