Monday, August 8, 2016

WAZIRI MKUU AITAKA TRA KUACHA TABIA YA KUWAPANDISHIA WAFANYABIASHARA KODI KIHOLELA


TIMU YA ARSENAL YAIZAMISHA MANCHESTER CITY KWA MAGOLI 3-2


DIEGO COSTA, OSCAR, EDEN HAZARD NA PEDRO WAIZAMISHA WERDER BREMEN


KOCHA JOSE MOURINHO AANZA KWA KUTWAA NGAO YA HISANI


TUNAMSUBIRI WAZIRI MKUU


STARTIMES YACHANGIA MADAWATI MKOANI MTWARA

1
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakiwa kwenye baadhi ya madawati yaliyochangiwa na kampuni hiyo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati nchi nzima iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli. Zoezi hio la uchangiaji wa madawati lilifanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mwishoni mwa wiki hii.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakiwa wamekaa kwenye madawati hayo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kulia) , akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mh. Dkt. Khatib Malimi Kazungu
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo.

STAMICO YAWATANGAZIA NEEMA WACHIMBAJI WA MADINI TANZANIA


MTATURU: WANANCHI WANATAKIWA KUFUGA KUKU SIO KUISHI NA KUKU

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua kuku waliofungwa kisasa ambapo jogoo mmoja aliyefikisha umri wa mwaka mmoja anauzwa shilingi 20,000.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la maonesho ya Nanenane la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa Rehema F. Malila kutoka Kijiji cha Unyangwe, Kata ya Iseke ya namna usindikaji unavyofanyika Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipata ufafanuzi kutoka kwa Mratibu wa Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) Edward Bulilo Maselo alipotembelea banda la maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Singida juu ya umuhimu wa jamii kujiunga na mfuko huo

MAJALIWA AWASILI MBEYA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya Agosti 7, 2016 ambako Agosti 8, 2016 atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea heshima kutoka kwa Skauti wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Songwe Agosti 7, 2016 ambako Agosti nane atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakifurahia ngoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya Agosti 7, 2016 ambako Agosti 8, 2016 Mheshimiwa Majaliwa atahitimisha maonyesho ya wakulima Nanenane. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PAUL POGBA ARUHUSIWA NA JUVE KWENDA KUFANYA VIPIMO MAN UTD


MVUA YA GHARIKA YASABABISHA VIFO VYA WATU 20 NCHINI MACEDONIA


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI LINDI


MAJALIWA USO KWA USO NA ASKOFU GWAJIMA


MATARUMA YA KIWANDA CHA KONGOLO CHA TAZARA-MBEYA KUJENGA RELI YA KISASA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kushoto) akitoa maelekezo kwa Afisa Mfawidhi Kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw.Denis Daudi, wakati alipokagua huduma za mabasi katika kituo cha nane nane Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili Kushoto), akikagua moja ya kifaa kinachotumika kwenye Reli wakati alipotembelea kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA), Kongoro Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akikata moja ya kifaa kinachotumika kujengea reli wakati alipotembelea kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, Kongoro Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.

WANANCHI WAZIDI KUFURAHIA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI

Mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho ya Kilimo na Mifugo ya Nanenane Kanda ya Kaskazini yanayofanyika kwenye uwanja wa Taso Themi akipata maelezo kwenye banda la kampuni ya Simba Cement
Meneja Mauzo wa Simba Cement mkoa wa Arusha,Christopher Mgonja(kulia)akimkabidhi mmoja wa wananchi waliotembelea banda hilo,Thomas Mollel kofia na tisheti .
Bwana Shamba wa kampuni ya mbegu ya Seed Co,Lukinga Miho akizungumzia kampuni hiyo kuanza kuzalisha mbegu za mbogamboga ambazo zina soko kubwa ndani na nje ya nchi.

LIVERPOOL YAICHAKAZA BARCELONA KWA MAGOLI MANNE KWA UBUYU

Timu ya Liverpool ya Uingereza imeichakaza Barcelona kwa magoli 4-0 katika mchezo wa kombe la Kimataifa la Mabigwa katika dimba la Wembley.

