WAZIRI Mkuu wa zamani
wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, Edward Lowassa amewatembelea
wananchi wa mji wa Bukoba walioathirika na tetemeko la ardhi na kuwasihi
Watanzania kuwasaidia wananchi hao kama ilivyo desturi yetu.
Akizungumza na Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu) Salum Kijuu Septemba 10, 2016 alipofika
Ofisini kwake kumpa pole kufuatia tetemeko hilo lililotokea Septemba 10, 2016
na kuua watu 17. Lowassa alisema, amefika mkoani humo ili kutoa mkono wa pole
kufuatia maafa hayo na kumpapole Mkuu wa mkoa huo kwa niaba yawananchi wa mkoa
wa Kagera.
“Nawasihi watanzania wenzangu tuendelee
kujitolea kuwasaidia wahanga kama ilivyo desturi ya umoja wa kitaifa tulionao”.
Ameandika Lowassa katika ukurasa wake wa Tweeter.
Baada ya kuona hali
ilivyo sasa kwa baadhi ya wakazi wa mkoa huo kupoteza ndugu zao, nyumba na mali
zao kuharibika, Lowassa ametumia ukurasa wake wa Twitter kufikisha ujumbe kwa
jamii ya watanzania sehemu yoyote walipo duniani kote.
Ujumbe wa kwanza
Lowassa aliandika “Poleni ndugu zangu Wa Kagera na mlioathirika na tetemeko,
Tupeane nguvu ili tuvuke katika kipindi hiki kigumu pamoja”
Lowassa akizungumza na wakazi wa Hamugembe, baada ya kutembelea eneo hio lililoathirika sana na tetemeko hilo
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza
na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini,
Awa Dabo (kulia), kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake
na UNDP. Dabo alimtembelea Naibu Waziri Masauni ofisini kwake jijini Dar es
Salaam leo. Wapili kushoto ni Nirine
Kiplagat, Meneja wa Miraji katika Shirika hilo, na Godfrey Mulisa wa UNDP. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA
NCHI).
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa
Dabo wakati alipokuwa akizngumza kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati
ya Wizara yake na UNDP. Dabo alimtembelea Naibu Waziri Masauni ofisini kwake
jijini Dar es Salaam leo. Wapili
kushoto ni Nirine Kiplagat, Meneja wa Miraji katika Shirika hilo, na Godfrey
Mulisa wa UNDP.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka kwenye Msikiti Mkuu wa Mafia bada
ya kushiriki sala ya Ijumaa akiwa katika siku ya kwanza na ziara ya
mkoa wa Pwani Septemba 23, 2016. (PICHA
NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya Ijumaa kwenye
Msikiti Mkuu wa Mafia akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Pwani
Septemba 23, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
ndege wa Mafia kwa ziara ya kikazi wilayani humo Septemba 23, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Pwani
baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kwa ziara ya kikazi
Septemba 23, 2016
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.
Mtengenezaji wa Sauti katika chaneli ya
StarTimes Kiswahili, Tracy Luo (katikatio) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kufanyika kwa fainali za
shindano la vipaji vya sauti litakalofanyika kesho katika ukumbi wa
Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kushoto ni mshiriki wa shindano
hilo kutoka Zanzibar, Safiya Ahmed na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Masoko wa kampuni hiyo, Damien Li. Washiriki 18 kati ya 547 wameingia
hatua ya fainali ambapo washindi 10 watajipatia fursa ya kwenda kufanya
kazi makao makuu ya StarTimes yaliyopo Beijing, China.
Mshiriki Safiya Ahmed kutoka Zanzibar (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mtengenezaji wa Sauti katika chaneli ya StarTimes Kiswahili, Tracy Luo.
Mshiriki Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam (kulia), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
Mshiriki kutoka mkoani Arusha, Mathew
Mgeni (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni mshiriki Hilda
Malecela kutoka Dar es Salaam.
Taswira meza kuu kwenye mkutano huo.
Washiriki wa shindano hilo. Kutoka kulia
ni Safiya Ahmed kutoka Zanzibar, Mathew Mgeni kutoka Arusha na Hilda
Malecela kutoka Dar es Salaam
Washiriki wa shindano hilo wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
WASHIRIKI 18 waliotinga fainali ya
shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloendeshwa na kampuni ya
StarTimes watapanda jukwaani kesho katika ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam kupigania nafasi kumi za kwenda kufanya kazi
jijini Beijing, China.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitaliya Taifa
Muhimbili, (MNH), Profesa Lawrence Museru, (kushoto), akifafanua jambo
wakati akizungumza na waandishi wa habarikwenye ukumbi wa mikutano wa
OPD, wa hospitali hiyo jijini Dar es Salaam leo Septemba 23, 2016 kuhusu
safariya wataalamu wa afya saba wa hospitali hiyo wanaoondoka nchini
Septemba 25, 2016 kuhudhuria mafunzo kwa vitendo ya
ya
upandikizaji wa kifaa cha usikivu
(Cochlear-implant), katika hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi nchini
India. Kulia ni Dkt. Edwin Liyumbu, ambaye atajkuwa mkuu wa msafara.
