Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu wa pili kushoto akitoa maagizokwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai wa kwanza kulia
wakati alipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es
salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai
wa kwanza kulia akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati alipotembelea
wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliopo katika taasisi ya
Mifupa Muhimbili (MOI)alipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo leo
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akimfariji
mtoto Rahel Razaro wa kwanza kushoto aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa
Muhimbili(MOI) alipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini
Dar es salaam na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi
hiyo Dkt. Samuel Swai.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali chini ya Wizara ya Afya
,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imeitaka Taasisi ya Mifupa
Muhimbili(MOI) kuhudumia wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuondoa
msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo na kuwaruhusu wakaendelee na
shughuli za kujenga taifa.
Akizungumza hayo alipotembelea
wagonjwa MOI Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kuwahudumia
wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuwapa fursa ya kwenda kufanya
shughuli za kimaendeleo kwa ajili ya taifa.
“Mnatakiwa kuhudumia wagonjwa kwa
haraka na ufanisi mkubwa ili kuwasaidia watanzania kutotumia muda
mwingi wakiwa hospitalina na badala yake wapone waende wakaendelee na
shughuli zao za kujenga taifa kwa maendeleo ya Nchi yetu”alisema Mhe.
Ummy
Aidha Mhe. Ummy ameongeza kuwa
licha ya kuwa na changamoto zinazojitokeza hospitalini hapo Wizara ipo
bega kwa began a Taasisi hiyo kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa
wananchi chini ya kitengo hiko ili kufikia malengo ya milenia.
“Nafahamu kama kuna changamoto
zinazoikabili taasisi hii kama mlivyonieleza lakini tupo pamoja katika
kuziondoa na nyinyi hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii ili kuondoa
malalamiko ya wananchi na kuleta huduma bora na kwa wakati” alisisitiza
Mhe. Ummy.
Mbali na hayo Mhe. Ummy ameitaka
taasisi hiyo kurudisha huduma ya kufanya upasuaji kwa wagonjwa siku za
jumamosi bila ya kukosa tena kwa haraka ili kupunguza mlundikano wa
wagonjwa kwenye taasisi hiyo.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji MOI Dkt. Samuel Swai amesema kuwa wamepokea agizo hilo na wapo
tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya watanzania kwa haraka
na ubora zaidi.
“Tupo tayari kutekeleza agizo la
Mheshimiwa Waziri la kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya
watanzania kwa haraka na ataona matokeo mazuri kuanzia leo hii”
alisisitiza Dkt. Swai.
DC WA ILALA MH SOPHIA MJEMA AKABIDHIWA MSAADA WA MADAWATI KWA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO WENYE ASILI YA CHINA JIJINI DAR LEO
Muwakilishi
wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akimkabidhi moja ya
dawati kati ya 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Karikoo wenye
asili ya China ,kwa Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema mapema
leo jijini Dar.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema akizungumza kwenye hafla fupi ya
kukabidhiwa madawati 200 kutoka kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye
asili ya China leo jijini Dar,kwa ajili ya shule ya msingi Maghorofani
iliyopo Gongolamboto,jijini Dar Es Salaam.Wafanyabiashara hao waliahidi
kumkabidhi Mh.DC Mjema Madawati 200 lakini leo wamekabidhi nusu ya
madawati hayo (100),huku mengine yakiendelea kutengenezwa.Shule hiyo ya
Maghorofani ilikuwa na uhitaji wa madawati 525,yakapatikana madawati 250
na kupungukiwa madawati 275.
Muwakilishi
wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akizungumza kwa ufupi
mbele ya Waalimu,wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),kabla ya
kukabidhi madawati 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariako wenye
asili ya China jijini Dar,pichani kulia ni Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh
Sophia Mjema.
Baadhi
ya Wanafunzi wa shule hiyo ya Maghorofani wakiwa wamekalia baadhi ya
madawati yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya
China jijini Dar.
Wakiwa katika picha ya pamoja .PICHA NA MICHUZI JR.
MKUU WA MKOA WA SINGIDA AFUNGUA MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA KATI DODOMA
Mkuu
wa Mkoa wa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kushoto) akisalimiana
na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ufunguzi wa
maonyesho ya Nane Nane katika uwanja wa maonyesho ya kilimo Nzuguni
Mkoani Dod
Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Singida wakitembelea baadhi ya vibanda vya maonyesho wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Nane Nane
Mgeni rasmi alipotembelea banda la dawa za kilimo, uvuvi na ufugaji Farmer Centre and Farm base
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya
kilimo cha zao la zabibu
Mgeni rasmi akisikiliza kwa kina maelezo juu ya matumizi ya matrekta kwa ajili ya kilimo
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya mboga
mboga
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya bwawa
la samaki lenye samaki aina ya perege, kambare na kamongo liloandaliwa
na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba
Zoezi la kutembelea mabanda ya maonyesho likiwa linaendelea
………………………………………………………………………………………………………
Na Mathias Canal, Dodoma
Ufunguzi wa siku kuu ya wakulima
Nane nane Kanda ya kati Dodoma mwaka 2016 umefanyika leo katika Uwanja
wa Maonyesho ya kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma huku kauli mbiu ya mwaka
huu ikiwa ni “Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana
shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Maonyesho haya yanahusisha
shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi,
wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo,
wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, taasisi za
umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizungumza katika ufunguzi huo
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe
amesema kuwa sekta ya kilimo bado ni mhimili wa uchumi wa Tanzania kwa
sababu inaajiri zaidi ya asilimia takribani 80 ya watanzania na kwa
kuzingatia malengo ya maendeleo ya Taifa ya kuwa nchi yenye uchumi wa
kati unaotegemea viwanda hivyo kilimo kikiboreshwa viwanda vitapata
malighafi ya uhakika na kuimarisha masoko kwa wakulima hivyo kuwepo na
ajira ya kuaminika kwa vijana na watanzania kwa ujumla.
