Tuesday, September 6, 2016

UNESCO KUTUMIA BILIONI 3 KUSAIDIA WATOTO WA KIKE KURUDI SHULE

 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akizungumza kuhusu mradi ambao una malengo ya kurejesha watoto wa kike shuleni. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Hashina Begum na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi akizungumza kuhusu mipango ya serikali kukabiliana na tatizo la watoto wa kike kukatishwa masomo.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Hashina Begum akizungumzia sababu ya watoto wa kike kutokuwepo shuleni na jinsi ambavyo UNWOMEN watashiriki katika mradi wa kusaidia watoto wa kike kurudi shuleni.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watu Duniani (UNFPA), Maria Karadenizli akielezea takwimu za watoto wa kike ambao hawapo shuleni. 
 Mkuu wa Ofisi wa Shirika hilo la Maendeleo la (KOICA), Joosung Park akielezea ushiriki wa KOICA katika kusaidia mradi huo kukamilika sawa na mipango iliyowekwa.


Na Mwandishi wetu

Katika kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa shuleni na hatimaye kumaliza masomo yao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetenga Dola 1,605,000 ambazo ni zaidi ya Bilioni 3 za Kitanzania ambayo zitatumika kuwasaidia watoto wa kike nchini kurejea katika shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo.

Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodriguez alisema kuwa Tanzania bado inaonekana kuwa na tatizo la watoto wa kike kuachishwa masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo kupata mimba za utoto na ndoa za utotoni hivyo kupitia mradi huo wataweza kuwasaidia watoto hao kuendelea na masomo.

Bi. Rodriguez alisema UNESCO imeamua kushirikiana na serikali ili kuwasaidia watoto wa kike kurejea masomoni na utafanyika kwa uhakika bila kumwacha mtoto yoyote na wana matumaini utaweza kusaidia watoto wa kike ambao wamekatishwa ndoto zao kimaisha kutokana na kukatishwa masomo.

“Tanzania kuna tatizo la watoto wa kike kusahaulika katika elimu na UNESCO imejitoa kushirikiana na serikali ya Tanzania ili kusaidia kukuza elimu ya watoto wa kike, “Baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kuchangia ni pamoja na mambo ya asili, wamekuwa wakiwaozesha ndoa za utotoni na na watoto wengine wamekuwa wakipata mimba za utoto na hivyo kuacha masomo … mradi huu ni wa uhakika na utasaidia kukuza elimu,” alisema Bi. Rodriguez.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi alisema serikali inafahamu kuwepo kwa changamoto hizo na imekuwa ikifanya jitihada ili kuhakikisha kuwa matatizo ya watoto wa kike kukatishwa masomo yakimalizika.

Alisema kuwa makabila mengi ya Tanzania yamekuwa yakiwaona watoto wa kike kama watu wa kukaa nyumbani na kulea watoto lakini kama jamii ikiwa na mtizamo tofauti na kuwawezesha watoto wa kike basi wanaweza kusaidia nchi kukuza uchumi.

“Tumeona kazi ambayo wameifanya UNESCO hata machifu huko Ngorongoro wameanza kuelewa umuhimu wa watoto wa kike kuwa shuleni na kwa mpango huu matarajio ya serikali ni kumaliza changamoto iliyokuwepo awali,

“Serikali inafahamu kuna changamoto nyingi ambazo zinawakuta watoto wa kike na sio katika elimu pekee bali ni maeneo mengi … serikali inataka kukuza thamani ya elimu kwa watoto wa kike ambao wengi wao wanakatishwa kwa sababu ya mimba na ndoa za utotoni,” alisema Bi. Tarishi.

Nae Afisa Mradi wa Maswala ya Afya ya Uzazi kwa Vijana (UNFPA), Fatina Kiruviya alisema mradi una malengo ya kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa shuleni na kwa kuanza wanataraji kufanya mradi Ngorongoro, Pemba, Geita na Sengerema.




POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imewaonya wazazi kuwa makini na mienendo yawatoto wao, baada ya kubaini baadhiya vijana kuendesha mazoezi ya kareti na matumizi ya silaha misituni.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Polisi (CP), Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, wakati akionyesha “shehena” ya silaha zilizokamatwa na polisi kufuatia operesheni ya kimyakimya inayoendelea hivi sasa kwenye viunga vya jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani.
“Niwaombe wazazi wenzangu kufuatilia mienendo ya vijana wetu, kwani kutofanya hivyo kunaweza kupelekea mzazi kutojuavitendo viovu vinavyofanywa na mototo wako, utakuta watoto wanajifunza kareti na matumizi ya silaha, hii sio dalili njema hata kidogo,” Alionya Kamanda Siro huku akiwaonyesha waandishi wa habari silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi kwenye operesheni hiyo.
Mwezi uliopita, polisi wanne waliuawa kwa kupigwa na risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, kwenye eneo la tawi la benki ya CRDB, Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilifuatiwa na tukio linguine la kuuawa kwa afisa mwandamizi wa polisi wa kikosi cha kudhibiti majambazi, wakati polisi wakiwa kwenye jitihada za kuwasaka wahalifu hao huko Vikindu wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.
Baada ya tukio hilo, polisi walizidisha msako mkali dhidi ya wahalifu hao na hatimaye katika kipindi cha siku 10 tangu kutokea kwa matukio hayo mawili ya kusikitisha,
Polisi ikiwatumia watuhumiwa watatu ambao walikwisha tiwa mbaroni na polisi, na ambao waliwachukua polisi ili kuwapelekea kwenye ngome yao kwenye msitu wa Mbande, ambako wakati wanakaribia eneo hilo, huku polisi wakiwa wamewatanguliza watuhumiwa mbele, walishitukia mashambulizi ya risasi yakielekezwa upande wao na ndipo polsi wakalala chini ili kujihami na mashambulizi hayo na kuwaacha hao watuhumiwa watatu wakishambuliwa na risasi ambapo walipofikishwa hospitali, Daktari alitangaza kuwa wamekwishakufa.
Katika operesheni hiyo, Kamanda Siro anasema, jumla ya bunduki 23 za aina tofauti tofauti zilikamatwa, ikiwa ni pamoja na risasi 835, fulana za kuzuia risasi kupenya mwilini (Bullet Proof), Sare za polisi, pingu 48 na Redio za mawasiliano za polisi (Radio Call) 12.




NA K-VIS BLOG
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, (pichani), amekanusha taarifa kuwa ameomba kujiuzulu wadhifa wake.
Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari kutoka ofisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 6, 2016, imekanusha vikali habari zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii zikisema, Mama Samia amemuandikia barua Rais John Pombe Magufuli, akiomba ajiuzulu wadhifa wake.
“Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla wake kupuuza taarifa hizo ambazo zinalenga kuupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya viongozi wetu,” taarifa hiyo imesema.
Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa, wasambaza taarifa walilenga kuliweka taifa kwenye taharuki na kuwahakikishia wananchi kuwa Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Taarifa hiyo imehitimishwa kwa kuwataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii  na kujiepusha na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu wa nchi.

Hii ni mara pili, Makamu wa Rais kuzushiwa habari ambazo si za kweli. Mnamo Februari 8, 2016, Ofisi ya Makamu wa Rais, ilikanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii kuwa Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, AMEANZISHA SACOS, VICOBA na vitu vingine kama hivyo na kwamba atatoa mikopo kwenye vikundi hivyo.



NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jafo Selemani Said, (picha ndogo kulia) amenusurika kifo baada ya gari lake kugongana na gari dogo eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya.
Polisi wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo ilihusisha gari la Mh. Naibu Waziri aliyekuwa akitokea Tukuyu mkoani humo kikazi, akielekea Mbeya njiani kwenda Dodoma, wakati gari hilo aina ya Toyota lilikuwa likitokea Mbeya kwenda wilayani Rungwe.
Picha zilizopigwa kwenye eneo la ajali, zinaonyesha sehemu iliyogongwa ni upande aliokuwa amekaa Naibu Waziri na kutokana na mshindo wa ajali hiyo, kitufe cha usalama (kinachokaa mbeleya abiria), kilifyatuka ili kumuhami abiria asepatwe na madhara makubwa.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema gari  la Naibu Waziri kulikuwemo watu watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.
Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanyiwa uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa. Hata hivyo taarifa za Daktari zimethibitisha kuwa wote watatu wako salama. Naibu Waziri na wenzake waliruhusiwa kuondoka baada ya uchunguzi huo.

(PICHA KWA HISANI YA  MBEYA YETU)
 Hii ndiyo sehemu ambayo iligongwa, upande ambao Naibu Waziri alikuwa ameketi.
 Polisi wa usalamabarabarani, akifanya uchunguzi sehemu ambayo gari la Mh. Naibu Waziri liliathirika
 Polisi wa usalama barabarani, wakifanya vipimo kwenye eneo la ajali

Gari lililogongana na gari la Naibu Waziri Jafo, likiwa nje ya barabara baada ya ajali hiyo


