Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Kutoka kwa Mwenyekiti Mwenza
na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa Taasisi ya The
Investment Climate Facility for Africa (ICF), Rais Mstaafu, Benjamin
Mkapa, Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye hoteli ya
Serena jijini Dar Septemba 1, 2016. (PICHA
NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaina na Mwenyekiti
Mwenza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya The Investment
Climate Facility for Africa (ICF), Neville Isdell na Katikati ni Mwenyekiti
Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa ICF, Ris Mstaafu,
Benjamin Mkapa katika hafla ya kuzindua Ripoti ya Hali ya Hewa Barani
Afrika, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016.
Kampuni ya Tigo Tanzania leo imekabidhi madawati 185 yenye thamani ya shilingi milioni 31 yatakayogawiwa shule nne katika mkoa wa Geita ikiwa ni sehemu ya mkakati wake unaoendelea nchi nzima wa kutoa msaada wa madawati ambayo yatainufaisha mikoa 14 bega kwa bega na tamasha la Tigo FIESTA 2016.
Mkakati wa kutoa msaada wa madawati katika msimo huu wa Fiesta unajulikana, “‘Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora; Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Elimu bora, Imooooo!’
Akizungumza katika sherehe za kukabidhi madawati hayo zilizofanyika katika Shule ya Msingi Mwatulole, Meneja wa Kikanda wa Tigo Kanda ya Ziwa Edgar Mapande, alisema umekuwepo uhitaji mkubwa wa madawati katika shule za msingi na kutokana na kuwepo kwa uhaba wa madawati imebainika kuwa ni moja ya sababu zinazoathiri uwezo wa kujifunza pamoja na ufanisi wa masomo miongoni mwa wanafunzi katika shule zetu nyingi za msingi.
“Lengo letu kama kampuni ni kuhakikisha kuwa tunaboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zetu za msingi na tunayo furaha kwamba msimu wa FIESTA 2016 unaleta mabadiliko kwa kizazi cha baadaye ambacho ni wanafunzi walio katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai tena chini sakafuni,” alisema Mapande.
Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyingu ambaye alisema kuwa madawati hayo 185 yataboresha kwa kiwango kikubwa mazingira ya kujifunza kwa watoto katika mkoa huo na kutoa witom kwa watu wengine wenye mapenzi mema kujitokeza na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madawati uliobakia katika mashule mkoani humo.
Kyingu alizitaja shule zitakazonufaika na madawati hayo na idadi yake katika mabano kuwa ni Mwatulole (50), Nyankumbu (45), Ukombozi (45), na Kivukoni (45).
“Tunawashukuru sana Tigo kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza idadi ya uhaba wa madawati katika shule za msingi mkoani Geita. Tunaamini madawati haya 185 yatatufikisha mbali katika kuwawezesha mamia ya watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili ya mafanikio katika kuelekea kuwa viongozi wa baadaye,” alisema Kyingu.
Mradi mkakati wa madawati wa Tigo Fiesta ulianzia mkoani Mwanza na hadi sasa Tigo imeshatoa madawati wilayani Kahama na mkoani Kagera.
Baada ya juzi Agost 30,2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuzindua aina mpya ya Kondomu iitwayo Zana Kondomu mkoani Mbeya, Uzinduzi kama huo unatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza Septemba 05,mwaka huu.
Afisa
Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni (pichani), jana
alisema mkoa wa Mwanza unatarajia kupokea ugeni kutoka wizara hiyo ambao
utajumuisha wataalamu mbalimbali wa afya watakaokuwa wakitoa semina na
elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia vyombo vya habari, wakielezea
juu ya uzinduzi wa kondomu hiyo.
Alisema
miongoni mwa dhumuni la kuzindua aina hiyo mpya ya Kondomu, ni kusaidia
katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukwimwi ambapo
Wizara itakuwa ikigawa bure kondomu hizo zenye ubora kwa wananchi, kote
nchini.
Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni
Baadhi ya Wanahabari mkoani Mwanza, wakimsikiliza Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza.
NA THOMAS NYINDO-TUME YA
MIPANGO
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara, (anayezungumza pichani) amewataka
maafisa mipango na wachumi kuibua miradi ya maendeleo inayotekelezeka ili
kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
Dkt. Ntara amesema miradi mingi inayoibuliwa imekuwa
haitekelezeki na siyo endelevu hivyo kuna haja ya kuzingatia mwongozo wa
uwekezaji wa umma ili kuleta maendelea endelevu katika maeneo yao.
Katibu Tawala amesema hayo katika Mafunzo ya Mwongozo wa
Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma yanayoratibiwa na Tume ya Mipango kwa Maofisa na
watendaji wa Idara za Sera na Mipango wa mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na
Katavi.
Akizungumza katika mafunzo hayo yanayoendelea katika
ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Ntara amesema
maafisa mipango na wachumi wanatakiwa kutoa msaada wa kitaalam kwa uongozi wa
wilaya na mkoa katika kuibua na kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo
yao.
Dkt. Ntara amesema mafunzo hayo yanalenga katika kuleta
mabadiliko chanya katika kuibua, kutekeleza na kufuatilia miradi ya maendeleo.
Amesema fedha za miradi ya maendeleo haziwezi kupatikana
kwa urahisi kama maafisa mipango na wachumi hawataandaa andiko la miradi
kitaalam. “Tunaposhindwa kuibua miradi mizuri, tunashindwa kupata fedha kutoka
serikalini na kwa wafadhili wengine,” alisema Dkt. Ntara.
Awali akimkaribisha Katibu Tawala, Kaimu Naibu Katibu
Mtendaji wa Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, Dkt. Lorah Madete alisema
Serikali imeandaa Mwongozo
wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma (Public Investment Management Operational Manual) kwa lengo la kuimarisha
utendaji, uwajibikaji na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma
zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo.
Dkt. Madete amesema vipaumbele vya Serikali katika miaka
mitano ijayo vimeainishwa kwenye Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano
2016/17 – 2020/21 ambao una lenga zaidi katika kuweka mazingira rafiki ya
uanzishwaji wa viwanda kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya
binadamu. Kwa hiyo mafunzo hayo ni hatua muhimu katika kuboresha, kusimamia utekelezaji,
pamoja ufuatiliaji na kufanya tathmini ya miradi ya maendeleo.
Dkt. Lorah Madete,
Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa
neno kwa Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya
Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi ambao ni washiriki wa mafunzo yanayohusu Mwongozo wa Usimamizi wa
Uwekezaji wa Umma kabla ya
kumkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara (wa pili kushoto) Wengine ni Dkt. Jehovaness
Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na Bibi Rukia S. Manduta, Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu
Mkoa wa Tabora.
No comments :
Post a Comment