Rc Mtigumwe amesema kuwa wastani
wa ukuaji wa sekta ya kilimo unabadilika mwaka hadi mwaka kutokana na
kilimo kwa kiwango kikubwa kutegemea mvua ambazo zimekuwa zikinyesha kwa
viwango na mtawanyiko unaotofautiana kila mwaka ambapo kwa mwaka 2010
sekta ya kilimo ilikuwa kwa asilimia 4 ikilinganishwa na asilimia 6.5 ya
mwaka 2015.
“Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali
zinaonyesha kuwa kanda ya kati ina rasilimali ya maji yakutosha ya chini
ya ardhi hivyo kuendelea kuitamka kama kanda kame hakuna usahihi wa
jambo hilo ipo haja ya kuona kuwa rasilimali hiyo inapatikana kwa ajili
ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji hivyo kupunguza kilimo cha
kutegemea mvua” Alisema Mtigumwe
Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida
kabla ya kuwahutubia wananchi waliojitokeza katika ufunguzi huo
alitembelea baadhi ya mabanda ya maonesho na kuona shughuli mbalimbali
za uzalishaji wa mazao, ufugaji, uvuvi, usindikaji na wauzaji wa zana na
pembejeo za kilimo ambapo amejionea matokeo ya juhudi mbalimbali
zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuinua ukuaji wa sekta
ya kilimo ambapo juhudi hizo zinajumuisha uzalishaji wa mbegu mbalimbali
zinazostahimili hali ya hewa ya maeneo ya kanda ya kati.
“Natoa wito maalumu kwa wakulima,
wafugaji, wavuvi, wajasiriamali na wadau wa sekta zingine kuhakikisha
kuwa bidhaa zenu zinafikia ubora wa hali ya juu kuanzia shambani
zinakozalishwa, zinakosindikwa na kuhifadhiwa na hadi kumfikia mlaji,
ikumbukwe kwamba kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu
kutawezesha bidhaa zetu kuhimili ushindani wa hapa nchini na nje ya nchi
na kuuzwa kwa bei nzuri” Alisema Mtigumwe
Akitoa neno la shukrani kwa niaba
ya waandaaji wa maonyesho ya Kilimo, Mifugo na sherehe za nane nane,
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amesema
kuwa hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida itakuwa ya
mazingatio ili kurahisisha na kuendeleza kasi ya serikali ya awamu ya
Tano kwa vitendo hususani katika kuakisi na kuwasaidia wananchi ambao ni
wakulima na wafugaji kupata mbinu bora za kufuga na kulima kisasa ili
kupata mazao kwa wingi.
Hata hivyo Dc Mtaturu amesema
kuwa ana imani thabiti kuwa baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo
wakulima, wafugaji na wananchi washiriki watakuwa wamejifunza vyema
mbinu bora za kukabiliana na changamoto za kilimo na ufugaji hivyo
kujikita zaidi katika mbinu bora na za kisasa za kilimo na ufugaji pia.
Dc Mtaturu amesema kuwa shughuli
kuu ya wakazi wa kanda ya kati inayoundwa na mikoa miwili ya Singida na
Dodoma yenye jumla ya Wilaya kumi na mbili na Halmashauri 15 shughuli
zao kuu ni kilimo na ufugaji.
WAZIRI MKUU ATOA SIKU MOJA KWA MANISPAA YA MOROGORO KUTANGAZA MAENEO KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA WADOGO
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa uongozi wa Manispaa ya
Morogoro kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na
kuyatangaza kesho.
“Mbali na kutenga maeneo pia
nawaagiza muwasaidie wafanyabiashara hawa kuunda vikundi kulingana na
aina ya biashara wanazozifanya ili kuwawezesha kupata mikopo kwa urahisi
kutoka katika taasisi za fedha” alisema.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo leo
(Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa
kituo cha mabasi Msamvu unaojengwa kwa ubia kati ya Manispaa ya Morogoro
na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Awamu ya kwanza ya mradi huo
inatarajiwa kufunguliwa Agosti 12 mwaka huu utakuwa ni kituo cha mabasi
cha kwanza cha kisasa Tanzania ambapo Waziri Mkuu amezitaka halmashauri
zote zilizoko makao makuu ya mikoa nchini kuiga mfano huo.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo
kulipongeza Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro na LAPF kwa
kubuni mradi huo wa kisasa utawezesha abiria kupata taarifa ya basi
lilipo na muda litakapowasili kituoni hapo hivyo kupunguza udanganyifu
kutoka kwa mawakala wasiokuwa waaminifu.
Kwa upande wake Meneja wa mradi
huo Stanley Mhapa alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 40 ambapo
Manispaa inamiliki asilimia 40 ya hisa na mfuko wa LAPF unamiliki
asilimia 60.
“Mafanikio ya mradi huu ni pamoja
na kuiwezesha Manispaa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka sh 350,000
kwa siku hadi kufikia sh. milioni 1.7 kwa siku,” alisema.
