Monday, August 8, 2016

RAIS MAGUFULI ASALI KANISA LA BIKIRA MARIA PAROKIA YA CHATO, ATEMBELEA KANISA LA ANGLIKANA, AIC PAMOJA NA MSIKITI WA OMAR BIN-L-KHATTAB CHATO




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiimba wimbo wa Amani pamoja na Kwaya ya Kanisa la  African Inland Church la Chato Mkoani Geita mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo Agosti 7, 2016


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakisali katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Chato Zacharia Samson mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo la Anglikana Chato Mkoani Geita.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihamasisha mchango wa ujenzi wa Kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waamini wa kanisa Katoliki wa Parokia ya Chato mara baada ya Ibada katika kanisa hilo Chato Mkoani Geita.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Padre wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Henry Mulinganisa mara baada ya kushiriki Ibada katika Kanisa hilo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Mwalimu wake wa zamani wa Shule ya Msingi Chato Mkoani GeitaMwalimu Mkuu Mstaafu  Jackson Nyamwaga mara baada ya kumuona wakati akitoka katika Kanisa la  African Inland Church la Chato Mkoani Geita.


Shekhe wa Bakwata Wilaya ya Chato Hassan Issa Mnubi akiongoza dua ya Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli nje ya Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab Chato Mkoani Geita. PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono waamini wa Kanisa Katoliki Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita hawapo pichani mara baada ya kushiriki Ibada katika kanisa hilo

 



PPF Nane nane 2016 -1
Baadhi ya Wananchi wakijaza Fomu ya Kujiunga na WOTE SCHEME katika Banda la PPF Viwanja vya Nane Nane Ngongo Kama Picha Inavyoonekana Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel akitoa maelekezo ya Jinsi ya Kujaza Fomu Hizo.
PPF Nane nane 2016 -2
Wananchi waliotembelea Banda la PPF, wakimsikiliza kwa Makini Afisa Masoko PPF Wakati akitoa Elimu Juu ya Mfumo wa WOTE SCHEME.
PPF Nane nane 2016 -3
Baadhi ya Wananchi wakijaza Fomu ya Kujiunga na WOTE SCHEME katika Banda la PPF Viwanja vya Nane Nane Ngongo Kama Picha Inavyoonekana Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel na Afisa Masoko PPF, Wakitoa maelekezo ya Jinsi ya Kujaza Fomu Hizo
PPF Nane nane 2016 -4
Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel akimkabidhi kadi ya WOTE SCHEME kwa mwananchi aliyejiunga na Mfuko huo.


Mfuko wa Pensheni wa PPF upo katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi katika Maonesho ya Nane nane ili Kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya Mfumo wa WOTE SCHEME kwa Sekta Binafsi kama Vile Wakulima,Wafugaji, Mama Lishe, Madereva Bodaboda na Wajasilamali mbalimbali ili waweze kujiwekea Akiba wakati huohuo wakinufaika na Bima ya Afya, Mikopo kwa Ajili ya Kujiendeleza Kielimu, Kuongeza Mtaji na Kunufaika na Pensheni za kila Mwezi.

Akiongea na Lindiyetu.com 
Bi Janeth ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutembelea Banda hilo la PPF kwa ajili kupata elimu na kujiunga na mfuko huo na kufaidika na fursa zinazotolewa na PPF.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.
  Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo kwa wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.
  Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III katika kijiji cha Mwamgoba Wilayani Busega, wakiwasikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na katibu tawala Jumanne Sagini (hawapo pichani), walipozungumza nao kabla ya zoezi la uhawilishaji wa fedha za ruzuku kwa ajili ya mpango huo.
  Bw. Methesela Mrobi akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya(hawapo pichani) Bwawa dogo alilochimba kwa kutumia fedha za ruzuku za Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III, ambalo analitumia kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji
   Mkuu wa Wilaya ya Busega , Mhe. Tano Mwera (katikati) na Katibu Tawala Wilaya ya Busega, Bw. Sebastian Masanja (kulia) wakizungumza jambo kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijiji cha Mwamgoba, Wilayani Busega  (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akimkabidhi fedha Bw. Methesela Mrobi wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III ,katika kijiji cha Mwamgoba, Wilaya ya Busega Mkoani humo. 
 
                Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkoa wa Simiyu)
Mkuu wa  mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kata na vijiji kuwabaini wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya TASAF III(PSSN) wanaojihusisha na ulevi na kuwaondoa katika orodha ya wanufaika wa mpango huo.
Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega katika zoezi la uhawilishaji fedha za TASAF III PSSN, ambapo jumla ya shilingi 2,976,000 zimegawiwa kwa wanufaika 82 kijijini hapo.
Mtaka amesema lengo la mpango wa TASAF III ni kuwatoa watanzania katika hali ya umaskini kwa kuwapa ruzuku itakayowasadia kupata huduma muhimu ikiwa ni pamoja huduma za afya, kuwasaidia watoto wao waweze kwenda shule lakini baadhi ya wanufaika wamekuwa wakitumia fedha hizo kulewa badala ya kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku, mbuzi na kondoo pamoja na kilimo ili miradi hiyo iwasaidie kuwaongezea kipato.
“Hatuwezi kuleta fedha  tukifikiri zitawasaidia kujikwamua katika Umaskini lakini mnashinda baa na vilabuni kulewa , wengine mnaongeza wake, tukiwabaini mtaondolewa kwenye huu mpango” , alisema Mtaka.
Mtaka amewataka wanufaika hao kujishugulisha na kilimo na ufugaji na kuondokana na dhana ya  kuwa watakuwa wanufaika wa mpango huo siku zote, ambapo alieleza azma ya  Serikali ya awamu ya tano ya kuwatoa wananchi katika umaskini na kuwaondolea changamoto mbalimbali kama kutoa elimu ya bila malipo na kuanzisha Mfuko wa Huduma ya Afya Watanzania wasio na uwezo waweze kupata matibabu kwa gharama nafuu  na akatoa wito kwa wanufaika hao kujiunga na Mfuko wa Huduma ya Afya ya Jamii (CHF)ambao utawasaidia wao wenyewe pamoja na wategemezi wao kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea huduma za Afya.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi kuwakumbusha watoto wao wajibu wa kuwatunza kwa sababu kumekuwa na baadhi ya wazee ambao wametambuliwa kuwa ni maskini, wakati wana watoto wenye nguvu na uwezo wa kuwasaidia lakini hawatimizi wajibu wao kuwatunza kwa kuwapa mahitaji muhimu.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo Bibi. Christina Robert ambaye ni mnufaika wa mpango wa TASAF amesema mpango huo umemsaidia kuondokana na kuishi katika nyumba ya nyasi na matope na kumuwezesha kujenga nyumba ya matofali na bati.
“Naishukuru TASAF maana imenisaidia sana, ruzuku niliyopewa mara ya kwanza ilinisaidia kutibiwa nilipofanyiwa upasuaji, mara ya pili nilitumia tena kwenye matibabu, mara ya tatu nilinunua kuku na bata, mara ya nne  nikanunua bati nikajenga nyumba ya vyumba viwili”, alisema Christina.
Pamoja na kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya fedha za ruzuku za TASAF Mtaka amewataka wananchi wa Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuongeza juhudi katika kilimo cha mazao ya mikunde kwa kuwa tayari Serikali ya India imekubali kununua zaidi ya tani milioni sita ya choroko, dengu na mbaazi kutoka Tanzania,  hivyo wakati utekelezaji wa makubaliano hayo utakapoanza wananchi walime kwa wingi mazao hayo kwa kuwa kutakuwa na soko la uhakika.
Jumla ya kaya 4260 zilibainishwa katika vijiji 41 vya wilaya ya Busega ambapo kaya 53 ziliondolewa katika mpango wa TASAF III PSSN baada ya uhakiki na kubaini kuwa hazikukidhi vigezo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Lindi mchana huu akitokea mkoa wa Dar es Salaam kwa njia ya barabara ambapo hapo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha   Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa kwenye viwanja wa Ngongo katika Manispaa ya Lindi.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya Nane nane hapo kesho kwa  niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli.

Alipowasili ikulu ndogo mjini Lindi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa LINDI Godfrey Zambi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa.


Katika Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo, Maliasili na Uvuvi wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid.




STAMICO YAWATANGAZIA NEEMA WACHIMBAJI WA MADINI TANZANIA

Katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika na kazi zao na kuepuka kuondolewa na wachimbaji wakubwa wameshauriwa kuchukua leseni ndogo za awali za uchimbaji.
STAMICO Nane nane 2016 -1
Kaimu Mkurugenzi wa utafiti na Uchimbaji wa Shirika la Madini (STAMICO) Alex Rutagwelela (Katikati) akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Nane nane Viwanya vya Ngongo - Lindi.

