Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura (kushoto) akionyeshwa vazi lililodariziwa na
mjasiriamali ambaye pia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi.
Elizabeth Matarimo leo jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA: LORIETHA
LAURENCE – WHUSM)
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura (kushoto) akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na mjasiriamali
Bi. Helen Mwamkoa wa Nambua Enterprises Products leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa bidhaa ya vikapu vya asili kutoka kwa
mjasiriamali Bibi. Nicola Boymanda wa Iringa Baskets (kushoto) leo jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth
Matarimo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura (katikati) akisikiliza ufafanuzi kutoka kwa mjasiriamali
Bibi. Potamia Nuena wa PAT designs (kushoto) leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth
Matarimo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura(katikati) akipewa maelekezo kuhusu vikombe mbalimbali
vya ushindi wa maonyesho ya bidhaa kutoka kwa mratibu wa Handproduct of
Tanzania Bw. Eucharius Ng’oge (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa bidhaa ya vikapu vya asili
vilivyotengenezwa kwa kitenge kutoka kwa mjasiriamali Bibi. Flora Mosha wa
Nancy Tailoring Mart (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa
Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao na kikundi cha
wajasiriamali wa Handproduct of Product leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo.
Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo
(kushoto), akiongea wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia), leo jijini Dare s Salaam.
NA LORIETHA LAURENCE.
Wajasirimali na wabunifu wa kazi za mikono nchini wahimizwa kuwa
na hatimiliki ili kudhibiti wizi wa kudurufu bidhaa zao unaofanywa na
baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia James Wambura alipokutana na kikundi cha wajasiriamali
cha Handproduct of Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Anastazia ameeleza kuwa endapo kazi za wajasriamali
zitalindwa kwa kuwa na hatimiliki itasaidia katika kukuza uchumi wao binafsi na
kuongeza pato la Taifa.
“Ni muhimu kulinda kazi za wajasirimali kama ambavyo kazi za
sanaa ya muziki zinavyolindwa kwa kuwa na hatimiliki ili kuwasaidia katika
kulinda haki zao za ubunifu” alisema Mhe. Anastazia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi.
Elizabeth Matarimo ameeleza kuwa kukosekana kwa hatimiliki katika kazi zao
kumeleta changanmoto kubwa na bidhaa feki kutoka kwa wafanyabiashara wa nje
ambao wamekuwa wakidurufu kazi zao na kuuza bidhaa kwa bei nafuu.
Aidha Bibi. Elizabeth aliongeza kuwa changamoto nyingine ni
ukosefu wa eneo la kufanyia maonyesho ya bidhaa zao kitendo ambacho
kinasababisha kukosekana na soko lililoimara kwa bidhaa hizo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Wizara Habari,
Utamduni, Sanaa na Michezo Bibi. Lilian Beleko amesema kuwa kweli changamoto
hizo zipo na wanazifanyia kazi kuwawezesha wajasiriamali hao wa kazi za sanaa
na utamaduni ili waweze kufanya kazi zao kiufanisi.
Kikundi cha Handproduct of Tanzania kilisajiliwa mwaka 2006 na
kinajumisha wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na kazi za mikono
kutengeneza bidhaa mbalimbali za utamaduni na sanaa katika kuenzi utamaduni wa
Mtanzania.
No comments :
Post a Comment