Mhapa alisema mradi huo
utakapokamilika utatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za
kibenki, vibanda vya biashara, sehemu za chakula, ofisi na sehemu ya
mapumziko ya abiria na vibanda vya kukatia tiketi.
WAZIRI MKUU AWATAKA WAFUGAJI WAKUBWA KUJIANDAA KUFUGA KISASA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiteremka kuelekea eneo la
kuchinjia ng’ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo
Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua eneo la kuchinjia
ng’ombe katika kiwanda cha nyama cha Nguru Hills Ranch cha Morogoro
Agosti 3, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda hicho,
Danstan Mrutu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizingumza na Mkurugenzi na
mshauri wa kiwanda cha nyama cha Ngulu Hills Ranch cha Morogoro ,
Dunstan Mrutu (kulia kwa Waziri mkuu) ) wakati walipokitembelea kiwanda
hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watoto
na wananchi wa kijiji cha Majichumvi wilayani Mvomero wakionyesha
mabango wakati WaziriMkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao
kuwasikiliza Agosti 3, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga
wakati alipokagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Morogoro Agosti 3,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Stendi mpya ya mabasi la Msamvu
mjini Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mjini Morogoro baada
ya kukagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Agosti 3, 2016. Kulia ni Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Stephene Kebwe na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Eliud Sanga. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Awamu
ya kwanza ya jengo la stendi mpya ya mabasi ya Msamvu mjini Morogoro
iliyokamilika kwa asilimia 90. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliitembelea
stendi hiyo na kuzungumza na wadau Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Halima Mwishehe alipouliza
swali wakati Waziri Mkuu alipozungumza na Wananchi kwenye stendi mpya ya
Msamvu Morogoro baada ya kukagua ujenzi wake Agosti 3, 2016. Kulia ni
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini
kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na
Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.
Pia aliwataka wafugaji hao
kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya maeneo hayo
ikiwemo ujenzi wa visima vya maji na majosho ili ufugaji wao uwe na
tija.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika
nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Movomero.
Hata hivyo Waziri Mkuu alisema
kitendo cha wafugaji hao kuhamia katika ranchi kitawezesha mifugo yao
kuwa na ubora kwa sababu aina ya ufugaji wa sasa ya kutembeza mifugo
umbali mrefu inasababisha ufugaji wao kuwa na tija ndogo.
Akizungumzia kuhusu uwepo wa
kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero Waziri Mkuu alisema
kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa
wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani hapo.
“Uwepo wa viwanda katika maeneo
yetu utatuwezesha kupunguza matatizo tuliyonayo katika maeneo yetu
ikiwemo suala la migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Viwanda ndiyo
vitakavyotuondoa kutoka katika uchumi wa chini hadi wa kati,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi na
Mshauri wa kiwanda cha Nguru Hills Ranch, Dunstan Mrutu alisema kiwanda
hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa
siku kinatarajiwa kufunguliwa mwezi Desemba mwaka huu.
Mkurugenzi huyo alisema takriban
asilimia 80 ya nyama itafungashwa na kuuzwa nje ya nchi hasa Uarabuni
kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa na mvuto maalum
katika nchi hizo.
“Mbali na uwekezaji huu wa
kiwanda cha nyama pia tunatazamia kuwekeza katika mnyororo wa thamani
kuanzia kusindika ngozi inayotoka kiwandani hadi kuzalisha viatu,
mikanda na bidhaa zote za ngozi na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo
kutoka nje ya nchi,” alisema.
Mrutu alisema nia yao ni kuitikia
wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kutaka viwanda vizalishe viatu nchini
kuanzia vya majeshi na wananchi wote ambapo wamepanga kuanzia mwakani
wataanza kuuza bidhaa hizo.
Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda
hicho utatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kuuza majani, mifugo na
mazao ya chakula kama mtama, mahindi, ambapo tayari wameanza kuhamasisha
jamii za wafugaji na wakulima wa Mvomero, Ngerengere na sehemu
zinazozunguka eneo la kiwanda kuchangamkia fursa hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero kufanya mapitio ya mashamba ili
kujua wamiliki wake na kama hawajayaendeleza wachukue uamuzi wa haraka
wa kuyatwaa na kuyarudisha mikononi mwa Serikali.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo
wakati akijibu ujumbe uliokuwa katika mabango yaliyobebwa na wananchi wa
kijiji cha Maji ya Chumvi wilayani Mvomero waliosimamisha msafara
wakati ukitokea kwenye kiwanda cha nyama.
Mama Kanumba azindua “Kanumba Star Search”
Mshiriki
Mkuu wa Shindano la Kanumba Star Search, Florence Mutegoa (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya AM Arts
Promotion pamoja na Mdhamini wa Shindano la “Kanumba Star Search” kwenye
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) leo tarehe 03.08.2016 Jijini Dar es Salaam,
………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mshiriki Mkuu wa Shindano la
Kanumba Star Search, Florence Mutegoa (Mama Kanumba) amezindua shindano
la kusaka vipaji vya waigizaji watakaoigiza filamu itakayoenzi maisha ya
Marehemu Steven Kanumba.
Uzinduzi huo umefanywa leo Jijini
Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambapo
Mshiriki Mkuu wa Shindano hilo ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa
wingi kudhamini shindano hilo litakaloibua vipaji vipya vya uigizaji.
“Tunatambua thamani ya maigizo
ndio sababu tumeamua kuanzisha shindano hili ili kuibua vipaji
vilivyojificha, hivyo tunawakaribisha wananchi wote wenye uwezo wa
kuigiza waje washiriki kwenye mashindano yetu pia tunaomba wadhamini
kujitokeza zaidi ili watusaidie kufanikisha shindano hili”, alisema
Mutegoa.