Katika mchezo huo Sadio Mane alikuwa wakwanza kuifungia Liverpool goli kufuatia shambulizi lililofanywa kwa kuwahusisha Adam Lallana na Philippe Coutinho.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Javier Mascherano alijifunga baada ya kipindi cha pili na kuizawadia timu yake hiyo ya zamani goli la pili.

Divock Origi aliongeza goli la tatu kwa Liverpool kwa kuupitisha mpira kati kati ya miguu ya Claudio Bravo na baadaye Marko Grujic alifunga goli la nne kwa kichwa cha kunyanyua.
             Mchezaji mpya wa Liverpool Sadio Mane akiifungia timu hiyo goli la kwanza
          Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi akishangilia goli lake alilofunga 
        Kipigo kikiwaacha hoi wachezaji wa Barcelona Luis Suarez na Lionel Messi

PAUL POGBA NA RAPA DRAKE WATANUA PAMOJA KWENYE KLABU MAREKANI

Urafiki baina ya rapa Drake na Paul Pogba umeendelea kushika kasi baada ya wawili hao kupigwa picha wakiondoka kwenye klabu ya usiku Jijini New York Marekani jana majira ya alfajiri.

Rapa huyo Mmarekani na mchezaji mpira anayesakwa kwa fedha nyingi, wamekuwa wakila bata, huku Pogb akimkabidhi Drake jezi yake ya Juventus aliyoiweka saini yake baada ya kuhudhuria tamasha huko Madison Square Garden.

Wawili hao waliendelea kuikaribisha wikiendi wakiwa pamoja, huku mchezaji huyo anayewaniwa na Manchester United akiambatana tena na Drake katika kiwanja cha starehe cha Beautique Lounge Jijini New York. 
                        Pogba akimpatia Drake t-shirt yake ya Juventus yenye jina lake
                  Paul Pogba akitoka klabu baada ya kuponda starehe Jijini New York

MWANARIADHA WA AFRIKA KUSINI OSCAR PISTORIUS AUMIA AKIWA GEREZANI

SERENGETI BOYS YAIDINDIA AFRIKA KUSINI

NAIBU WAZIRI JAFO: WATANZANIA WANAPASWA KUTHAMINI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NDANI YA NCHI

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa maonesho ya nane nane Nzuguni mjini Dododma
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa makini maelezo ya kilimo cha mbogamboga yanayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri hiyo
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa makini maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyeji wake katika Maonesho hayo ambaye ni mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji Jumanne Mtaturu

AFRICAN SPEAKERS LOBBY FOR A STRONGER CONTINENTAL ASSEMBLY -WANT AU MEMBER STATES TO RATIFY MALABO PROTOCOL

                                                           A section of the African Speakers in attendance
The Prime Minister of Lesotho, Rt Hon Bethuel Pakalitha Mosisili opens the 8th Conference of Annual Speakers at the PAP headquarters in Midrand, South Africa.
GOOD TO SEE YOU: PAP President, H.E. Roger Nkodo Dang and the EALA Speaker, Rt Hon Daniel F. Kidega in consultation.
EALA Speaker, Rt Hon Daniel F. Kidega shares a light moment with ECOWAS Speaker, Rt Hon Moustapha Cisse earlier today.

East African Legislative Assembly, Midrand, South Africa: August 5, 2016: The 8th Annual Conference of Speakers has opened in Midrand, South Africa. In attendance at the two-day Conference whose theme is from “Adoption of the African Union Treaties in particular the new Protocol of the PAP” are over 30 Speakers from the National Assemblies and Regional Parliaments in the continent.

The Prime Minister of Lesotho, Rt Hon Bethel Pakalita Mosisili opened the two-day conference.

In his remarks, the Prime Minister reiterated the importance of ratifying the Constitutive Act of the African Union relating to the Pan-African Parliament that empowers the continental Assembly to execute its mandate to accord credence to the AU Policies and programmes.


“African States are urged to sign and ratify the Malabo Protocol. In addition, a balance of legislative powers must be struck between the National Parliaments and the Continental Assembly (PAP) to ensure acceptability as we move towards continental free trade area and continental integration” the Premier said.