9PICHA NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
JOPO
la wataalamu saba wa Afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH), litaondoka nchini Jumapili Septemba 25, 2016
kuhudhuria mafunzo kwa vitendo juu ya upandikizaji wa kifaa cha usikivu
(Cochlear-implant), katika hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi nchini India.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa OPD wa hospitali hiyo jijini
Dares Salaam, Septemba 23, 2016, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili, (MNH), Profesa Lawrence M. Museru, alisema, mafunzo hayo
yatawawezesha wataalamu wa Afya wa Hospitali hiyo kuongeza ujuzi na hivyo uwezo
wa hospitali hiyo kutoa huduma kwa wagonjwa ambao hapo awali walilazimika kuzifuata
huduma hizo nje, wataweza kuzipata hapa nchini.
Jopo la wataalamu hao litaongozwa na Dkt.
Dkt.Edwin Liyumbu, Dkt.Shaaban Mawela,Mariane Pessa,
John Bosco Kambanga,Mathayo Alfred, Fikiri Idd, na Christina Simangwa.
Dkt.Edwin Liyumbu, Dkt.Shaaban Mawela,Mariane Pessa,
John Bosco Kambanga,Mathayo Alfred, Fikiri Idd, na Christina Simangwa.
“Wataalamu
hawa watajifunza kwa njia ya vitendo jinsi ya kufanya upasuaji na upandikizaji
wa kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto.” Alifafanua Profesa Museru.
Alisema,
wataalamu hao ni pamoja na madaktari bingwa wawili wa upasuaji wa pua, koo na
masikio, wauguzi wawili wa chumba cha upasuaji, mtalaam mmoja wa kupima usikivu
pamoja na watalaam wawili wa kufundisha jinsi ya kuongea hususani kwa watoto
waliozaliwa na tatizo hilo.
Takwimu
za Hospitali ya Taifa Muhimbili zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya wagonjwa ambao
wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa kifaa cha usikivu ni watoto wadogo.
Hivyo tunatarajia huduma hii kusaidia watoto wengi hapa nchini na pia kujenga
uwezo kwa wataalamu wa ndani ya nchi.
Gharama
za kupandikiza kifaa cha usikivu kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi milioni 80
hadi 100 anapopelekwa nje ya nchi wakati mgonjwa mmoja anayepandikizwa figo nje
ya nchi pia hugharimu kiasi cha shilingi milioni 40 hadi 60. Uwepo wa huduma
hizi hapa nchini utawezesha watanzania wengi kupata huduma hii na kwa gharama
nafuu zaidi na kupunguza mzigo kwa Serikali wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi
kwani gharama za matibabu zitapungua kwa zaidi ya asilimia 50.
Wataalam
hawa wanatarajia kurejea hapa nchini Oktoba 28, 2016 tayari kuanza kutoa huduma
hiyo. Mapema mwezi huu Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipeleka nchini India
wataalamu 18 wa fani mbalimbali kwa ajili ya kujengewa uwezo wa upandikizaji
figo kwa watu wenye matatizo ya figo ambapo timu hiyo inatarajia kurejea
mwishoni mwaka huu.
Gharama
za kupeleka timu zote mbili ya upandikizaji wa figo pamoja na upandikizaji wa
kifaa cha usikivu ni shilingi milioni 528 zikijumuisha gharama za mafunzo,
nauli, fedha za kujikimu pamoja na gharama nyingine za mafunzo. Fedha hizi zote
zitalipwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kujenga uwezo wa watalaamu wake.
Aidha
Hospitali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 3.4 ili kuongeza vyumba
vya upasuaji kutoka 12 hadi 20, na sasa hivi tunavifanyia ukarabati
viliyokuwepo 12 na kuweka vifaa vipya katika vyumba vya upasuaji
vitakavyoongezwa. Eneo la huduma za uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo
litapanuliwa na kuongeza vitanda kutoka 17 vya sasa hadi vitanda 42 sambamba na
kuongeza mashine zake kufikia 42 na kuweka mtambo wa kuchuja
maji (water-treatment plant). Hospitali itaongeza pia vyumba vya
wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu vipya vinne (ICUs) vikiwa na jumla ya
vitanda 40 na kuviwekea vifaa vipya pamoja na vyumba vinne vya kupokea wagonjwa
baada ya kutoka ICU (step-down ICU) na kabla ya kwenda kwenye wodi za
kawaida navyo vitakuwa na vitanda 40. Aidha Ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu
hii unaendelea na unatarajiwa kuwa umekamilika ifikapo mwishoni mwa Disemba
2016.
