Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.
Suzan Kolimba (katikati), akizungumza na madereva 10 wa Tanzania
waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni waasi Jamhuri ya Demokrasia ya
Conco (DRC), wakati wa hafla fupi ya kuwapokea iliyofanyika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni
Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba na kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Afrika katika wizara hiyo, Balozi Samweli Shelukindo.
Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Mmiliki wa Kampuni ya Simba Logistic
ambayo magari yake na madereva walitekwa, Azim Dewj (kushoto),
akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapokea madereva hao.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisubiri kuchukua taarifa za kuwapokea madereva hao.
Madereva hao wakipokelewa uwanjani hapo.
Madereva hao wakiwa chumba cha mkutano cha uwanja huo wakati wa mapokezi yao.
Dereva Mbwana Said (kulia), akielezea jinsi walivyotekwa.
Dereva Kumbuka Seleman (kulia), akisimulia jinsi alivyotoroka na kutoa taarifa ya kutekwa kwao.
Dereva Athuman Fadhili (kulia),
akisimulia walivyookolewa na majeshi ya Congo na jinsi walivyojificha
porini na kutembea umbali mrefu kwa kutambaa ambapo ilifika wakati
waliomba bora wafe kuliko mateso waliyokuwa wakipata.
Hapa ni furaha ya kukutana na ndugu jamaa na wafanyakazi wenzao.
Picha ya pamoja na viongozi waliowapokea.
Ndugu, Jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzao wakiwa nje ya jengo la VIP uwanjani hapo wakisubiri kuwapokea.
Mapokezi yakiendelea.
Ni furaha ya kukutana na wapendwa wao.
Hapa Dereva Mbwana Said akikumbatia na mjomba wake Kassim Salim katika hafla hiyo kwa Mbwana ilikuwa ni furaha na majonzi.
Mbwana Said (katikati), aamini macho yake baada ya kukutana na mke wake Mariam pamoja na mtoto wake Kauzari.
Na Dotto Mwaibale
MADEREVA 10 wa Tanzania waliotekwa na
watu wanaodhaniwa ni waasi Jamhuri ya Demokraia ya Congo (DRC) wamesema
waliponea tundu la sindano kuuawa.
Kauli hiyo imetolewa na madereva hao
katika hafla ya kuwapokelewa iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo jioni.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mbwana
Said alisema analishukuru jeshi la Congo kwa jitihada kubwa walioifanya
kwa ajili ya kuokoa maisha yao."
" Tunaishukuru serikali ya Congo kwa
kutuokoa kwani tulikuwa katika wakati mgumu na leo kuungana tena na
ndugu zetu" alisema Said.
Alisema walilazimia kutembea kwa muda
mrefu huku risasi zikirindima kati ya majeshi ya serikali na waasi hao
hadi walipofanikiwa kutuokowa kutoka kwenye mikono ya waasi hao.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba aliishukuru serikali
ya Congo kwa jitihada iliyoifanya na kufanikiwa kuwaokoa madereva hao.
Balozi wa Congo nchini Jean Mutamba
aliwataka madereva hao kuacha viza na nyaraka zao ubalozini pindi wanapo
safiri na kurudi ili iwe rahisi kuwatambua pale wanapopata matatizo.
"Tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya na kutoa wito kuwa waendelee kusafiri kwa kufuata taratibu zilizopo," alisema Mutamba.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
DC MTATURU: SERIKALI ITAVISAIDIA VIKUNDI VITAKAVYO KUWA TAYARI KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Mkuu
wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza umakini kwa
wananchi waliojitokeza kwenye Kikao cha Mafunzo ya namna bora ya
kushiriki katika kilimo chambogamboga na matunda kupitia umwagiliaji
Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ikungi Ayub Sengo akiwasihi wananchi kutumia njia za kisasa katika
kilimo cha umwagiliaji na kufuata taratibu wanazoelekezwa na wataalamu
wa kilimo
Baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali
vya ujasiriamali sawia na wajumbe washiriki kwenye mafunzo hayo
wakifatilia kwa makini Muelimishaji
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya
kiserikali ya RIWADE
Mhandisi Ayubu Massau, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Moses Msai Mratibu wa RIWADE
mkoa wa Singida na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo
Kulia ni Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na kulia kwake ni Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe
wakifatiliakwa makini mafunzo ya namna bora ya kujishughulisha na kilimo
cha umwagiliaji kwa kutumia Gree House
Kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Hassan Tati, Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya
kiserikali ya RIWADE
Mhandisi Ayubu Massau, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe, Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Moses Msai Mratibu wa RIWADE
mkoa wa Singida na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo
Dc Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo hayo
Na Mathias Canal, Singida
Uongozi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida umeahidi kuvisaidia vikundi
mbalimbali ambavyo vitakubali kujihusisha na kilimo cha mbogamboga na
matunda (Perishable Crops) sambamba na kilimo hicho kwa kutumia Kitalu
Nyumba (Green House).
