Thursday, September 29, 2016

RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, (kulia-katikati) akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016




Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (PICHA NA IKULU)




SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-
TAREHE:    Jumamosi 01 Oktoba, 2016
MUDA:       02:00 Asubuhi hadi 11:00 jioni
SABABU:   Kujenga laini mpya ya Mburahati na ukarabati wa laini za Tandale Textile ili
                   kuboresha hali ya umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Maeneo yote ya Tandale, Manzese, Sinza Uwanja wa TP, Sinza Vatican, Namnani Hotel, Iteba, Sinza Kijiweni,  Sinza Kumekucha, Sinza Mwika, TTCL Manzese , Urafiki Quarters, Urafiki Textile,TSP Ltd Millenium business, Sinza Lion Hotel, Rombo Sunflower, Strabag compound, Engen petrol station, Masamaki Plastic Bags Ltd pamoja na maeneo ya jirani.
TAREHE:     Jumapili 2 Octoba, 2016
MUDA:       02:00 Asubuhi hadi 11:00 jioni
SABABU:   Matengenezo kwenye Kituo cha Kupozea Umeme Ubungo 33kv ili kuboresha hali 
                    ya umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Parts of Mandela road, I ndustrial area near Mandela road, Ubungo NBC, Tbs  Ubungo, Ubungo Bus Terminal, Parts of  Sinza, Part of Kimara, Baruti,Kimara Kimara Korogwe,Kimara Mwisho, Kimara Matangini, Kimara Mavurunza, Ubungo Maziwa, TTCL Ubungo Kisiwani,  Mabibo,TGNP Mabibo, Mabibo Hostel, Mabibo Jeshini, Mabibo, Makabe, Mpigi Magohe, Goba,Kimara King’ong’o, Tegeta A,Mavurunza, Suka, Stopover, Changanyikeni, Makongo Mwisho pamoja na maeneo ya jirani.
Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo Magomeni 0222171759/66, 0784/0715271461, Kimara Ofisi ya Wilaya 0717/0788379696, Au Kituo cha miito ya simu 2194400 Au 0768 985100.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:  Ofisi ya Uhusiano, TANESCO Makao Makuu                      


Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leoSeptemba 29, 2016, jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa ofisi hiyo Bi. Joy Sawe. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.


Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa wa Ofisi hiyo Daniel Masolwa. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.

(PICHA NA EMMANUEL GHULA)




NA VERONICA KAZIMOTO
PATO la Taifa limekua kwa jumla ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 10.9 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema ukuaji wa pato la Taifa umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, misitu na uvuvi ambapo shughuli  hizo zimekuwa  kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 1.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Kwa upande wa shughuli za uchumi za viwanda na ujenzi, Dkt. Chuwa alisema kumekua  na ongezeko la asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na ukuaji wa asilimia 11.2 mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto.
Aidha shughuli za uzalishaji bidhaa na viwanda zimeongeza kwa asilimia 9.1 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na kasi ya asilimia 5.2 ya mwaka 2015.
Shughuli za uchukuzi na uhifadhi, Dkt. Chuwa amesema kuwa shughuli hizo zimekua kwa kiwango cha asilimia 30.6 zikisababishwa  na usafirishaji wa abiria kwa njia ya reli na barabara ikiwa ni pamoja na usafiri wa UDART.
Vilevile, shughuli za fedha na bima zimeongezeka kwa kasi ya asilimia 12.5 ikilinganishwa na asilimia 10.0 iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa  huduma za elimu zimekua kwa kasi ya asilimia 8.0 katika robo hiyo ya mwaka ikilinganishwa na aslimia 7.4 ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 ambapo ukuaji wa shughuli hii imetokana na ongezeko la wanafunzi waliodahiliwa mwaka 2016.
Kwa upande wa Nchi za Afrika Mashariki ambazo zimeshachambua na kutoa Pato la Taifa katika kipindi kinachoishia Juni 2016 ni Rwanda ambapo Pato halisi la Nchi ya Rwanda katika kipindi cha Aprili – Juni 2016 limeendelea kukua kwa asilimia 5.4 ikilinganisha na asilimia 7.2 ya miezi kama hiyo mwaka 2015.
Takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka hupimwa kwa kutumia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini katika vipindi vya miezi mitatu mitatu ambavyo ni Januari – Machi, Aprili – Juni, Julai – Septemba na Oktoba – Desemba ambapo hujumuisha shughuli zote za kiuchumi, na hutumika katika kutathmini, kupanga mipango na kutayarisha sera za kiuchumi.