Mutegoa amefafanua kuwa shindano
hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Kanumba the Great Film
na Kampuni ya AM Arts Promotion ambapo hadi sasa shindano hilo lina
mdhamini mmoja kutoka Kampuni ya simu za mkononi za KZG – Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya AM Arts Promotion, James Mwombeki amesema kuwa
marehemu Kanumba alikuwa na mchango mkubwa katika kuitangaza nchi
kimataifa pamoja na kuibua vipaji vya wasanii wa maigizo hivyo hatuna
budi kumuenzi kwa kuiendeleza Sanaa ya uigizaji.
“Sisi kama AM Arts Promotion
tumeamua kushirikiana kwa pamoja na Mama Kanumba kufanya shindano hili
kwa nia ya kuendeleza tasnia ya filamu nchini kama vile marehemu Kanumba
alivyokua akijitahidi kuwapa fursa ya uigizaji watu wa kila rika”,
alisema Mwombeki.
Naye, Msanii wa filamu, Mayasa
Mrisho amewasisitiza wananchi kushiriki kwa wingi kwenye mashindano hayo
kwani Sanaa ya uigizaji ni njia mojawapo ya kujipatia kipato na kuinua
maisha ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Mkurugenzi wa Kampuni ya
Simu za Mkononi za KZG – Tanzania, Raymond Kalikawe amesema kuwa
wamekubali kuwa wadhamini wa shindano hilo kwa kuwa ukuzaji wa vipaji
vya wasanii wa maigizo ni jambo muhimu pia amewaomba wadhamini wengine
kujitokeza zaidi kusaidia shindano hilo.
Shindano hilo linatarajiwa kuanza
mwezi Septemba mwaka huu, litaanzia Mikoa ya Kanda ya ziwa na baadae
kuendelea katika Mikoa mingine.Washindi wataigiza filamu ya kumuenzi
marehemu Kanumba itakayojulikana kama “Maisha ya Kanumba.
KITUO CHA TELEVISHENI CHA TV 1 KURUSHA MATANGAZO YA LIGI KUU SOKA YA UINGEREZA EPL
Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati),akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo
cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa
moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo
ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes, kushoto ni Felix Awino
Meneja
Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu (katikati), akizungumza katika mkutano
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha
Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja
ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo
yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa TV
1, Joseph Sayi na kulia ni Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah.
Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah (katikati), akizungumzia masuala ya mpira katika mkutano huo.
Production Meneja wa TV 1, Mukhsin Khalfan Mambo akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakiwa kazini.
Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.
Mchambuzi wa michezo, Ally Kashushu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Mmiliki wa Blog ya Kajuna Son, Cathibert Kajuna (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
Wapiga picha za habari wakiwa kazini.
Baadhi ya wafanyakazi wa TV 1 wakiwa wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano.
Mkutano ukiendelea.
………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
KITUO
cha Televisheni cha TV1 Tanzania kinatarajia kuanza kurusha matangazo
ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL
matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu.
Ligi
kuu soka nchini Uingereza ndio ligi maarufu zaidi duniani na hii ni
kutokana na kushirikisha timu kongwe zenye ubora na mashabiki dunia
nzima ikiundwa na timu maarufu duniani kama vile Manchester
United,Liverpool, Arsenal pamoja na Chelsea.
TV1
Tanzania ndio kitakuwa kituo pekee cha runinga hapa nchini kupewa haki
za kurusha matangazo haya yatakayokujia moja kwa moja yaani Live
yakihusisha pia uchambuzi wa ligi hiyo ambapo kutakuwa na vipindi vya
kabla ya mechi na baada ya mechi husika.
Kwa
upande Mkuu wa Kituo cha TV 1 Tanzania Joseph Sayi alisema hii ni
fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa
moja, Mkuu wa kitengo cha masoko wa TV1 Gillian Rugumamu alisema lengo
ni kuwapelekea watazamaji wao wa Tanzania ligi kuu England ambayo ni
ligi inayopendwa na kufuatiliwa na Watanzania.
Baadhi
ya watangazaji na wachambuzi watakaokuwa wakishiriki katika urushaji wa
matangazo hayo na uchambuzi ni Ally Kashushu na Dkt. Leakey Abdallah
ambaye ni mchambuzi mwenye uzoefu wa miaka 20 kwenye tasnia ya michezo
husasani uchambuzi.
Mchambuzi
wa Michezo Dk. Leakey alisema watanzania wategemee uhondo wa ligi hiyo
kutokana na uwepo wa wachezaji nyota na makocha mahiri kama Antonio
Conte,Arsene Wenger,Jurgen Klopp na makocha hasimu Jose Mourinho wa
Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.
Tv1
Tanzania ni kituo cha runinga kilianza mwaka 2013 ambapo kilianza
kurusha matangazo yake rasmi Januari 2014 ambapo kimekuwa kikiandaa na
kurushwa vipindi vyenye ubora wa hali ya juu ambapo TV 1 inapatikana
kupitia ving’amuzi vya Startimes namba 103,Azam 119 na Ting 36.
Filamu mpya ya “The Foundation” by J.Plus
Watakushangaa
sana pale utakapo zungumzia Tasnia ya filamu za Action Tanzania bila
kumtaja Mwasisi wa Filamu hizo Jimmy Mponda maarufu kama J.Plus ambaye
ndiye mmiliki wa ‘Mzimuni Theatre Arts’ aliyewahi kushikiria ubora wake
miaka 5 kwa filamu yake ya “Misukosuko” yaani 2005-2010.