Kauli ya serikali imetolewa na Mkuu wa
Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati akifunga mafunzo kwa
wajasiriamali, wakulima na wafugaji yaliyoendeshwa na Asasi isiyo ya
kiserikali ya Right Way For Development (RIWADE) kwenye ukumbi wa
Mikutano katika Shule ya Sekondari Ikungi na kuhudhuriwa na watu 115
ambao wanatokea katika Kata 24 kati ya Kata 28 zilizopo Wilayani humo.
Katika Mafunzo hayo jumla ya Vikundi 39 vimehudhuria ambavyo vimetakiwa
kujishughulisha zaidi kukimbia kilimo cha mazoea ambacho wakulima
hulima msimu mmoja hadi mwingine na hatimaye kujihusisha na kilimo cha
umwagiliaji ambacho kinatumia muda mchache kukamilika na kuanza kwa
mavuno.
DC Mtaturu amevitaka vikundi hivyo kwa pamoja kutumia
vyema fursa ya Makao makuu ya serikali kuhamia Mjini Dodoma kwani
itakuwa taswira chanya katika kukuza soko la mazao yao pasina kupata
ugumu wa uuzaji.
Amesema kuwa Mkoa wa Singida mara nyingi umekuwa
ukitajwa kama mkoa masikini nchini Tanzania kati ya mikoa 10 ambayo ipo
mkiani katika maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya wananchi wenyewe
kutofanya ubunifu katika kilimo chao jambo ambalo linasababisha
uzalishaji mdogo na kupelekea kipato kuendelea kuwa duni ilihali
maandalizi ya mashamba ni makubwa.
Mtaturu amesema kuwa wananchi
wanapaswa kutoa ushirikiano kwa serikali katika kukamilisha adhma yake
katika uwekezaji na Tanzania ya viwanda kwani endapo watakubali kulima
kilimo cha kisasa na kuwa na uzalishaji mkubwa itakuwa rahisi kwa
serikali kuanzisha viwanda vya kusindika mazao.
Kwa upande wake
muwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya
kiserikali ya RIWADE ambayo imesajili kwa lengo la kiwasaidia vijana
wasio na ajira waweze kufanya kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Mazingira
Mhandisi Ayubu Massau alisema kuwa wananchi wanapaswa kufikia kilimo cha
kuachana na kuuza mazao yao kwa madalali badala yake kuuza moja kwa
moja kwa mtumiaji jambo ambalo litatoa fursa chanya ya mafanikio makubwa
katika pato la mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Hata
hivyo amepigia chepuo zaidi kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) na
kusema kuwa ndicho kilimo pekee chenye uwezo wa kuwatoa wananchi kwenye
kadhia ya umasikini kwani kilimo hichp kupitia umwagiliaji wa kisasa
unatumia maji machache na matokeo yake ni makubwa kama wakulima
watafuata taratibu zote za utunzaji wa shamba.
Massau alisema
kuwa umefika wakati wa wananchi kuachana na vyama vya kufa na kuzikana
badala yake kujihusisha zaidi na vyama vya kujikwamua kiuchumi kupitia
vikundi mbalimbali.