The Prime Minister called for popular participation and engagement of citizens in the processes. “It is absolutely critical that we carry our people along. It cannot and must not be a leaders’ or a Governments’ issue alone. Our people must fully comprehend, accept and own the process. The need for concerted education on the matter cannot be overemphasized. This is so as to avoid a repeat of what happened in Europe – Brexit”, he added.

LHRC YAMPA MAPOKEZI MAKUBWA MWANAHARAKATI GELINE FUKO AKITOKEA MAREKANI

MKUU WA MKOA WA LINDI ATEMBELEA BANDA LA PPF VIWANJA VYA NANENANE LINDI

SIMBACHAWENE AVUTIWA NA MPANGO WA TOTO AFYA KADI UNAOTOLEWA NA NHIF

Waziri wa Tamisemi,George Simbachawene akipata Maelezo mafupi ya Mpango wa Toto Afya Kadi pamoja na KIKOA,Toka Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi,Fortunata Kullaya,Baada ya Waziri Huyo Kuembelea Mabanda Mbalimbali ya Maonesho ya Nane nane Kanda Ya Kusini,Viwanja vya Ngongo Lindi
Waziri Simbachawene akipokea Vipeperushi vya Mfuko wa Bima ya Afya Toka kwa Sabina Komba kwa Niaba ya Mkurugenzi mkuu wa NHIF Mara baada ya kumaliza kukagua Banda la Mfuko huo linalotoa Huduma mbalimbali za Ushauri,Upimaji pamoja na Uandikishaji wa wanachama ikiwemo wa CHF
Afisa Vijana Mkoa wa Lindi ,Saida Mponjoli alikuwa Mmoja wa Wadau waliotembelea Banda la NHIF Viwanja vya Ngongo
Saidi Ally Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Tulieni Manispaa ya Lindi nae alitembelea Banda Hili kupata Elimu ya Mpango Mpya wa TOTO AFYA KADI

DC IKUNGI AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akikagua vijana wa mafunzo ya Mgambo kutoka vijiji vitano vya Dung’unyi, Munkinya, Kipumbuiko, Samaka na Damankiya vinavyounda Kata ya Dung’unyi katika Tarafa ya Ikungi
Kundi la vijana wa Mgambo kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakionyesha umahiri wao katika mafunzo waliyoyapata mbele ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Ikungi
Kundi la vijana wa Mgambo kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akijadili jambo na Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi Fortunatus Ndalama
Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturua akizungumza na watendaji Kata, na viongozi wa vijiji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya mgambo yatakayodumu kwa wiki 16.

WAZIRI SIMBACHAWENE AKAGUA BANDA YA SSRA,MAONESHO YA NANE NANE VIWANJA VYA NGONGO LINDI

Waziri Simbachawene akipokea Vipeperushi mbali kuhusiana na Shughuli zinazotekelezwa na Mamlaka Hiyo
Picha na Na ; Abdulaziz ,Lindi
Picha ya pamoja kati ya watumishi wa SSRA na Baadhi ya wadau waliotembelea Banda Hilo Ikiwemo wakulima waliotembea Kujifunza jinsi Mifuko ya Jamii Inavyojiendesha Chini ya Usimamizi wa Mamlaka Hiyo
Mmoja wa Wanachama wa Mifuko ya Jamii Ambae alijitambulisha Kwa Mstaafu Mtarajiwa Akipokea Vipeperushi vya Mamlaka Hiyo Toka kwa Sarah Msika
Afisa Uhusiano na Uhamasishaji SSRA,Ally Masaninga akikabidhi Zawadi kwa Bi Saida,Afisa Vijana Mkoa wa Lindi Alietembelea Banda la Mamlaka Hiyo katika Viwanja Vya Ngongo Lindi Manispaa

PAUL POGBA AITWA NA KOCHA WA JUVENTUS KUJIUNGA NA KAMBI YA MAZOEZI

MSANII JAGUAR AMUKOA DEFAO KWA KUMLIPIA DENI LA MALAZI HOTELINI


KENYA YATUMBUKIA GIZANI BAADA YA KUTOKEA KWA HITILAFU YA UMEME

MOTO WAUWA WATU 13 KATIKA SHEREHE YA KUZALIWA NCHINI UFARANSA

SHAMRASHAMRA KIBAO ZAPAMBA UFUNGUZI WA MICHUANO YA OLIMPIKI 2016

DIWANI WA CHADEMA ASWEKWA NDANI KWA KUKIUKA MAADHIMIO YA BARAZA LA MADIWANI WILANI IKUNGI

Kutoka Kushoto ni Eng Sadick Chakka Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga, na Kulia ni Abel Suri Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

