Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Jordan Lugimbana baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
Dodoma Septemba 4, 2016 kwa ajili ya vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza
Septemba 6, 2016. (PICHA NA OFISI YA
WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana
Septemba 4, 2016 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama
baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge
vinavyotarajiwa kuanza Septemba 6, 2016
Wasanii wa Clever
Boys ambao wameingia fainali ya mashindano yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania ya Dance 100%, wakichuana kwenye
nusu fainali ya mashindano hayo katika viwanja
vya Don Bosco jijini Dar es Salaam
Mmoja wa Majaji wa
mashindano yanayodhaminiwa na Vodacom Tanzania ya Dance100%, Super Nyamweli (kulia) akionyesha umahiri
wake wa kucheza kwenye nusu
fainali ya mashindano hayo jijini Dar es Salaam huku akishangiliwa na
mmoja wa majaji wenzake Khalila Kellz
Wasanii wa Clever
Boys ambao wameingia fainali ya mashindano yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania ya Dance 100%, wakichuana kwenye
nusu fainali ya mashindano hayo katika viwanja
vya Don Bosco jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa bodi mpya.kesho |
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira leo itazindua
bodi mpya yake iliyoteuliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Gerson Lwenge
Julai
Mosi mwaka huu baada ya ile ya awali kumaliza muda wake ambayo ilidumu kwa
kipindi cha miaka mitatu.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine
Shigella anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ambayo inatarajiwa kuanza
asubuhi.
Akizungumza jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua
Mgeyekwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa halfa hiyo pia itatumika kutambua
na kupongeza juhudi zinazofanywa na bodi,menejimeni na wafanyakazi wa mamlaka
hiyo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa kushoto aliyesimama na PRO wa Mamlaka hiyo |
Alisema licha ya wafanyakazi hao lakini pia wateja
wao kwa kuiwezesha mamlaka hiyo kuwa bora kwa utoaji wa huduma za maji safi
miongoni mwa mamlaka 23 za maji safi na usafi wa mazingira hapa nchini kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo tokea mwaka
2012/2013.
Aidha alisema pia mamlaka hiyo imepata leseni ya
daraja la kwanza baada ya kukithi vigezo vya mdhibiti wa huduma za nishati na
maji hivyo kuwa mamlaka ya kwanza ya maji safi na usafi wa mazingira hapa
nchini kufikia hatua hiyo ya juu katika ufanisi wa utendaji wa
mamlaka.
“Waandishi
wa habari kama mnavyojua mamlaka yetu ina cheti cha ithibati ya Ubora (ISO
9001) ambacho imekipata tangu mwaka 2007 tokea kipindi hicho mamlaka imekuwa
ikifanya kazi zake kwa viwango vya kimataifa katika usimamizi wa mfumo wa
kumhudumia mteja kwa kufuata vigezo vya ubora
“Alisema.
Waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya mkurugenzi huyo |
“Lakini pia
cheti hiki huuishwa kila baada ya miaka mitatu kwa kukidhi vigezo vya utoaji wa
huduma vinazohitajika ,uhuishaji ulifanyika miaka 2010 na 2013 kwa kupata ISO
9001:2008 na mwaka huu Tanga Uwasa imekuwa taasisi ya kwanza nchini chini ya
kampuni ya Ithibati ya SGS Tanzania kupata cheti cha Ithibati cha
9001:20015.
Aidha aliongeza kuwa mafanikio makubwa sana ambayo hayo yametokana na juhudi za pamoja kati ya bodi ya wakurugenzi, menejimenti,wafanyakazi,wateja na wadau wa Tanga Uwasa.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Rais
John Pombe Magufuli, akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam usiku huu Septemba 3, 2016. Rais alikuwa kwenye ziara ya
siku mbili visiwani Zanzibar kuwashukuru wananchi kwa kuichagua
CCM.(PICHA NA IKULU).
Meneja wa Tigo Mkoa wa Mara, Edwin Kisamo akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Utegi wilayani Rorya wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kwa shule hiyo jana. |
Wanafunzi
wa shule ya msingi Utegi wakiwa wameketi kwenye madawati
waliopewa na kampuni ya simu za mkononi Tigo jana.
|
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Nelson Mlela
akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na
Mazingira walipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam
leo Septemba 3,2016 . (PICHA ZOTE NA OFISI YA BUNGE)
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.
Khatib Said Haji Mbunge wa Konde akichangia hoja katika kikao baina ya wadau wa
biashara na Kamati hiyo walipokutana kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara
katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3,2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Mhandisi Deusdedit
Kakoko(kushoto) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge
ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu masuala mbalimbali ya kibiashara
katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3, 2016 kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na
Mazingira Mhe. Dkt Dalaly Peter Kafumu Mbunge wa Igunga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na
Mazingira Mhe. Dkt Dalaly Peter Kafumu Mbunge wa Igunga akizungumza na uongozi
wa Bandari na watendaji wa Wizara husika walipokutana kujadili masuala
mbalimbali ya kibiashara katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3, 2016.
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini TAFF Bw. Otieno Ogobo akitoa maoni
yake kwa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na
Mazingira walipokutana kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara katika Bandari
za Tanzania leo Septemba 3, 2016.
Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Jocktan Kyamuhanga akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge
ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu masuala mbalimbali ya ukusanyaji
mapato katika Bandari za Tanzania leo Septemba 3,2016 .
Kaimu Meneja wa Bandari ya
Dar es Salaam Bw. Nelson Mlela akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge
ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea kuangalia utendaji kazi wa
Bandari ya Dar es Salaam leo Septemba 3,2016
No comments :
Post a Comment