Naye Moses Msai ambaye ni Mratibu wa RIWADE
mkoa wa Singida alisema kuwa wakulima wanapaswa kutambua kuwa sekta
pekee yenye uwezo wa kuajiri watu wengi na kuwatoa kwenye lindi la
umasikini ni Sekta ya Kilimo hivyo ni vyema kufanya kilimo cha kisasa
kwani ndicho kitakacho wanufaisha wananchi.
Ametoa fursa kwa
wananchi kujiunga na RIWADE kwani watapata fursa ya kuunganishwa na
wataalamu ili kuelekezwa namna bora ya kulima kilimo cha umwagiliaji.
Hata hivyo Mjasiriamali na mkulima aliyeshika nafasi ya Kwanza kanda ya
kati katika sekta ya kilimo Hassan Tati aliwasihi wakulima hao
waliopatiwa mafunzo kuwa mafanikio kwenye kilimo ni makubwa endapo
wakulima watafuata taratibu za kilimo na kuwasikiliza wataalamu.
Tati amesema kuwa hakuna ajira nzuri duniani kama kuwekeza kwenye kilimo
lakini amewasihi wananchi kuing'ang'ania Asasi ya RIWADE kwani ni
taasisi muhimu kwa kila mmoja kwa kujitolea kutoa mafunzo ya kilimo na
ufugaji.
Asasi isiyo ya kiserikali ya Right Way For Development
(RIWADE) ilianzishwa Mwezi June 2016, ikiwa ni dhima ya kutengeneza na
kutoa fursa kwa watanzania wote ili waweze kupata elimu ya ujasiriamali
na namna ya kutengeneza mitaji kwa ajili ya ukuaji endelevu wa kijamii
na kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Gdwin GOndwe akisalimiana na mkazi wa kijiji cha nyasa.
Mkuu
waa Wilaya ya Handeni,Mh Godwin Gondwe Jana alifanikiwa kusuluhisha
mgogoro wa mpaka uliokuwa ukivihusisha vijiji viwili vya kata ya
kang'ata wilayani Handeni .Vijiji hivyo ni Madebe na Nyasa ambao walikua
hawafahamu mpaka wao unaishia wapi,suluhu hiyo ilifanikiwa kumalizwa na
mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Handeni ,Bwa.William Makufwe.
DC
Gondwe pia aliwataka wananchi na viongozi wajikite katika shughuli za
kimaendeleo badala ya kujikita kwenye suala la mipaka ,Kwa madai wapate
maeneo ya kulima wakati wakigombania maeneo ili wauze. Amewaonya
wasiuze ardhi kiholela na kufanya vizazi vijavyo kuwa watumwa kwenye
ardhi yao.
Mkuu
wa wilaya Mh.Godwin Gondwe akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa wilaya
ya Handeni,Ndugu William Makufwe (pichani kushoto) akitoa ufafanuzi kwa
wananchi wa vijiji vya nyasa na madebe.
Mwenyekiti
wa kijiji cha nyasa na madebe wakipeana pongezi baada ya kujua mipaka
yao huku wakisistizwa kujikita zaidi katika masuala ya maendeleo.
Mkuu
wa wilaya ya Handeni Mh. Gondwe akipeana mkono wa pongezi na Mwenyekiti
wa kijiji cha Nyasa baada ya kupata mpaka wa maeneo yao.
Mkuu
wa wilaya ya handeni Mh.Gondwe akizungumza na wananchi wa vijiji vya
nyasa na madebe akiwakataza wasiuze ardhi kiholela na wasigombanie
maeneo ili wayauze.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya
Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird (kulia kwake)
na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kulia) baada ya kuweka jiwe la
msingi la jengo la Hakimu Mkazi Mahakama ya Pwani na Mahakama ya wilaya ya
Kibaha Septemba 21,2016. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarest Ndikilo. (PICHA NA OFISI YA
WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akionyesha Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za
Mahakama ya Tanzania baada ya kuuzindua mjini Kibaha, Septemba 21, 2016.
