Friday, September 23, 2016

MKURUGENZI MTENDAJI WA CRDB BANK DKT CHARLES KIMEI ATUNUKIWA TUZO NA AFRICAN LEADERSHIP, NEW YORK NCHINI MAREKANI



 
Tuzo aliyotunukiwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 jijini New York nchini Marekani katika hotel ya St. Regis, New York. African Leadership hutoa tuzo katika kutambua michango unaotolewa na viongozi wa bara la Afrika katika kuleta maendeleo na utendaji wa kazi wenye ufanisi' katika kukuza uchumi kwa kusaidia kukuza na kuwainua wawekezaji wazawa. African Leadership ilishawahi kutoa tuzo kama hilo kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka April 9, 2014  katika hotel ya St Regis ya Washington, DC. Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production, New York.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa viongozi wa Afrika iliyofanyika siku ya Alhamisi Sepemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis New York. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akielezea mafanikio na utendaji wa benki ya CRDB na jinsi gani inavyowawezesha wawekezaji wazawa kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu katika kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akitunukiwa tuzo na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
 kushoto ni Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akisalimiana na Rais wa Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika mara tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei kupokea tuzo iliyotolewa na African Leadership siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis, New York. kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
 Picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa benki ya CRDB, Bwn. Frederick  Nshekanabo, Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei alipokua akifanyiwa mahaojiano mara tu baada ya kupokea tuzo kutoka African Leadership katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016.

 Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akifuatilia sherehe ya Tuzo kutoka kwa African Leadership iliyofanyika katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.


Hapa ni siku Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, alipomkabidhi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014

KOCHA ARSENAL ARSENE WENGER KUTOSOMA KITABU CHA HASIMU WAKE JOSE MOURINHO

CIARA NA SERENA WILLIAMS WAPONDA RAHA WIKI YA MITINDO YA MILAN

CLAUDIO RANIERI AZIKA 'BIFU' NA KUSEMA KOCHA JOSE MOURINHO NI MTU MZURI

MZOZO WA BRAD PITT NA MTOTO WAKE MADDOX WADAIWA KUWA NDIO CHANZO CHA JOLIE KUDAI TALAKA

NAIBU WAZIRI MASAUNI APANDA MABASI YA MWENDO KASI, JIJINI DAR ES SALAAM

drt1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata tiketi ya mabasi ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo hicho kuelekea Posta. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga naye akiwa mmoja wa wasafiri wa mabasi hayo. Masauni aliyapanda basi la Mwendo kasi mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
drt2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiigusisha tiketi yake katika mashine ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam ili mruhusu kuingia ndani ya stendi hiyo kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo hicho kuelekea Posta. Mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
drt3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiingia ndani ya Basi la Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na basi hilo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
drt4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam akitoka kituo cha Ubungo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAJALIWA APOKEA MISAADA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 16 kutoka kwa Dkt. Ave Maria Semakafu (kulia), Berious Nyasebwa (wapili kushoto) na Benjamin Thomson wote kutoka Group la Whats App la Leaders Forum ukiwa ni mchango wa group hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya ambao walitoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini .Kutoka kushoto ni Sheikh Tahir Mahmood Chaundhry, Issa Mwakitalima, Khuram Shahzad na Jamil Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa tani 40 za saruji zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 kutoka kwa Dhruv Jog na Lebulu Victor (kulia) wote wa Kampuni ya ujenzi a Advent ukiwa ni mchango kwa waahirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba 22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VODACOM TANZANIA, Bw. Ian Ferrao (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ukiwa ni mchango kwa waarhirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SUZA YAWA MWENYEJI WA CHAWAKAMA

TUME YA MIPANGO YAENDESHA WARSHA KUJENGA UELEWA JUU YA MIPANGO YA MAENDELEO YA KIMATAIFA NA KIKANDA

Washiriki wakisikiliza moja ya mada zilizotolewa katika warsha hiyo
Washiriki wakiwa wanasikiliza hotuba ya ufunguzi kutoka kwa balozi Innocent Shiyo.
Washiriki wakipata ufafanuzi wa malengo ya warsha hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe mara baada ya ufunguzi.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent Shiyo (katikati) kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya kufungamanisha sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya kitaifa na ile ya kimataifa na kikanda iliyofanyika Septemba 22, 2016 katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe na kulia ni Bw. Maxwell Mkumba kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Washiriki wakichukua hoja kutoka kwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango (hayupo pichani) katika warsha hiyo. (Picha zote na Adili Mhina)

No comments :

Post a Comment