EAC
Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko with H.E. Sahle-Work Zewde,
the Director General of the UN Office in Nairobi outside the EAC
Headquarters in Arusha, Tanzania today
Director
General of the UN Office in Nairobi, H.E. Sahle-Work Zewde, with EAC
Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko outside the EAC Headquarters.
On the left is Ms. Ruphina Mbua Manono, the Political Adviser to the
Director General
EAC
Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko with H.E. Sahle-Work Zewde,
the Director General of the UN Office in Nairobi outside the EAC
Headquarters in Arusha, Tanzania.
SSRA YAWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI
Mkurugenzi
wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akitoa
ufafanuzi mbalimbali kwenye semina ya siku moja ya wanahabari kuhusu
mifuko ya jamii Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na
Uhamasishaji, SSRA, Sarah Kibonde.
Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Tathmini wa SSRA, Ansgar Mushi akitoa mada katika warsha hiyo.
Waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
VIJANA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUONDOKANA NA UMASIKINI
Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi yenye maendeleo na iliyo na watu ambao wamefanikiwa kimaisha, vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikomboa na janga la umaskini lakini pia kulisaidia taifa kupata maendeleo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri wakati akizungumza na vijana ambao wanajifunza ujasiriamali na kuwambia ni vyema wakaongeza bidii katika ndoto wanazotamani kuzifikia ambazo pia zitawasaidia kuondokana na umaskini ambao umekithiri nchini.
Alisema ili mtu kufanikiwa kimaisha haitaji zaidi elimu ya darasani bali ni muhusika mwenyewe kujiongeza kwa kufanya kazi kwa bidii katika jambo ambalo anatamani kulifikia na akiwatolea mfano yeye mwenyewe kuwa tangu amalize masomo yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hajawahi kurudi chuoni kuchukua cheti chake lakini amefanikiwa kimaisha.
"Mimi simchukii mtu ila nauchukia umaskini alionao, ukiwa na juhudi katika biashara na kujituma hata Rais Magufuli hatakufikia mshahara watu wanaweza kusema unafanya biashara ya kawaida lakini inakulipa sana, ni wewe tu na juhudi zako unazofanya ili ufanikiwe,
"Maisha hayana formula kuwa kufanikiwa ni lazima uwe na masters ndiyo upate mafanikio, masters ya maisha ni kuwa mtaani maisha yakupige alafu uinuke upambane na uyashinde hapo ndiyo umeyashinda maisha, ukitaka kufanikiwa lazima ufanye kazi kwa bidii hata mimi natumia muda wangu mwingi kujifunza ili nizidi kufanikiwa," alisema Mashauri.
Aidha Mashauri aliwataka vijana hao kutumia fursa ambayo inatolewa na kampuni yake ya kuuza vifaa vya viwandani ya HiTech International kwa kuwapatia mkopo wa mashine watu ambao wanatamani kufanya biashara za aina mbalimbali ili waweze kufanikiwa kama matajiri wengine wakubwa nchini wamevyofanikiwa.
Nae mwendesha mafunzo kwa vijana hao kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Benny Mwambela alisema mafunzo hayo yameanzishwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ili kuwasaidia vijana kupata mbinu za jinsi gani wanaweza kufanikiwa kibiashara na baada ya mafunzo hayo, wahitimu watakwenda kutoa elimu kwa vijana wengine.
"Tunafundisha walimu ambao watakwenda kufundisha watu wengine kuhusu ujasiriamali, kuna watu wasiopungua 10,000 wamejiandikisha kujifunza ujasiriamali kwahiyo tunawafundisha watu hawa ili wakawafunze na wengine ili na wao wajue jinsi gani wanaweza kufanya biashara,
"Wanafundishwa jinsi ya kubuni wazo la biashara, kuna wengine wana mawazo ya biashara watafundishwa jinsi ya kuanzisha biashara, na kuna wengine wanafanya biashara wanafundishwa jinsi ya kutanua biashara na watafundishwa kuhusu kuanzisha vikundi na jinsi gani ya kutumia fedha," alisema Mwambela.
SERENGETI BOYS WATUA CONGO
Baadhi
ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
- Serengeti Boys, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara
baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda walikopiga kambi
kabla ya kuwavaa vijana wenzao wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016
kwenye dimba la Massamba Sebat, Brazzaville. Timu hiyo imefikia Hoteli
ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini hapa. Kikosi
hicho kimetua salama salmin kujindaa kuifumua Congo Jumapili. (Picha na
Alfred Lucas wa TFF)
Makocha
wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti
Boys, Muharami Mohammed Sultan maarufu kama Shilton (kushoto) anayewanoa
makipa, Kocha Mkuu Bakari Nyundo Shime au Mchawi Mweusi na Mshauri wa
Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya kuwasili Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela
jijini Brazzaville, Congo.
No comments :
Post a Comment