Wengine pichani kutoka kushoto ni Dkt. Hassison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na
Sheria, Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande na Naibu Spika wa Bunge, Dkt Ackson
Tulia
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaidiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mohamed Chande Othaman kukata utepe wakati alipozindua Mpango Mkakati na
Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania mjini Kibaha,
Septemba 21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mohamed Chande Othman baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama
ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango
Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba
21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge
Dkt, Tulia Ackson baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango Mkakati
na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba 21,
2016.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza katika uzinduzi Mpango
Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza
katika uzinduzi Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya
Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini
Kibaha Septemba 21, 2016.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na
Somalia, Bella Bird akizungumza katika uzinduzi Mpango
Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza katika uzinduzi
katika uzinduzi Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho
ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Mradi wa Maboresho ya Huduma za
Mahakama ya Tanzania baada ya kuuzindua mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
Wengine pichani kutoka kushoto ni Dkt. Hassison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na
Sheria, Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande na Naibu Spika wa Bunge, Dkt Ackson Tulia
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa
Nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird kitabu cha Mradi wa
Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania baada ya kuuzindua
mjini Kibaha Septemba 21, 2016. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande
Othman na kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Mpango
Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuashiria ufunhuzi wa jengo la Mahakama
ya Hakimu Mkazi Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Sptemba 21, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mohamed Chande Othman baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama
ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango
Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba
21, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarest Ndikilo baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua
Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania
Septemba 21, 2016
Baadhi ya watumishi wa serikali na wananchi wengine
Baadhi ya watumishi wa serikali na wananchi wengine
Waziri Mkuu katika picha ya pamoja
Meneja
Mkuu wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nd. Ali Ibrahim Kilupi kushoto
akimkabidhi msaada wa mtambo maalum wa mawasiliano ya Simu za ndani {
Inter call } Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd.
Joseph Abdulla Meza kwa ajili ya Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ
Mjini Dar es salaam.
Wa kwanza kutoka Kulia anayeshuhudia tukio la makabidhiano hayo ni
Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam
Ndugu Issa Mlingoti Ali.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Meza akiuwasilisha
msaada huo wa Mtambo wa mawasiliano ya Simu kwa mlengwa Mratibu Mkuu wa
Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam Ndugu Mlingoti.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza alisema jamii na hasa wananchi Wazalendo wenye uwezo wanapaswa kuendelea kujenga tabia ya kusaidia nguvu katika kupambana na changamoto zinazoikabili serikali pamoja na wananchi katika maeneo mbali mbali nchini.
Alisema mfumo uliozoeleza kwa kipindi kirefu sasa katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo ni ule uliotegemewa zaidi wa kupokea misaada kutoka Mashirika, taasisi na mataifa ya nje ya nchi.
Ndugu Joseph Abdulla Meza alitoa kauli hiyo wakati akipokea msaada wa mtambo maalum wa mawasiliano ya ndani { Inter call }kwa ajili ya Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam uliotolewa na Uongozi wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi hafla iliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema wakati umefika kwa wananchi wenyewe kurejesha ari iliyowahi kutekelezwa miaka ya nyuma katika nia ya kujenga nchi kwa kushirikiana kwenye Nyanja zote zinazohusika za kujenga Taifa lenye nguvu za Kiuchumi, maendeleo na ustawi wa Jamii.
{ Tumezoea kupokea misaada kutoka nje ya nchi lakini ni vyema tukapaswa kujenga tabia ya Wananchi wenyewe kusaidia changamoto zinazotukabili sisi pamoja na Serikali yetu “. Alisema Nd. Meza.
Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushukuru Uongozi wa Hoteli ya Kendwa Rocks kwa uamuzi wake wa kusaidia nguvu za kiuwezeshaji changamoto zinazozikabili baadhi ya Taasisi za Umma Nchini.
Mapema Meneja Mkuu wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nd. Ali Ibrahim Kilupi alisema Taasisi yake imeamua kutoa Mtambo huo ili kuwasaidia watendaji wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
OFISI YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ YAPOKEA MTAMBO MAALUM WA MAWASILIANO YA NDANI

WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WAAGIZWA KUWA NA KIWANGO CHA UFAULU KUANZIA ASILIMIA 41
Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati wa
kikao chake na Wakuu wa Shule za sekondari Wilayani humo
Na Mathias Canal, Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi amewaagiza wakuu wa shule za Sekondari zote za Wilaya hiyo kuhakikisha wanafikia ufaulu kuanzia asilimia 41% ili kuakisi hali ya ukuaji wa ufaulu nchini na kupata wanafunzi waliopikwa vyema darasani ili kuwa na wasomi wenye weledi pasina mashaka.