                                                                                               Na Mathias Canal, Singida

Jeshi la polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida limemtia nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Emmanuely Njingu kwa kosa la kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali kufanya kazi yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha awali kabla ya kuwekwa nguvuni na jeshi la polisi alivuliwa ujumbe wa kamati hiyo kutokana na kukiuka taratibu na makubaliano ya baraza la madiwani jambo ambalo limepelekea kuhamishiwa katikakamati nyingine.

Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa diwani huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Irisia Ally Juma Mwanga amesema kuwa Diwani huyo amekamatwa kwa mujibu wa sheria hivyo yeye kama mwenyekiti hawezi kuingilia taratibu, sheria,na kanuni za serikali.

Mwanga amesema kuwa tarehe 19 mwezi Julai moja ya maadhimio ya kamati ya fedha na vikao vya baraza ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri lakini diwani huyo amekiuka makubaliano hayo kwa kung’oa mageti ya vizuizi vya barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa mazao jambo ambalo limepelekea kuzorota kwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.

Ameongeza kuwa Mjumbe yeyote anayekiuka maazimio wanayokubaliana na kutoa siri za kamati adhabu yake kisheriani kupoteza sifa ya kuwa mjumbe wa kamati husika.

Amesema diwani huyo ameondoshwa katika nafasi hiyo baada ya maridhiano ya kamati hiyo na kukubaliana kumuhamishia katika kamati nyingine ya huduma za uchumi.

“Jambo mkishakubaliana kisheria tena kwenye vikao vya kisheria maana yake linakuwa ni sheria hivyo kwa kiongozi yeyote akikiuka taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake, kanuni za Halmashauri ni za watu wote hazichagui upande mmoja” Alisema Mwanga

Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alihutubia Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mara yake ya mwanzo kabisa tangu alipochaguliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na kuzungumzia kuwepo kwa changemoto ya uhaba wa maabara, afya duni na miundombinu pia alizungumzia kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato jambo ambalo linairudisha nyuma Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Bajeti ya Wilaya ya Ikungi kwa Mwaka 2013/2014 ilikuwa na Shilingi 509,701,044 namakusanyoyakeyakawa ni 338,325,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kuwa na upungufuwa shilingi 171,376,044.

Mwaka 2014/2015 ilipangwa bajeti ya shilingi 631,455,000 lakini makusanyo yake yakawa ni shilingi 457,555,172 ambapo mwaka ulimalizika kwa kukusanya 173,899,828.

Mwaka wa bajeti 2015/2016 bajeti ya Halmashauri iliyopangwa ilikuwa ni shilingi 1,127,030,000 makusanyo yalikuwa ni 679,283,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kwa kuwa na upungufu wa shilingi 450,747,000 hivyo kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji.

Mwanga amesema kuwa Kutofikiwa malengo hayo kumesababishwa na kutopewa ushirikiano watendaji katika ukusanyaji wa mapato hii ikiwa ni kufuatia kauli za mazuio zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.

Hata hivyo ametoa Mwito kwa viongozi wa serikali, wanasiasa, taasisi za dini na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo ya kuifanya Ikungi kukua kiuchumi .

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANZIBARI BOSTON

                           Wazanzibari wakimsikiliza Maalim Seif (Picha na Swahilivilla)

Karibuni wapenzi Wasomaji wetu katika sehemu ya nne ya mfululizo wetu wa makala ya "Maalim Seif azungumza na Wazanzibari Boston" katika mkutano wake na Wazanzibari uliofanyika katika jimbo la Massachusetts, Marekani 30 Julai 2016.

Katika sehemu iliyopita, Maalim Seif alielezea kile kilichotokea katika uchaguzi wa Oktoba, 2015 mpaka uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016. Sasa endelea na sehemu ya nne:
                                                                               Baada ya Uchaguzi wa Marudio

Kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, hakikupata uungwaji mkono tangu ndani hadi nje ya visiwa hivyo. Jamii ya Kimataifa ilikataa kushiriki katika uangalizi wa uchaguzi huo kwa vile haukuwa na mashiko yoyote ya Uhalali.