Baadhi ya wataalamu hao kutoka kushoto,
Marina Pessa, Mathayo Alfred, na Dkt.Shaaban Mawela, (wakwanza kulia ni
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Dkt.Hedwiga Swai (hayumo kwenye msafara)
Dkt.Edwin Liyumbu, (Mkuu wa msafara na pia Mkuu wa Idara)
Dkt.Shaaban Mawela
John Bosco Kambanga
Marina Pessa
Mathayo Alfred
Fikiri Idd
Christina Simangwa
Baadhi ya wanahabari
Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Hospitali
ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, (aliyesimama), akiwatambulisha
wataalamu hao wa Afya, kabla ya kuanza kwa mkutano huo. (katikati) ni
Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Museru
Baadhi
ya wananfunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana na Songe, Musoma wakipitia
machapisho mbalimbali ya elimu ya Mpiga
kura yaliyotolewa na Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika shule
hiyo wakati wa uzinduzi wa program ya utoaji wa elimu ya mpiga kura kwa
wananchi. (PICHA/ARON MSIGWA –NEC).
Mkuu
wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa NEC, Bi. Giveness Aswile
akiwaeleza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe Musoma mfumo unaotumiwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) katika kuwawezesha watu walio katika makundi maalum hasa watu
wenye ulemavu wenye sifa kupiga kura
kupitia karatasi maalum.
Mkurugenzi
Idara ya Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Emmanuel
Kawishe akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe
nje kidogo ya mji wa Musoma juu ya majukumu na utendaji wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati wa uzinduzi wa programu endelevu ya utoaji wa elimu ya mpiga
kura kwa kuyafikia makundi mbalimbali nchini.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe iliyoko nje kidogo ya mji wa Musoma
wakionesha vipeperushi na machapisho mbalimbali waliyopewa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kwa lengo la kuwawezesha kuongeza uelewa juu ya majukumu ya Tume
wakati wa uzinduzi wa program endelevu ya utoaji wa elimu ya mpiga kura mjini
Musoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhandisi Manyiri Isaya akitoa
ufafanuzi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe nje kidogo
ya mji wa Musoma juu ya daftari la wapiga kura na namna taarifa za wapiga kura
zinavyotumika kwenye chaguzi mbalimbali. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Huduma za
Kisheria wa Tume Bw. Emmanuel Kawishe.
Mwanafunzi
wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe, Musoma
akiwauliza swali Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (hawapo pichani) juu ya
matumizi ya TEHAMA katika kuwabaini wananchi waliojiandikisha kwenye kituo cha
kupigia kura zaidi ya kimoja.
Baadhi
ya wananfunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana na Songe nje kidogo ya mji wa
Musoma, wakifuatilia kwa makini elimu ya Mpiga kura iliyokuwa ikitolewa na
Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika shule hiyo wakati wa uzinduzi
wa program ya utoaji wa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akihutubia wakati akifungua
Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Ambwene Mwakyusa akizungumza katika semina hiyo.
Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akipeana
mkono na Msaji wa Bodi hiyo Jehad Jehad baada ya kumaliza kutoa hutuba
yake.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.
Taswira meza kuu katika semina hiyo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mbarawa.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi, Waziri
Mbarawa (aliyekaa katikati), Wengine kutoka kulia waliokaa ni Mkurugenzi
wa Huduma na Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Profesa Mhandisi William
Nshana, Mwenyekiti wa Bodi, Ambwene Mwakyusa, Msajili wa Bodi, Jehad
Jehad na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili, Dk.Adelina Kikwasi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akishuhudia
Dereva wa Basi la Tahmeed (kulia) akipimwa kilevi na Trafiki Nuru Mvungi kabla
ya Basi lake kuruhusiwa na safari. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika
Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na
Kibaha mkoani Pwani leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akielekea
Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani Ubungo, jijini Dar es Salaam wakati alipofanya
ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa
abiria katika Stendi hiyo pamoja na Stendi ya Kibaha mkoani Pwani. Masauni alilizuia Basi la Shambarai lenye namba za usajili T419
BUF na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga
kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza
kuhatarisha maisha ya abiria. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwauliza abiria wa
Basi la Harambee linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, maswali
mbalimbali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wakati wanaposafiri. Masauni
alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani,
Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua mikanda
katika Basi la Shambalai wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Stendi
Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akioneshwa
na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga,
tairi la Basi la Shambalai ambalo halina ubora kwa ajili ya kusafirisha abiria.
Hata hivyo Masauni aliagiza basi hilo lizuiwe kufanya safari na pia kuchukuliwa
hatua kali kwa Mmiliki wa basi hilo pamoja na Dereva. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai)
akizungumza na madereva wa Basi ya mikoani pamoja na wa magari madogo ya mizigo
yanayopaki Stendi Kuu Ubungo, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka madereva
hao kufuata sheria za usalama barabarani. Hata hivyo, madereva hao walilalamika
kuwa hawana mikataba ya kazi zao. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika
Stendi hiyo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
waandishi wa habari, Picha ya Ndege Kibaha, Pwani, mara baada ya kukamilisha
ziara yake ya kukagua mabasi mabovu na usalama wa abiria. Masauni alifanya
ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini
Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akihoji
usalama wa mtoto baada ya kugundua siti moja kukaa watoto wawili jambo ambalo
ni hatari kwa usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika
Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye
alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments :
Post a Comment