Kwa madai yake J.Plus,
amesema kuwa baada ya kufanya vizuri kwa muda mrefu miaka kadhaa
iliyopita, kisha kukaa kimya ili kuwaachia nafasi wasanii wengine waweze
kuonesha uwezo wao katika Tasnia hio, kwa sasa amedai ni wakati wake
tena.
Kwa maana hiyo J.Plus
ameamua kurejea tena ulingoni ili kuitetea tasnia hiyo coz ameona kama
ina legea legea na huenda ikapoteza ubora kwa mashabiki wa Filamu za
Action Tanzania.
Baada ya siku chache,
J.Plus anategemea kuachia Filamu yake mpya inayoitwa “The Foundation”
ambayo ndani yake amecheza pia Inspector Seba. Akipiga stori na
mwandishi wetu J.Plus alimaliza kwa kusema,
“Kwanza Nashukuru Mungu
kwa uzima, ukimya wangu haukuwa wa nia mbaya bali ni katika harakati za
kuboresha kazi zangu, na kuangalia nini niwaletee mashabiki wangu ili
walizike. Ujio huu utakuwa katika kasi kubwa maana lengo ni kutoa kitu
juu ya kitu, Nitaanza na Filamu ya “The Foundation” ambayo nimecheza na
Inspector Seba ‘I hope’ itarudisha heshima ya Action Movies Tanzania.
Ombi langu kwa watanzania ni mapokezi mema kutoka kwao ushauri na maoni
pia ni muhimu kwenye ufanisi wa kazi zetu asante”
HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA YADHAMIRIA KUOKOA MIL.516.792
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha
,itaokoa sh.mil.516.792 katika mwaka wa fedha 2016/2017,zilizokuwa
zikipotea katika makusanyo ya ushuru wa mchanga,machinjio na stend
kutokana na udanganyifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya mawakala.
Awali halmashauri hiyo ilikuwa
ikitumia mawakala kukusanya ushuru wa vyanzo hivyo vya mapato na
kusababisha upotevu huo wa fedha .
Akitoa ufafanuzi juu ya suala
hilo,mjini Kibaha,mwenyekiti wa halmashauri ya Mji huo ,Leonard Mloe
,alisema aligundua kuwepo kwa udanganyifu huo hivyo kuamua kuagiza
makundi ya madiwani kwenda kufuatilia.
“Baada ya kuwaagiza madiwani hao
kufanya uchunguzi ndipo kulipobainika kweli kulikuwa na upotevu mkubwa
wa fedha ambazo zilikuwa zikifaidisha mawakala kuliko
halmashauri”alisema Mloe.
Mloe alielezea kuwa kati ya fedha
hizo zitakazookolewa ni pamoja na mil.335.392 zilizokuwa zikipotea kwa
mwaka kwenye ushuru wa mchanga.
Alisema katika ushuru wa mchanga
walikuwa wakipokea mil.264.608 kwa mwaka ambapo baada ya kutuma madiwani
waligundua watakuwa wakipata mil.600 kwa mwaka.
“Katika ushuru wa stend
,halmashauri ilikuwa ikipokea makusanyo ya sh.mil.320 kwa mwaka baada ya
uchunguzi tumebaini tunapata mil.458 kwa kipindi hicho na kuokoa mil
138 zilizokuwa zikipotea”alisema Mloe.
Mloe alisema upande wa machinjio
walipata mil.25 kwenye tathmini imebainika fedha halisi zinazopatikana
ni mil.68.400 hivyo wameokoa mil 43.400.
Aidha mwenyekiti huyo,alieleza
vyanzo vyote,vya halmashauri hiyo, vibadilike hesabu zake kuanzia sasa
kwani wanahitaji mapato yanayoendana na chanzo cha mapato.
Mloe alisema kuanzia sasa halmashauri hiyo imeanza kutumia vibarua watakaokuwa wanakusanya ushuru wa vyanzo hivyo kwa usimamizi wa watendaji wa halmashauri badala ya mawakala ambao wamebainika sio waaminifu.
“Vibarua hawa watatumiwa ndani ya miezi mitatu na baada ya hapo watakuwa wakibadilishwa ili kuondokana na tatizo la kupotea kwa fedha”alisisitiza Mloe.
Mloe alisema kuanzia sasa halmashauri hiyo imeanza kutumia vibarua watakaokuwa wanakusanya ushuru wa vyanzo hivyo kwa usimamizi wa watendaji wa halmashauri badala ya mawakala ambao wamebainika sio waaminifu.
“Vibarua hawa watatumiwa ndani ya miezi mitatu na baada ya hapo watakuwa wakibadilishwa ili kuondokana na tatizo la kupotea kwa fedha”alisisitiza Mloe.
Akingumzia kuhusiana na makusanyo
ya mwaka 2015/2016 ,makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Robert
Machumbe,alisema halmashauri ilikisia kukusanya zaidi ya bil.31.836.942
kutokana na vyanzo vyake vya mapato mbalimbali.
Alielezea kuwa halmashauri kwa
robo ya nne inayoishia mwezi juni 2016 imekusanya bil.7.370.215.637 na
kufanya jumla ya mapato yaliyokwisha kukusanywa kwa kipindi cha robo
zote nne kuanzia Julai-Juni 2016 kuwa zaidi ya bil.25.938 sawa na
asilimia 81 ya makisio ya kipindi hicho.