Na kwa upande wa ndani, Chama Kikuu cha upinzani Cha Wananchi (CUF) ambacho kiliususia uchaguzi huo hakikuitambua serikali mpya iliyoundwa na Mheshimiwa Ali Mohammed Shein, na kikaamua kuisusia kama kilivyoususia uchaguzi wenyewe.

Maalim Seif alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wameigomea serekali hiyo na sasa iko taabani, na kusisitiza: "Na wala hatushirikiani nayo kwa jambo lolote lile" Aliendelea kuelezea kuwa CUF walikaa kimya kwa muda, jambo ambalo liliwafanya viongozi wa chama Tawala cha CCM waamini kuwa wamemaliza Simba wa Nyika. 

"Tulikaa kimya kwa muda na wao wakadai CUF tumeimaliza......, mpaka tulipoanza ziara za Wilaya mbalimbali Unguja na Pemba zikifuatiwa na kuwatembelea wagonjwa..."

Ni vizuri kukumbusha kuwa Maalim Seif alianza ziara zake hizo kwa kuzitembelea wilaya za Pemba ambako alipokelewa na halaiki ya wananchi waliokuwa wakisema "raisi..raisi...raisi". Kufuatia ziara hizo aliitwa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na kuhojiwa kwa muda wa masaa kadhaa.

Mgomo wa wananchi umeimarika, na umekuwa ukiitikisa serikali na kupelekea ukamataji ovyo wa wananchi kinyume na sheria: "Wameghumiwa, mgomo wa wananchi umeshika kasi...., wakaanza kukamata watu kinyume cha sheria" alisisitiza Maalim Seif.

Badala ya kushughulikia maendeleo ya nchi, serikali imejikita kwenye mikakati ya kuimaliza CUF na wafuasi wake. Hata hivyo, mikakati hiyo imekuwa ikiwaathiri wananchama wa CCM pia. Alitoa mfano wa sakata la kukamatwa ng'ombe na wenyewe kutakiwa kwenda kuwagomboa.

"Kila wanachofanya ni kuwamaliza CUF, lakini ukweli ni kwamba wenye ng'ombe wengi ni wanachama wa CCM", alisema . Maalim Seif aliendelea kufafanua juu ya dhulma wanazofanyiwa raia na mali zao na kutoa mfano wa "jumba la treni", kwa kusema "Watu walihamishwa, kwa ajili ya ukarabati wa jengo lile, na mpaka leo hata ramani haipo" Itakumbukwa kuwa michoro ya kile kinachodaiwa kuwa ni ramani mpya ya mwonekano wa jengo hilo litakavyokuwa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, lakini kwa mujibu wa maelezo ya Maalim Sif, ilikuwa ni kiini macho tu.

Aidha Maalim Seif alifafanua kuwa Mji Mkongwe ni sehemu ya Turathi za Kimataifa. Kwa hivyo uvunjaji wa jengo lolote la kihistoria unapaswa kupata ridhaa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni. Hata hivyo, mpaka wakati tunaingia mitamboni hakuna karatasi yoyote inayoonesha kuwa tayari Serikali ya Zanzibar imewasiliana na kushauriana na shirika hilo. 

Kwa hivyo ni wazi kuwa uhamishwaji wa wanachi kutoka jengo la treni ulikuwa na malengo ya kisiasa na kuwadhalilisha wananchi.

                                                                                                  Upande wa Tanzania.

Kwa vile Tanzania ni Jamhuri ya Muungano nchi mbili huru Tanganyika na Zanzibar, yanayotokea upande mmoja yanaathiri upande mwengine wa Muungano huo kwa njia moja au nyengine. Kwa hivyo, Makamo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, hakusahau kuigusia hali ilivyo nchini Tanzania chini ya Utawala wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli. Maalim Seif aliilezea hali ilivyo nchini Tanzania kisiasa kuwa si yakuridhisha, na serikali iliyopo madarakani inaipelekea nchi pabaya.

