Wednesday, September 7, 2016

WAZIRI MKUU AKAGUA MAKAZI YAKE MJINI DODOMA


Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kuhusu ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu, kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Badhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7,2016. Katikati ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KIVUTIO CHA KIMONDO KUENDELEA KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI

WAZIRI MKUU AKIWA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Isimani na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia aliposimama Nangurukuru, wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa njiani kuelekea mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
Sehemu ya Wakazi wa Nangurukuru mkoani Lindi wakishangilia ujio wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia alipowasili kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
                                       .......................................................... 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari ili kudhibiti na tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na kuchangia kupungua kwa samaki baharini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016 wakati akisalimiana na wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi ambao walijitokeza kumsalimia wakati akielekea mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku NNE mkoani huo.
Makamu wa Rais amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya kukabiliana na hali hiyo.
Ameeleza kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli nyingine zikiwemo za utalii.
“Bahari yetu ndio mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu  tumeitumia vibaya mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa mazuri.”
Kuhusu uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zinazolenga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma bora za afya katika ngazi zote.
Amesema mpango huo wa uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda pamoja na utoaji wa elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati wa serikali wa kutoa elimu bure kuanzia wanafunzi darasa  la kwanza hadi kidato cha nne.
Katika ziara yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho 8-Sep-16 atazindua jengo la ofisi  za Tume ya Maadili ya Uongozi wa Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Makamu wa Rais tayari amewasili mkoani Mtwara na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio  mara  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo Septemba 7, 2016. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio (wa pili kulia) akiwa na ujumbe aliofuatana nao mara  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Bibi,Monica Patricio Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais leo,(katikati) Balozi Mdogo wa Msumbiji anyefanyia kazi zake Zanzibae Bw. Jorge Augusto Menezes

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la funguzi wa hotel ya Ramada Encore  yenye hadhi ya nyota 5 jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo Bw. Abdul Ismail.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa hoteli ya Ramada Encore iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli Ramada Encore  Bw. Abdul Ismail wakati wa halfa fupi wa uzinduzi wa Hotel ya Ramada Encore jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua hoteli ya nyota 5 ya Ramada Encore katikati ya jiji la Dar es salaam.

No comments :

Post a Comment