Wito huo kwa wachimbaji umetolewa na kaimu mkurugenzi wa utafiti na uchimbaji wa shirika la madini (STAMICO) Alex Rutagwelela alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ngongo Manispaa ya Lindi yanapofanyika maonyesho ya nane nane kitaifa.

Rutagwelela alisema wachimbaji wadogo wanatakiwa kuwa na leseni za awali zitakazowafanya wawe na haki kwenye maeneo wanayochimba. hivyo kuwa na uhakika wa kuto ondolewa bila taratibu na wachimbaji wakubwa kwenye maeneo wanayochimba.
STAMICO Nane nane 2016 -2
Wananchi wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Maafisa wa STAMICO walipotembelea Banda lao katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.

Aliwahakikishia wanahabari na wananchi shirika hilo linania ya kuwainua wachimbaji wadogo kwa kufanyia tathimini maeneo wanayochimba ili waweze kujua kiasi cha madini na mashapo yaliyopo katika maeneo hayo.

Katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika na kazi zao na kuepuka kuondolewa na wachimbaji wakubwa wameshauriwa kuchukua leseni ndogo za awali za uchimbaji.
STAMICO Nane nane 2016 -1
Kaimu Mkurugenzi wa utafiti na Uchimbaji wa Shirika la Madini (STAMICO) Alex Rutagwelela (Katikati) akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Nane nane Viwanya vya Ngongo - Lindi.

Wito huo kwa wachimbaji umetolewa na kaimu mkurugenzi wa utafiti na uchimbaji wa shirika la madini (STAMICO) Alex Rutagwelela alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ngongo Manispaa ya Lindi yanapofanyika maonyesho ya nane nane kitaifa.

Rutagwelela alisema wachimbaji wadogo wanatakiwa kuwa na leseni za awali zitakazowafanya wawe na haki kwenye maeneo wanayochimba. hivyo kuwa na uhakika wa kuto ondolewa bila taratibu na wachimbaji wakubwa kwenye maeneo wanayochimba.
STAMICO Nane nane 2016 -2
Wananchi wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Maafisa wa STAMICO walipotembelea Banda lao katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.

Aliwahakikishia wanahabari na wananchi shirika hilo linania ya kuwainua wachimbaji wadogo kwa kufanyia tathimini maeneo wanayochimba ili waweze kujua kiasi cha madini na mashapo yaliyopo katika maeneo hayo.

MSHINDI WA AIRTEL TRACE MUSIC STAR 2015 AZUNGUMZA NA VIJANA JIJINI MWANZA. PIA KUDONDOSHA BURUDANI USIKU HUU.


Star wa Airtel Trace Music 2015, Mayunga Andrew Nalimi-MAYUNGA, akizungumza na #BMG kuhusiana na project yake ambayo anaifanya na star M-Rap.
Na George Binagi-GB Pazzo

Project inaitwa Across Lovers and Friend Music Tour ambayo Mayunga anaitumia kukutana na mashabiki zake na kuwapa burudani ikizingatiwa tangu atoke Marekani hakuwahi kufanya tour kama hiyo kwa ajili ya mashabiki zake.

Mayunga amesema Project hiyo imeanzia Mwanza na itaendelea katika mikoa mingine na hata nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda, Malawi na Afrika Kusini.
Usiku huu anapiga show Jembe Beach Jijini Mwanza.

Awali Mayunga pamoja na M-Rap kwa kushirikiana na Star Foundation na Kwanza Online na timu nzima ya Trace Music, waliweza kukutana na vijana Jijini Mwanza kwa ajili ya kuzungumza nao kuwahamasisha kutumia vipaji vyao ili kujikwamua kimaisha.
Mayunga akizungumza na BMG
Stella Mutta ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Star Foundation ya Jijini Mwanza, akizungumza na BMG
Petro Malongo ambaye ni mmoja wa Vijana waliohudhuria Inspiration Event ya hii leo
Mkurugenzi wa Star Foundation akizungumza na Vijana Jijini Mwanza
Mmoja wa viongozi wa Star Foundation akizungumza na Vijana Jijini Mwanza
Baadhi ya Viajana Jijini Mwanza waliohudhuria event hiyo
Mkurugenzi wa Star Foundation
Mayunga (Kushoto) na M-Rap (Kulia)
Vijana katika picha ya pamoja
Picha ya pamoja
GB (L) with Mayunga (R).
Bonyeza HAPA Kusikiliza Mahojiano. Au bonyeza Play hapo chini