Machumbe alisema halmashauri ya Mji huo imekisia kutumia zaidi ya bil.31.836 kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi wa mji huo
Alieleza katika utekelezaji wa
shughuli zake kwa robo ya nne iliyoishia juni 2016 imetumia
bil.5.950.420 na kufanya jumla ya matumizi kwa julai/juni mwaka huu
kufikia bil.21.614.164 sawa na asilimia 67 ya makisio.
POLISI KUBORESHA VITUO VYAKE VYA AFYA.
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na
Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua
kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi
na tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la
JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika
mkoani Dodoma.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Naibu Inspekta Jenerali wa
Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa
kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na
Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini
kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la
Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika mkoani Dodoma.Kulia ni
Mganga mkuu wa Polisi Dk.Janda Lushina na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Lazaro Mambosasa
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Baadhi
ya Maofisa wa Polisi ambao ni Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi
wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu ndani ya Jeshi la Polisi
wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mkoani Dodoma.Mradi
huo unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na
tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la
JSI-AIDS Free tawi la Tanzania. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Dodoma
Jeshi la Polisi nchini
litaendelea kuboresha vituo vyake vya afya ili kuwawezesha Askari kupata
huduma zilizo bora jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi wakiwa na
afya pamoja na morali katika kupambana na uhalifu nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki Mkoani Dodoma wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua
kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi
na tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la
JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.
Kaniki alizitaja juhudi
zinazoendelea kuchukuliwa kuwa ni pamoja na kuboresha majengo, kutoa
mafunzo kwa watendaji pamoja na kuhakikisha kuwa hospitali za Polisi
zinakuwa na vifaa bora kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Wizara ya
Afya .
Aidha alitoa wito kwa Shirika
la JSI-AIDS Free kuongeza wigo wa huduma zake katika vituo vngine
ambavyo havijafikiwa na mradi huo hapa nchini ili kuhakikisha kuwa kila
mahali palipo na kituo cha Afya cha Polisi kunakuwepo na mradi huo ambao
umesaidia sana askari na watumiaji wengine wa huduma hizo.
Kwa upande wake Mwakilishi
mkazi wa Shirika hilo kwa upande wa Tanzania Dk.Beati Mboya alisema
lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ili kubaini mafanikio na
changamoto zinazovikabili vituo vinavyotekeleza mradi huo ilikuzipatia
ufumbuzi.
Alisema wanatarajia kufanya
tathmini hiyo kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha hakuna
ucheleweshaji katika kutoa huduma baada ya kubaini changamoto na
kuzifanyia kazi kwa haraka.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Afya
cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Paul
Kasabago alisema kikosi hicho kitaendelea kutoa huduma zilizobora ili
kuimarisha afya za Askari na familia zao kote nchini licha ya kukabiliwa
na upungufu wa wahudumu wa Afya.
Kilele Maadhimisho Siku ya vijana Kitaifa kufanyika Mkoani Simiyu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Anthony Mavunde akiongea na waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es
salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani inayoadhimishwa
Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani Simiyu ambapo vijana wametakiwa kutumia
fursa zilizopo kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na Kushoto
ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajiara
na Wenye Ulemavu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Anthony Mavunde akisisitiza umuhimu wa wa wadau mbalimbali
kujitokeza kusaidia jitihada za Serikali kuwawezesha Vijana kiuchumi.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi
Vijana Ajiara na Wenye Ulemavu.
Baadhi
ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde na
waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku
ya Vijana Duniani itakayoadhimishwa Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani
Simiyu.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo
………………………………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku
ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika
Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa
Habari.
Mhe Mavunde amebainisha kuwa
Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa
uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.
Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo
Mhe. Mavunde amesema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi
wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika
shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi
ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili
kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 20130.
Akizungumzia maadhimisho hayo
Kitaifa Mhe . Mavunde amesema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki
shughuli mbalimbali kama makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya
Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.
“Tanzania tutasherekea siku ya
Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa
tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na
Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Wazo la kuwa na siku ya Vijana
Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991
Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha
fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku
ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu
ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Wananchi Zanzibar watakiwa kulipia huduma ya maji
Na Rahma Khamis Maelezo -Zanzibar
Wananchi wa Zanzibar wametakiwa
kulipia huduma ya maji kwa wakati ili kuweza kupata huduma hiyo kwa
ufanisi zaidi na kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza.
Wito huo umetolewa na Afisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Zahour Suleiman Ofisini
kwake Msikiti Mabuluu Mjini Zanzibar wakati akitoa maelezo kuhusiana na
ulipaji wa huduma ya maji.
Amesema maji ni moja ya huduma
muhimu katika maisha ya wananchi hivyo ni muhimu kuhakikisha
yanapatikana muda wote na suala la kulipia huduma hiyo ili iwe
endelevu ni jambo la msingi.
Afisa huyo amefahamisha kuwa
badhi ya wananchi wamekuwa na mwamko mdogo katika kulipia huduma ya
maji na kusababisha Mamlaka kukosa uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa
ufanisi.
Aidha amesema kuwa kwa sasa
huduma hiyo inaelekea kuzidiwa kutokana na kukuwa kwa harakati za
kimaendeleo hasa kwa matumizi ya kilimo ambacho kinatumia maji mengi
ukilinganisha na matumizi ya majumbani.
Afisa huyo amefahamisha kuwa
wameanzisha utaratibu wa kupita katika maeneo kwa lengo la kutoa elimu
kuhusiana na umuhimu wa kulipia maji na wale watakaoshindwa kuufahamu
mpango huo Mamlaka huwapa onyo na baadae kusitishwa kupata huduma.