 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Millicom ambayo ni kampuni Mama ya Tigo Tanzania Mauricio Ramos (Kushoto) akijibu maswali kutoka kwa wafanyakazi wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tigo jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita. Ramos yuko nchini kutembelea kampuni ya Tigo na miradi yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Millicom ambayo ni kampuni Mama ya Tigo Tanzania Mauricio Ramos (Kushoto) akijibu maswali kutoka kwa wafanyakazi wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tigo jijini Dar es salaam. Ramos yuko nchini kutembelea kampuni ya Tigo na miradi yake.  Kushoto kwake ni Mjumbe wa bodi ya Millicom na Mkurugenzi wa uendelezaji vipaji  wa kampuni ya Tigo, Catherine Olak.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Millicom ambayo ni kampuni Mama ya Tigo Tanzania Mauricio Ramos (Kushoto) akijadiliana jambo na wafanyakazi wa Tigo mara baada ya mkutano pamoja nao mapema wa wiki iliyopita.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ,Bi Zainab Telack (aliye vaa ushungi) akiongozwa na Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Elias Kasitila (kushoto kwake) wakati wakielekea uwanja wa Taifa wa mjini Kahama kwa ajili ya makabidhiano ya Madawati kutoka kampuni ya Acacia. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akihutubia wananchi  katika uwanja wa Taifa Kahama wakati wa zoezi la Kukabidhiwa madawati kutoka kwa kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Acacia, Bulyanhulu.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,kutoka kushoto ni Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Elias Kasitila, Afisa Miradi Mzee Hamisi, Afisa Mahusiano ya Jamii William Bundala Chungu pamoja na Afisa Mahusiano ya Jamii David Magege, wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama kabla ya zoezi la Kukabidhi Madawati .
Baadhi ya waandishi wa habari wa  mkoa wa Shinyanga wakichukua taarifa kwa ajili ya kuuabarisha umma juu ya tukio la makabidhiano ya Madawati.
Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia kwa ajili ya shule katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi,Zainab Telack akikata utepe kuashiria kupokea madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia.

Na Dixon Busagaga,Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amekabidhiwa madawati 2,000 yenye thamani ya Shilingi 240,800,000/= na Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Makabidhiano yamefanyika leo mjini Kahama.

Akimkabidhi madawati hayo Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila amesema, “hii ni awamu ya nne kwa mgodi wa Acacia Bulyanhulu kukabidhi madawati ndani ya mwaka huu katika kipindi ambacho taifa linaendelea kutekeleza kampeni ya kitaifa ya dawati kwa kila mwanafunzi iliyoagizwa na Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa lengo la kuboresha mazingira ya elimu nchini Tanzania.”

Ameongeza kuwa, “licha ya Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kuchangia madawati pia inachangia miradi mingine kwenye jamii lakini kwenye sekta ya elimu mgodi unashirikiana na jamii kuitekeleza miradi kama vile ujenzi na ukarabati wa nyumba, ofisi za walimu madarasa, maabara za sayansi na udhamini wa masomo kwa wanafunzi.”

Miradi ya Madawati 2016 kutoka Mgodi wa Acacia Bulyanhulu

  • Mei tulikabidhi madawati 380 kwa Halmashauri ya Msalala yenye thamani ya shilingi  28,500,000/=
  • Juni tulikabidhi madawati 1,000 kwa Halmshauri ya Msalala  yenye thamani ya shilingi 88,500,000/=
  • Julai tulikabidhi madawati 500 kwa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita yenye thamani ya shilingi 37,500,000/=
  • Na hii leo Agosti tunakabidhi madawati 2,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga yenye thamani ya shilingi 240,800,000 /=
  • Aidha mwaka 2013 mgodi wa Acacia Bulyanhulu pia ulikabidhi dawati 1,389 kwa Wilaya ya Kahama
Mchango wa Miradi ya Madawati Kwenye Ajira
  • Katika kipindi cha miezi minne, utengenezaji wa madawati yenye thamani ya shilingi 393,800,000 umewezesha kutolewa kwa tenda za kutengeneza madawati kwa vikundi vya wajasiliamali wadogo na kuwawezesha vijana kujipatia ajira.
  •  
Wanafunzi ambao Wamenufaika
  • Mradi wa Madawati wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu umewaondelea adha jumla ya wanafunzi 5,040 ya kuketi sakafuni wakati wa kupokea  masomo yao, baada ya kupata madawati 3,880 bora ya kudumu ambayo yametengenezwa kwa awamu nne hadi sasa.
  •  
Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu na Sekta ya Elimu Nchini
Mgodi wa Bulyanhulu unaamini kwamba elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii na unaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine wa maendeleo katika ngazi mbalimbali kuendeleza shughuli za uboreshaji wa elimu hapa nchini kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mgodi kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kampuni ya ACACIA, (ACACIA Maendeleo Fund).

Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi Zainab Telack amesema, “ Tukio hili la kukabidhiwa madawati ni tukio kubwa, nimefurahi sana na ninajua furaha ya watoto watakaotuhmia madawati haya itakuwa mara mbili yake, kwa hivyo kwa niaba ya Mkoa wa Shinyanga nawashukuru sana Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kwa kututengenezea madawati elfu mbili, mkoa wa Shinyanga ulikuwa na upungufu wa Dawati elfu 7000 lakini sasa kupitia mchango wa leo kutoka Bulyanhulu na wadau wengine sasa mkoa wetu unamaliza kabisa upungufu wa madawati.”
 

No comments :

Post a Comment