Dc Ndejembi amesema kuwa hatarajii kusikia shule mojawapo Wilayani humo ikiwa imeshika mkia Kiwilaya, Mkoa ana Taifa kwani kufanya hivyo ni kuonyesha jinsi ambavyo walimu hawakujiandaa vyema katika kuwaimarisha wanafunzi darasani ili kufikia ufaulu mahususi na kulijenga Taifa letu katika misingi bora ya elimu.
Ndejembi alisema kuwa anataraji kushirikiana na Afisa elimu sekondari ili kutoa hamasa kwa shule ambazo zitafanya vyema katika mitihani yao ili kuamsha ari kwa shule zingine Wilayani humo.
Walimu hao wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea, kuwa na hofu ya Mungu, na kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa katika kufundisha wanafunzi kwani walimu wana wajibu mkubwa wa kuwafanya wanafunzi kufaulu katika mitihani yao.
Sambamba na hayo pia Dc Ndejembi amewataka walimu hao kutokuwa na madaraja kati yao na wanafunzi wao kwani kufanya hivyo ni kutengeneza chuki kutoka kwa wanafunzi kwenda kwa walimu ambapo pia inapelekea kuyachukia masomo yanayofundishwa na walimu hao.
Na Mathias Canal, DodomaMkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi amewaagiza wakuu wa shule za Sekondari zote za Wilaya hiyo kuhakikisha wanafikia ufaulu kuanzia asilimia 41% ili kuakisi hali ya ukuaji wa ufaulu nchini na kupata wanafunzi waliopikwa vyema darasani ili kuwa na wasomi wenye weledi pasina mashaka.
Dc Ndejembi amesema kuwa hatarajii kusikia shule mojawapo Wilayani humo ikiwa imeshika mkia Kiwilaya, Mkoa ana Taifa kwani kufanya hivyo ni kuonyesha jinsi ambavyo walimu hawakujiandaa vyema katika kuwaimarisha wanafunzi darasani ili kufikia ufaulu mahususi na kulijenga Taifa letu katika misingi bora ya elimu.
Ndejembi alisema kuwa anataraji kushirikiana na Afisa elimu sekondari ili kutoa hamasa kwa shule ambazo zitafanya vyema katika mitihani yao ili kuamsha ari kwa shule zingine Wilayani humo.
Walimu hao wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea, kuwa na hofu ya Mungu, na kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa katika kufundisha wanafunzi kwani walimu wana wajibu mkubwa wa kuwafanya wanafunzi kufaulu katika mitihani yao.
Sambamba na hayo pia Dc Ndejembi amewataka walimu hao kutokuwa na madaraja kati yao na wanafunzi wao kwani kufanya hivyo ni kutengeneza chuki kutoka kwa wanafunzi kwenda kwa walimu ambapo pia inapelekea kuyachukia masomo yanayofundishwa na walimu hao.
VILLARREAL YATIBUA MIPANGO YA REAL MADRID KUWEKA REKODI
Real Madrid imepoteza nafasi ya
kuvunja rekodi ya kushinda michezo 17 mfululizo katika Ligi ya La
Liga baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Villarreal.
Wenyeji Madrid walijikuta wakifungwa
goli baada ya Sergio Ramos kuuzuia kwa mkono mpira na Bruno Soriano
kufunga kwa mkwaju wa penati.
Hata hivyo baadaye Sergio Ramos
alirekebisha makosa yake baada ya tu ya kuanza kipindi cha pili kwa
kufunga kwa kichwa mpira wa kona.
Sergio Ramos akiwa ameupiga mpira kwa kichwa ambao ulienda kujaa wavuni
Cristiano Ronaldo alidhibitiwa vilivyo na kushindwa kutikisa nyavu

No comments :
Post a Comment