Saturday, September 10, 2016

MANCHESTER CITY YAIBUKA MBABE KATIKA DIMBA LA OLD TRAFFORD

KOREA KASKAZINI YADAI KUGUNDUA DAWA INAYOTIBU UKIMWI NA EBOLA

JENNIFER LOPEZ AJIFUA MAZOEZI YA UBONDIA KWA AJILI YA FILAMU

Jennifer Lopez ambaye ni maarufu kwa kuimba na kudansi, ameingia kwenye klabu ya ndondi kujifua ili kujiweka fiti kimapambano kwa ajili ya kucheza filamu ya shoo ya TV ya Shades of Blue.
Mrembo Lopezi, 47, ameonekana Jijini Manhattan kwenye klabu ya ngumi akijifua na kutoka jasho katika kuuweka mwili wake vizuri ili kuweza kupiga picha za filamu hiyo akicheza kama bondia.
                 Jennifer Lopez akisaidiwa kuvalishwa gloves tayari kwa mazoezi ya ndoni

CRISTIANO RONALDO KUSHUKA DIMBANI KWA MARA YA KWANZA LEO TANGU AUMIE FAINALI YA EURO 2016

KOCHA JAMES SIANG’A AFARIKI DUNIA NYUMBANI KWAO BUNGOMA- KENYA

Mmoja wa makocha wanaoheshimika sana Afrika Mashariki, ambaye pia aliwahikuwa mchezaji mkubwa wa soka James Siang’a amefariki dunia jana huko Bungoma nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa afisa wa chama cha Kefoca, Bob Oyugi, Siang’a ambaye aliwahi kuchezea Gor Mahia, Luo Union na timu ya taifa Kenya Harambee Stars kama kipa amefariki dunia majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo.

Mbali na kuichezea Harambe Stars Siang’a pia alikuwa kocha wa Harambee Stara katika mwaka 1999 hadi 2000, kisha kuja Tanzania kuinoa Taifa Stars mwaka 2002. Pia aliwahi kuwa kocha wa klabu za Simba, Moro United na Express ya Uganda.
Akiwa na Moro United Oktoba 2004 Siang’a aliombwa kuinoa Taifa Stars lakini alikataa. Siang’a pia aliinoa Mtibwa Sugar kabla ya kurejea Kenya kuifundisha timu ya Gor Mahia

No comments :

Post a Comment