Monday, September 5, 2016

TUME YA MIPANGO: MWONGOZO WA UWEKEZAJI USAIDIE KUIBUA MIRADI SAHIHI


 Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo baada ya kupata mafunzo juu ya uwekezaji katika miradi ya umma.
 
Naibu Katibu Mtendaji –Uchumi jumla kutoka Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete, akiwaonyesha maafisa mipango kutoka mikoa ya Arusha, Tanga, na Kilimanjaro mwongozo wa kusimamia uwekezaji wa miradi ya Umma.
 Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo. 
 Mhandisi. Arnold Masaki moja ya wakufunzi akieleza jambo kwa washikiri wa mafunzo ya Uwekezaji katika miradi ya umma
Washikiri wa mafunzo ya Uwekezaji katika miradi ya umma wakifuatilia kwa makini mafunzo.

MOTO WA NYIKA WASABABISHA MAELFU KUHAMISHWA HISPANIA

MASHABIKI WAVAMIA UWANJANI NA KUMUANGUSHA NEYMAR MAZOEZINI

Mchezaji nyota wa timu ya Barcelona Neymar amevamiwa na mashabiki akiwa mazoezini nchini Brazil wakati timu ya taifa ikianza mazoezi, kujiandaa na mchezo dhidi ya Colombia.

Vijana wawili walivamia kiwanjani na kumkumbatia kwa furaha kiasi ya kujikuta wakianguka chini na mchezaji huyo ambaye alionekana kutokukerwa na kitendo hicho.
                            Neymar akianguka chini baada ya kukumbatiwa na mashaniki wawili 
   Walinzi na wasaidizi wa timu wakijaribu kuwaondoa mashabiki hao waliomuangusha Neymar
Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro (katikati), akizungumza kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi, iliyofanyika Jijini Mwanza leo.
Na BMG
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewahimiza wananchi kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondomu ili kujiepusha na mimba zisizotarajiwa pamoja na magongwa ya kuambukiza ikiwemo virusi vya Ukimwi.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, ametoa rai hiyo hii leo Jijini Mwanza, kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi.
Katikiro amesisitiza matumizi sahihi na endelevu ya kondom ya Zana kwa wananchi walio kwenye mahusiano ya kimapenzi, yatasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama virusi vya Ukimwi pamoja na mimba zisizotarajiwa na kwamba aina hiyo ya kondom ni imara na yenye ubora.
Mratibu wa mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, mkoani Mwanza, Geofrey Mabu, amesema mkoa wa Mwanza umejipanga vyema ili kuhakikisha kondom za Zana zinawafikiwa walengwa hususani kupatikana bure katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye vituo vyote vya afya, maeneo ya starehe pamoja na kwenye ofisi za serikali na binafsi.
Uzinduzi wa Zana Kondom kitaifa ulifanyika mkoani Mbeya wiki iliyopita ambapo kwa mkoa wa Mwanza uzinduzi utafanyika kesho Jijini Mwanza ambapo aina hiyo ya kondomu itakuwa mbadala wa kondom za MSD zilizokuwa zikitolewa pia bure na Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha mapambano dhidi ya Ukimwi yanafanikiwa
.
Washirki wa semina hiyo
Wanasemina
Wanasemina
Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
Picha ya pamoja

No comments :

Post a Comment