Mcheza sarakasi wa Marekani, Simone Biles anatarajiwa kuiletea medali ya dhahabu nchi yake kwenye mashindano ya 31 ya Olympic ya Rio, 2016. Mashindano hayo ambayo yamevuta wanamichezo kutoka kila pembe ya Dunia, yamezinduliwa usiku wa uamkia leo Agosti 6, 2016 kwenye uwanja wa michezo wa Maracana mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil kwa kurushwa fashifashi angani. Rais wa Mpito wa nchi hiyo, Michel Temer alitangaza kuanza kwa mashindano hayo ambapo Tanzania nayo inawakilishwa.

 Fashifashi (fataki), zikihanikiza anga la uwanja mkubwa kabisa nchini Brazil, Maracana wakati wa uzinduzi huo
Mwanamitindo wa Brazil, Gisele Bundchen
 Rais wa Mpito wa nchi hiyo, Michel Temer
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) na Mbunge wa Kisarawe jijini Dar es Salaam, Jaffo Suleiman Said, (katikati), akipokewa na Mkuu wa Wizalay ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu, wakati akiwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya Wakulima Nane Nane, Nzuguni mkoani Dodoma Agosti 6, 2016. Maonyesho hayo ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Lindi, huwapa fursa wakulima kuonyesha sjughuli zao za kilimo na ufugaji pamoja na zana za kilimo yatafikia kilele Agosti 8, 2016

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jafo Suleiman Said akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa maonesho ya nane nane Nzuguni mjini Dododma


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jafo Suleiman Said Jafo akisikiliza kwa makini maelezo ya kilimo cha mbogamboga yanayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jafo Suleiman Said Jafo akisikiliza kwa makini maelezo ya kilimo cha mbogamboga yanayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jafo Suleiman Said Jafo *watatu kushoto), akizungumza na Luteni AJ Massawe Meneja wa banda la JKT


Naibu Waziri akipokea zawadi ya mafuta ya alizeti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi

Naibu Waziri katika picha ya pamoja na
na Mkuu wa Wilaya ya ikungi na Kongwa pamoja na watendaji Mfuko wa LAPF

DAS ILALA, EDWARD MPOGOLO AZINDUA KITABU CHA BAJETI, AKATA KEKI KUNOGESHA MIAKA 16 YA TAASISI YA VIJANA YA TYVA, AWAASA KUANDAA MIPANGO INAYORANDANA NA YA SERIKALI


OfisaTawala wa wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo, akiwahutubia Vijana waalikuwa na wanachama wa Taasisi ya Vijana ya TYVA, wakati wa hafla maalum ya maadhimisho ya miaka 16 ya Taasisi hiyo, iliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam. 

Na Bashir Nkoromo

Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, pamoja na mambo mengine, Mpogolo amewaasa Vijana wa Taasisi ya Vijana ya TYVA kuhakikisha mipango yao ya kushirikisha Vijana katika shughuli za kimaendeleo, inaendana na mipango ya serikali ili kuwezesha utekelezwaji usiokinzana.

Amesema, iwapo TYVA itapanga kwenye malengo yao mipango inayotofautiana na ile ya serikali kuhusu maendeleo ya vijana na mengineyo, basi utekelezwaji wake unaweza kuwa siyo rahisi kutokana na kukinzana kwa kuwa malengo ya serikali yatakuwa yanaelekeza vingine wakati na wao wamelenga vingine.


Pia aliwataka vijana wa TYVA na wengine kote nchini kuhakikisha wanailinda amani ya Tanzania kwa gharama na nguvu zao zote, akitahadharisha kwamba, amani ni tunu ambayo ikishapotea si rahisi kurejeshwa.


Ameitaka TYVA na Taasisi ngingine za Vijana popote zilipo, kuhakikisha wanakuwa makini dhidi ya watu wasioitakia mema Tanzania, akisema, wapo ndani na nje ya nchi ambao hutamani sana kuona amani ya Tanzania inapotea au inatetereka kwa namna yoyote, na kibaya zaidi kujaribu kujipenyeza kwa makundi ya vijana ili kufanikisha azima zao mbaya.