Kufuatia changamoto zilizojitokeza katika zoezi la ufungaji wa mashine za kielektroniki zinazojulikana kama Electronic Fuel Pump Printer (EFPP) kwenye Vituo vya kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa na kufuatia agizo la Serikali kuwa wamiliki wa vituo vyote wawe wamefunga mashine hizo ifikapo tarehe 30 Septemba 2016, Wizara ya Fedha na Mipango, Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Chama cha Wamiliki na 

Waendeshaji wa Vituo vya Kuuza Mafuta Nchini (TAPSOA) umekutana na kujadiliana changamoto zilizopo katika zoezi la ufungaji wa mashine za EFPP na  kukubaliana yafuatayo;-

a)Serikali imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya kufunga mashine za EFPP, ili kutoa nafasi kwa TRA ikishirikiana na TAPSOA kutatua changamoto  zilizopo kwa sasa.

b)Wamiliki wa vituo vya kuuza mafuta ambao hawajakamilisha ufungaji wa mashine za EFPP waendelee kutumia mashine za mkono (ETR) mpaka hapo watakapotaarifiwa vinginevyo.

c)TRA inawakumbusha wamiliki wote wa vituo vya kuuza mafuta kuhakikisha kuwa wanatoa stakabadhi za kielektroniki kwa kila mauzo wanayofanya ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwemo adhabu kwa kukaidi agizo hili la kisheria.

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu


Kanisa la EAGT Posta “B” Mabatini Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Lameck Nkumba, linawakaribisha watu wote kwenye mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika katika viwanja vya kanisa hilo vinavyotizamana na geti la polisi Mabatini nyuma ya iliyokuwa Orange Tree Hotel.

Mhubiri wa kitaifa na kimataifa ambaye amehubiri mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Marekani, Canada, Uingereza, Ireland, Wales , Scotland, Ujerumani, Dernmark, Swirtzland, Afrika Kusini, DRC Congo na mengine mengi, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), atahudumu kwenye mkutano huo akishirikiana na wahubiri wengine.

Ni wiki moja yenye miujiza na uponyaji wa nguvu ya Mungu, kuanzia jumapili tarehe 9.10.2016 hadi jumapili tarehe 16.10. 2016 muda ni kuanzia saa 9.00 mchana hadi saa 12 jioni, kila siku.

Waimbaji mbalimbali akiwemo Mwanyamaki kutoka Morogoro, Emannuel Mgogo kutoka Dar es salaam pamoja na kwaya zinatotamba Jijii Mwanza kama vile Havillah Gospel Singers kutoka EAGT Lumala Mpya, na kwaya ya EAGT Posta “B” zitahudumu kwenye mkutano huo.

Ewe baba, mama, kaka, dada, ndugu, jamaa na marafiki, fika kwenye mkutano huo ili ukutane na nguvu ya Mungu ambapo wagonjwa mbalimbali, wenye mapepo, mikosi na waliofungwa na vifungo vya ibirisi watafunguliwa kwa jina la Yesu, bila malipo.
Kwa msaada wa Kiroho, piga simu nambari 0784 43 77 82 
Bonyeza HAPA Kusikiliza, Au Bonyeza Play hapo chini .

Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi yenye maendeleo na iliyo na watu ambao wamefanikiwa kimaisha, vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikomboa na janga la umaskini lakini pia kulisaidia taifa kupata maendeleo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri wakati akizungumza na vijana ambao wanajifunza ujasiriamali na kuwambia ni vyema wakaongeza bidii katika ndoto wanazotamani kuzifikia ambazo pia zitawasaidia kuondokana na umaskini ambao umekithiri nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akizungumza na vijana kuhusu ujasiriamali.
Alisema ili mtu kufanikiwa kimaisha haitaji zaidi elimu ya darasani bali ni muhusika mwenyewe kujiongeza kwa kufanya kazi kwa bidii katika jambo ambalo anatamani kulifikia na akiwatolea mfano yeye mwenyewe kuwa tangu amalize masomo yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hajawahi kurudi chuoni kuchukua cheti chake lakini amefanikiwa kimaisha.
"Mimi simchukii mtu ila nauchukia umaskini alionao, ukiwa na juhudi katika biashara na kujituma hata Rais Magufuli hatakufikia mshahara watu wanaweza kusema unafanya biashara ya kawaida lakini inakulipa sana, ni wewe tu na juhudi zako unazofanya ili ufanikiwe,
"Maisha hayana formula kuwa kufanikiwa ni lazima uwe na masters ndiyo upate mafanikio, masters ya maisha ni kuwa mtaani maisha yakupige alafu uinuke upambane na uyashinde hapo ndiyo umeyashinda maisha, ukitaka kufanikiwa lazima ufanye kazi kwa bidii hata mimi natumia muda wangu mwingi kujifunza ili nizidi kufanikiwa," alisema Mashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaeleza vijana jinsi wanavyoweza kufanikiwa kimaisha kwa kufanya biashara.

Aidha Mashauri aliwataka vijana hao kutumia fursa ambayo inatolewa na kampuni yake ya kuuza vifaa vya viwandani ya HiTech International kwa kuwapatia mkopo wa mashine watu ambao wanatamani kufanya biashara za aina mbalimbali ili waweze kufanikiwa kama matajiri wengine wakubwa nchini wamevyofanikiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaonyesha moja ya mashine ambazo Kampuni ya HiTech International inaziuza.
Nae mwendesha mafunzo kwa vijana hao kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Benny Mwambela alisema mafunzo hayo yameanzishwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ili kuwasaidia vijana kupata mbinu za jinsi gani wanaweza kufanikiwa kibiashara na baada ya mafunzo hayo, wahitimu watakwenda kutoa elimu kwa vijana wengine.
"Tunafundisha walimu ambao watakwenda kufundisha watu wengine kuhusu ujasiriamali, kuna watu wasiopungua 10,000 wamejiandikisha kujifunza ujasiriamali kwahiyo tunawafundisha watu hawa ili wakawafunze na wengine ili na wao wajue jinsi gani wanaweza kufanya biashara,
"Wanafundishwa jinsi ya kubuni wazo la biashara, kuna wengine wana mawazo ya biashara watafundishwa jinsi ya kuanzisha biashara, na kuna wengine wanafanya biashara wanafundishwa jinsi ya kutanua biashara na watafundishwa kuhusu kuanzisha vikundi na jinsi gani ya kutumia fedha," alisema Mwambela.
Na Rabi Hume, MO BLOG
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaeleza vijana jinsi wanavyoweza kuepuka umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii.
Baadhi ya vijana walioshiriki semina hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, waendeshaji wa mafunzo na washiriki wa mafunzo. (Picha zote na Rabi Hume, MO BLOG)
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.Bi Theresa May
Ametoa kiasi cha Paundiza Uingereza Milioni 2.3, sawa na Shilingi za Kitanzania, Bilioni 6 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera PICHA NA IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke kufatia mchango wa Waziri Mkuu wa Uingereza alioutoa kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera kiasi cha Paundi za Uingereza Milioni 2.3 sawa na Takribani Shilingi Bilioni sita za Kitanzania

No comments :

Post a Comment