Wednesday, August 3, 2016

WAZIRI MAHIGA AMPOKEA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UFARANSA


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Jean-Marc Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya kikazi nchini. 

Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia maendeleo ya nchi hizi mbili. 

Pia Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kumpa salamu za pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi karibuni. 

Mazungumzo hayo yalifanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2016   Waziri Mahiga akizungumza huku Mhe. Waziri Ayrault akimsikiliza. Wajumbe waliofuatana na Mhe. Waziri Aryault nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Malika Berak Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean-Marc Ayrault akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Mahiga alipotembelea Wizarani leo. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha nao wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.

DONALD TRUMP AJIBU MAPIGO ASEMA KIPINDI CHA URAIS CHA OBAMA NI 'MAJANGA'

Donald Trump amesema kipindi cha rais Barack Obama madaraka ni 'majanga', kauli ambayo ameitoa baada ya rais Obama kusema hafai kuwa rais.

Mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Bw. Trump akiongea na Fox News amesema Obama amekuwa dhaifu, asiemudu madaraka hayo.

Rais Obama alimkosoa Bw. Trump na kuhoji kwanini chama chake, hakikumzuia kuwania kugombea urais wa Marekani.

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA NA STENDI YA MSAMVU MOROGORO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiteremka kuelekea eneo la kuchinjia ng'ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua eneo la kuchinjia ng'ombe katika kiwanda cha nyama cha Nguru Hills Ranch cha Morogoro Agosti 3, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda hicho, Danstan Mrutu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizingumza na Mkurugenzi na mshauri wa kiwanda cha nyama cha Ngulu Hills Ranch cha Morogoro , Dunstan Mrutu (kulia kwa Waziri mkuu) ) wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watoto na wananchi wa kijiji cha Majichumvi wilayani Mvomero wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao kuwasikiliza Agosti 3, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga wakati alipokagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU AWATAKA WAFUGAJI WAKUBWA KUJIANDAA KUFUGA KISASA

JAMII YATAKIWA KUWAPA USHIRIKIANO WASICHANA WANAOSHIRIKI MASHINDANO YA UREMBO

Warembo wanaoshiriki shindano la miss kanda ya kaskazini kutoka katika mikoa ya Arusha,Manyara,Tanga na Kilimanjaro wakiwa nje ya hotel ya Clous view sehemu ambayo wanafanyia mazoezi kwa ajili ya shindano hilo linalofanyika july 6 katika viwanja vya ukumbi wa Triple A fm
Warembo hao wakiwa katika pozi

ZRB YASEMA MAPATO KWA MWEZI JUNI MWAKA HUU YAMEFIKIA BILIONI 16

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Umma za Fedha Zanzibar Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d.
Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar { ZRB } Ndugu Hamil Bakari aliyepo kati kati akifafanua jambo wakati wa kikao cha Watendaji wakuu wa Taasisi za Fedha na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akimueleza Balozi Mikakati inayochukuliwa na Wizara yake katika suala zima la ukusanyaji wa Mapato ya Serikali. Picha na –OMPR – ZNZ.


Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar { ZRB } Ndugu Hamil Bakari alisema kwamba makusanyo ya Mapato kwa mwezi wa Juni mwaka huu yamefikia shilingi Bilioni Kumi na Sita ikikadiriwa kufikia lengo la makusanyo ya shilingi Bilioni Ishirini mwezi Julai mwaka huu.

Hata hivyo alisema yapo baadhi ya makusanyo yanayofikia shilingi Bilioni Mbili ambayo hupatikana kutokana na mapato ya Wizara na Taasisi mbali mbali za Umma.

Kamishna Hamil Bakari alitoa takwimu hizo katika kikao cha pamoja kati ya Watendaji Wakuu wa Taasisi za Fedha wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d walipokutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Balozi Seif ameitisha Kikao hicho ikiwa ni muendelezo wa Mikutano yake ya kukutana na watendaji wapya wa Taasisi hizo kwa kutambuana kufuatia mabadiliko ya muundo mpya wa Serikali sambamba na kuangalia fursa za kukabiliana na changamoto zinazozikabili Taasisi hizo.

TAZARA WACHANGIA DAMU WAKIADHIMISHA MIAKA 40 YA UWEPO WAO


Zoezi la uchangiaji Damu likiendelea katika makao makuu ya TAZARA ambapo wafanyakazi mbalimbali wa Shirika hilo na watanzania wengine wamejitokeza kucnagia damu (PICHA NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI)
Wakati Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA wakiadhimisha miaka 40 ya uwepo wake nchini Tanzania maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi maalum la kuchangia damu zoezi ambalo limefanyika makao makuu ya TAZARA Dar es salaam Tanzania ambapo wafanyakazi wake wameitumia siku ya leo kuchangia damu zoezi ambalo liliongozwa na mpango wa Taifa wa damu salama Tanzania.
Akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo Tanzania wao kama TAZARA wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya kufanya zoezi moja la kuchagia damu zoezi ambalo linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU akizngumza na wanahabari wakati wakiendelea na zoezi la ucnagiaji wa Damu 
Amesema kuwa zoezi hilo linaonyesha ni jinsi gani wafanyakazi wa TAZARA wamekuwa wakiguswa na maswala mbalimbali ya kijamii hususani swala la ukosefu wa Damu mahospitalini huku akiyataka mashirika mengine na watu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachangia damu mara kwa mara wawezavyo kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wamaopoteza maisha yao kwa kukosa Damu.

WATANZANIA WATAKIWA KUTHAMINI BIDHAA ZA NDANI

Na Woinde Shizza. Wito umetolewa kwa Watanzania watumie na kuthamini bidhaa zinazotengenezwa na kupatikana ndani ya nchi badala ya kuzipa kipaumbele bidhaa za nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Old East International ndugu Moses Mwano ,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane njiro Jijini Arusha.

Mwao amesema kuwa Watanzania wengi wanathamini bidhaa zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi,ambazo baadhi hazina kiwango cha ubora unaotakiwa kwa mtumiaji.

Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Old East International amesema kuwa kampuni hiyo ni ya Kitanzania ,imesajiliwa na ipo chini ya Shirika la uwekezaji Tanzania wao ni wawekezaji wa ndani,wanahusika kutengeneza wino wa kuchapia unaofahamika kwa jina la Crown Cartridge.

Kwa upande wake Mwano amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dokta John Magufuli,katika jitihada zake za kuifanya Nchi kuwa ya Viwanda.

Sambamba na hayo amewaasa Watanzania watengeneze na kuingiza Bidhaa zenye kukidhi ubora na viwango ,huku akimalizia na msemo usemao " kizuri cha jiuza kibaya chajitembeza akimaanisha kuwa ukitengeneza bidhaa nzuri yenye kukidhi viwango na ubora unaohitajika wateja watafurahiwa nayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Old East International Moses Mwano akiwa anazungumza na wateja waliotembelea banda hilo katika Maonyesho yanayoendelea katika Viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.

No comments :

Post a Comment