Maalim Seif alikosoa hatua ya kuzuiliwa vikao vya Bunge kuonehswa moja kwa moja kwenye televisheni, na kusema lengo lake kuu ni kuua upinzani. Hii ni kutokana na kuwa Bunge lenye mijadala huru ndilo linalojenga upinzani.

Akakosoa hatua ya Wabunge 11 wa upinzani kuzuiliwa kushiriki katika vikao vya Bunge bila ya sababu yoyote ya kimsingi: "Nini kosa lao?, alihoji Maalim Seif, na kujibu mwenyewe kuwa: "Kosa lao kubwa ni kuikosoa Serikali".

Alielezea masikitiko yake kuwa majimbo ambayo Wabunge wao wamezuiliwa yatakosa uwakilishi Bungeni kwa muda mrefu kwani wengine wamefungiwa mpaka mwezi wa Januari mwakani.

Akijibu swali iwapo kuna Mbunge yeyote wa CUF kati ya 11 waliofungiwa, Maalim Seif mwenye upeo wa kuona mbali alisema kuwa hakuna Mbunge yeyote kutoka chama hicho kati ya hao walioathirika na hatua hiyo na kusisitiza: "Nia ni kuugawa upinzani, ili waseme kuwa CUF ni wasaliti"



Alifafanua kauli hiyo kwa kusema kuwa kuna Wabunge wengi wa CUF ambao ni wasemaji wazuri na wakosoaji wakubwa wa Serikali, lakini hawakufungiwa ili watu wenye nyoyo dhaifu waone kuwa CUF ni wasaliti, au vibaraka.

Aidha, mwanasiasa huyo shupavu, aliifananisha hali ilivyo Bungeni na uwanja wa vita kutokana na kuwepo kwa askari wengi ambao mara kadhaa wamekuwa wakiingia ndani ya Bunge."Ukienda Bungeni utadhani uwanja wa vita", alisema.

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI ATEMBELEA SHIRIKA LA TAIFA LA UTANGAZAJI (TBC)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba akimkabizi kitabu ta wageni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea ofisi za Shirika hilo mikocheni mapema leo asubuhi. PICHA ZOTE NA FC GODFREY PETER)
Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (wa kwanza kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mkuu wa TBC Dk. Ayoub Rioba na wa pili ni Kaimu Kamishna wa Usalama dhidi ya moto Fikiri Salla .
Mkurugenzi wa Matukio wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Bi Martha Swai (wa kwanza kulia) akitoa maelezo jinsi ya upokeaji wa habari za matukio mbalimbali kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (katikati) alipotembelea ofisi hizo mapema leo asubuhi (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Dk. Ayoub Rioba .
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyesimama mbele, akimsomea taarifa ya Jeshi hilo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba alipotembelea ofisi za Shirika hilo mapema leo asubuhi
                                                                                                        Kikao kikiendelea
Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (katikati) akipokea maelezo jinsi ya chumba cha matangazo kinavyofanya kazi (Studio) kutoka kwa Mtangazaji Bi Anna Mwasioke hayupo pichani, (kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa TBC Taifa

VIONGOZI WA DINI WATEMBELEA UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM KUONA MAENDELEO YA UJENZI WA TERMINAL 3

Viongozi wa dini wanaounda Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakiomba dua kuombea ujenzi wa Uwanja wa Jengo la Tatu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walipofanya ziara ya siku moja kutembelea jengo hilo Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Mohamed Milanga akitoa maelezo kwa viongozi hao wa dini waliotembelea uwanja huo Dar es Salaam jana.
                                                                   Mwonekano wa uwanja huo unaojengwa.
                                           Mwonekano wa chumba cha wasafiri katika jengo hilo.
                                                                             Baadhi ya wakandarasi wa ujenzi huo.
Askofu, Stephen Mang'ano wa Kanisa la Menonite (kushoto), akiongoza maombi ya kuombea ujenzi wa uwanja huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Ramadhan Maleta (wa pili kulia), akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo mbele ya viongozi wa dini wanaounda Kamati ya Amani.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Wolffgang Marschick akizungumza na viongozi hao wa dini.
Viongozi hao wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kukamilisha ziara yao. Na Dotto Mwaibale

No comments :

Post a Comment