Sambamba na hayo Zahour
amewashauri wanajamii kufuata sheria bila ya kushurutishwa kwa kulipia
maji kwa wakati ili kuipa uwezo Mmlaka ya maji kutekeleza wajibu wake wa
kuwapatia wananchi huduma hiyo kama kawaida.
MHE SPIKA NDUGAI ALIPOKUTANA NA MHE MBOWE
Kiongozi
wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar
es Salaam.Spika wa Bunge amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini
India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini
Dar es Salaam.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini
Dar es Salaam.
Kiongozi
wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akiagana na
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alipomtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar
es Salaam.(Picha na Ofisi ya Bunge)
Utumishi yapokea vijana wa kujitolea kutoka Japani
Serikali
ya Tanzania inadhamini mchango mkubwa unaotolewa na Serikali ya Japani
kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) ambalo
limekuwa likishirikiana na Serikali katika kazi mbalimbali za maendeleo
hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi
alisema hayo mapema leo katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi wakati wa
hafla fupi ya kuwakaribisha watalaam wa kujitolea kutoka Japani.
“Tangu mwaka 1967 hadi sasa zaidi
ya vijana wa Japani 1,500 wameshafika nchini na kufanya kazi za
kujitolea katika maeneo mbalimbali hata katika mazingira magumu” Bi.
Mlawi alisema na kuongeza kuwa kunufaika huko kwa Tanzania kunatokana
na ushirikano baina ya Serikali ya Japani na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Alisema Tanzania itaendelea
kudumisha ushirikiano huo na Japani ili kuendelea kunufaika hasa
katika suala zima la kujengewa uwezo katika sekta ya elimu na maendeleo
ya jamii , sekta ambazo pia zimepewa kipaumbele katika Awamu ya Pili
ya Mpango wa Serikali wa miaka Mitano (5) wa Maendeleo inayoanza mwaka
2016/17 na kumalizika mwaka 2021 /22.
Kwa upande wake, mwakilishi mkuu
wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo Japani (JICA) nchini Tanzania
Bw. Toshio Nagase alisema wataalam hao ambao wako sita (6)
watafanyakazi ya kujitolea katika sekta ya elimu kwa miaka miwili na
kwa kipindi hicho wanaamini Watanzania watakuwa wamenufaika na ujuzi
toka kwa vijana hao.
Alisema watajitolea kufundisha
masomo ya Sayansi, Hisabati, Masuala ya Maendeleo ya Jamii na Michezo
katika shule za Sekondari , Shule za Msingi na Ofisi za Maendeleo ya
Jamii katika Mikoa ya Morogoro, Pwani , Mtwara , Dodoma na Dar es
salaam.
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UTURUKI, MWAKILISHI UNHCR NCHINI
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akizungumza na
Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki. Mazungumzo hayo yalifanyika
ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimsikiliza
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Chansa Kapaya alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es
Salaam leo. Viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia
Wakimbizi nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza
Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp alipomtembelea ofisini kwake,
jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki. Mazungumzo hayo yalifanyika
ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (katikati) akizungumza
na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya
kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa
Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimkaribisha
ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin
Eralp kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimkaribisha
ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya.Viongozi hao
walijadiliana masuala mbalimbali jinsi ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
NHIF YASHIRIKI MAONESHO YA 8/8 KITAIFA NGONGO MKOANI LINDI KWA UPIMAJI WA AFYA NA UTOAJI ELIMU KWA UMMA
Meneja
wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Raymond
akiwapa maelezo ya mpango wa KIKOA unaowawezesha
wanavikundi,wajasiriamali kupata huduma za matibabu kuchangia mara moja
kwa mwaka (Shs 76,800),kwa wananchi waliotembelea katika banda la mfuko
lililopo kwenye viwanja vya Ngongo mjini Lind
Timu
ya wataalamu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya wakiendelea na zoezi la
upimaji wa afya kwenye magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi waliofika
kwenye banda la mfuko ngongo mjini Lindi.
Ofisa
matekelezo wa bima ya afya Salvatory Okum akitoa maelezo ya faida na
umuhimu wa uchangiaji wa huduma za matibabu kupitia mfuko wa afya ya
jamii (CHF) kwa wananchi waliotembelea banda la mfuko ambapo elimu kwa
umma ni moja ya huduma zinazotolewa.
CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA ZANZIBAR CHAANZISHA MPANGO WA KUWAPELEKA WANAFUNZI WAKE KUFANYA MAZOEZI YA VITENDO KATIKA TAASISI ZA KIJAMII
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar wakifuatilia
ufungaji wa mafunzo elekezi yaliyofanyika katika Chuo chao Chwaka Mkoa
Kusini Unguja.
Mratibu
wa mafunzo elekezi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar
Said Mohd Khamis akieleza lengo la Chuo kuanzisha mpango wa wanafunzi
kufanya mazoezi ya vitendo katika taasisi za kijamii.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na
Watoto Mauwa Makame Rajab akifunga mafunzo elekezi ya wanafunzi wa Chuo
cha Uongozi wa Fedha Zanzibar watakaoshiriki mazoezi ya vitendo katika
vikundi vya kijamii (kushoto) Mkurugenzi wa Vyama vya Ushirika Zanzibar
Khamis Simba na (kulia) Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt. Iddi.
…………………………………………………………………………………….
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
CHUO cha Uongozi wa Fedha
Zanzibar (ZIFA) kimeanzisha mpango wa kuwapeleka wanafunzi wa Chuo hicho
kufanya mazoezi ya vitendo katika vikundi vya Kijamii (SACCOS) kuanzia
mwaka huu.
Uamuzi huo unafuatia muongozo
uliotolewa na Baraza la Chuo baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi
wanapokuwa katika mazoezi ya vitendo katika Mawizara, Maidara na Taasisi
za Umma wanakaa maofisini bila ya kufanya kazi yoyote na kutofaidika na
mazoezi yao.
Jumla ya wanafunzi 130 wa mwaka
wa pili shahada ya kwanza wanaosoma fani ya Uhasibu, Manunuzi na Tehama
wataanza mazoezi ya vitendo katika SACCOS za Unguja na Pemba baada ya
kupatiwa mafunzo elekezi ya siku tatu yaliyotolewa na Idara ya Vyama vya
Ushirika kwa kushirikiana na ZIFA.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,
Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa
Fedha Maalim Said Mohd Khamis alisema lengo la mpango huo ni kuwawezesha
wanafunzi kutoa elimu kwa jamii baada ya masomo yao.
Amesema vyama vingi vya ushirika
vinakabiliwa na matatizo hasa katika masuala ya uhasibu, manunuzi na
matumizi ya Tehama hivyo wanafunzi wao watakwenda kusaidia katika kutoa
elimu kwa wanachama wa vikundi hivyo.
‘’Wanafunzi wetu watakwenda
kufundisha matumizi ya Teknolojia ya kisasa, utaratibu mzuri wa manunuzi
na masuala ya uhasibu”, alisisitiza Maalim Said.
Ameongeza kuwa mtazamo wa Chuo ni
kutoa huduma na fursa zinazopatikana chuoni hapo kwa jamii ili
kuisaidia Serikali katika juhudi zake za kuwapunguzia wananchi hali
ngumu ya maisha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,
Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mauwa Makame Rajab
amewaeleza wanafunzi hao kuwa baadhi ya SACCOS wanachama wake hawana
taaluma kubwa katika masuala ya ushirika hivyo mchango wao utasaidia
sana katika kuviimarisha vikundi hivyo.
Amewataka vijana hao kuitumia
elimu waliyonayo na fursa waliyopata ya kufanyakazi katika vikundi vya
kijamii vijijini kujiajiri kwa kuanzisha SACCOS ama kuongoza ziliopo
katika kukabiliana na tatizo kubwa la ajira liliopo.
Amewashauri wanafunzi hao kuwa
mabalozi wazuri katika sehemu watakazokwenda kupinga vitendo vya
udhalilishaji wa kijinsia vinavyozidi kuongozeka katika maeneo mbali
mbali ya Unguja na Pemba.
Aidha amevishauri vyuo vyengine
viliopo Zanzibar na Tanzania kwa jumla kuiga mfano ulioonyeshwa na ZIFA
kuwapeleka wanafunzi wao kufanya mazoezi ya vitendo katika vikundi vya
kijamii kusaidia masuala mbali mbali ikiwemo sheria, uongozi demokrasia
ndani ya vikundi vyao.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa
Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar amesema wameupokea mpango wa Chuo
kwenda kusaidia vikundi vya ushirika vijijini kwa moyo safi na ameahidi
watatoa mchango mkubwa.
Amesema wanauchukulia mpango huo
kama ni majaribio kwao na watajitahidi kuweka mazingira mazuri na kuwa
mfano wa kuigwa na wanafunzi wenzao watakaofuata hapo baadae.
MTOTO ATOA MSAADA WA MADAWATI DODOMA
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme (kushoto) akimshukuru mtoto Aisha
Mshantu kwa Msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5.2
aliyoyatoa katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala
Manispaa ya Dodoma. PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA
Mtoto
Aisha Mshantu (kulia )akimkabidhi madawati 50 yenye thamani ya
shilingi milioni 5.2 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme
aliyoyatoa katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala
Manispaa ya Dodoma. PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA
Mtoto Aisha Mshantu na wazazi wake Mzee Mshantu (wa kwanza kulia) na Bi
Rehema (wa pili kulia) wakiwa amekaa katika madawati aliyoyatoa mtoto
huyo kama msaada katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala
Manispaa ya Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina
Mndeme. PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA
PPF KATIKA MAONYESHO YA NANENANE LINDI
Afisa
uhusiano mwandamizi wa mfuko wa Pensheni wa PPF Janet Ezekiel
akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi shughuli
zinazofanya na mfuko ikiwemo faida ya kujiunga na mfuko wa wote
Scheme wakati alipokuwa anatembelea banda la mfuko huyo jana
Mfuko
wa Pensheni wa PPF umeshiriki maonesho ya nane nane yanayofanyika
kitaifa Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi ambayo
yamefunguliwa na waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo kwa
niaba ya Makamu wa rais Samia Suluhu yenye kauli mbinu KILIMO
MIFUNGO NA UVUVI NI NGUZO YA MAENDELEO VIJANA SHIRIKI KIKAMILIFU HAPA
KAZI TU. Kupitia fursa hiyo ya maonyesho hayo PPF inakutana na
wadau mbalimbali kueleza huduma zinazotolewa na shirika hilo
ikiwemo WOTE SCHEME mfumo wa maalumu wa kuchangia unazihusisha
sekta isiyo rasmi pamoja na ule mfumo wa ziada kwa sekta iliyo
rasmi
No comments :
Post a Comment