"Kitu kingine ninacho waasa wakati Taasisi yenu ya TYVA inatimiza miaka 16 sasa, waelimisheni vijana wenzangu, wajihadhari sana, wasije kutekwa na watu waliopo ndani na nje ya Tanzania ili kuwatumia kuharibu amani ya nchi yetu", alisema Mpogolo.


Baadaye Mpogolo alizindua Kitabu cha Mipangokazi au bajeti ya Taasisi hiyo na kukata keki  kushiria TYVA kutimiza miaka 16 tangu ilipoanzishwa na kuendelea kwa mafanikio kufanya kazi zake katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa.



 OfisaTawala Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo akizindua mpangokazi au bajeti ya Taasisi ya Vijana ya TYVA, wakati wa maaldhimisho ya miaka 16 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council Dar es Salaa.. Kushoto ni Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshale
 Vijana wakiwa wamenyoosha miko yao wakati Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (aliyesimama) alipokuwa akiwapiga tafakuri kuhusu umuhimu wa Amani ya Tanzania, alipozungumza nao wakati wa maadhimisho ya miaka 16 ya TYVA yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam. 
 Mhasibu Mkuu wa TYVA Zuleikha Ibrahim, akiwasilisha keki meza kuu kwa ajili ya mgeni rasmi, Osisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kulia) kuikata, kunogesha maadhimisho ya miaka 16 ya TYVA yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam. 
 Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akikata keki kunogesha maadhimisho ya miaka 16 ya Taasisi ya Vijana ya TYVA, yaliyofanyika katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam, leo. Kulia ni Ofisa Vijana mkoa wa Dar es Salaam, Masalida Sephania Njashi na kushoto ni Mhasibu Mkuu TYVA Zukeikha Ibrahim, na wapili ni Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare
 Keki baada ya kukatwa 
 Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare akimlisha keki Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo wakati wa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare akimlisha keki Ofisa Vijana Dar es Salaam, Masalida Njashi wakati wa hafla hiyo
 Mpogolo akimlisha keki Mwenyekiti wa TYVA wakati wa hafla hiyo. 
 Mpogolo akimlisha keki Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi ya TYVA, Makwita Abdul wakati wa hafla hiyo
 Mpogolo akimlisha keki Mhasibu Mkuu TYVA Zukeikha Ibrahim wakati wa hafla hiyo 
Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Vijana ya TYVA  mwishoni mwa hafla ya TYVA kutimiza miaka 16 tangu kuanzishwa kwake



Geline Fuko (kushoto) akipokea maua kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),ikiwa ni ishara ya kumpongeza baada ya kutua  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana, akitokea Marekani alikokuwa akihudhuria mafunzo ya vijana wa kiafrika yaliyoandaliwa na

Raisi Obama.


Na Dotto Mwaibale

SHANGWE ilitawala wakati mtanzania Geline Fuko alipo wasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa nne usiku jana Agosti 5, 2016 akitokea nchini Marekani alikohudhuria mafunzo ya viongozi vijana kutoka Bara la Afrika. 

Wafanyakaziwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao ni wafanyakazi wenzake wa Geline, familia ya Geline, ndugu na marafiki walitoa mapokezi ya kishujaa wa wanaharakati huyo aliyetajwa kuwa mfano wa kuigwa na Rais Obama.


Akizungumza na wanahabari, Geline alisema amefarijika na hakutarajia kama wazo lake la kuanzishwa kwa Kanzidata ya Katiba litakuwa wazo kubwa  ambalolitakubalika mpaka na Rais Obama. 

Hata hivyo Geline alisema amefurahishwa na program hiyo ya Mandela Washington Fellowship kwani imewawezesha washiri kikujifunza mambo mengi na  kupata uono mpana zaidi wakufanya mambo.

Geline iliwahimiza watanzania kutembelea Kanzidata hiyo iliyopo mtandaoni (http://katiba.humanrights.or.tz/) ili kuweza kuijua katiba yao na kuweza kujua haki zao kama watanzania. 

Mwisho alishukuru wa mapokezi makubwa ambayo pia hakuyatarajia.

Akitoa neno la shukurani kwa Geline kwa niaba ya LHRC, Mkurugenzi wa Fedha naUtawala-LHRC, Ezekiel Masanja amempongeza Geline kwa kuitoa kimasomaso LHRC na Tanzania kwa ujumla.

Geline Fuko amepata kutambulika baada ya Rais Obama kumtaja kama mfano wa kuigwa wa wanaharakati wa haki za binadamu wakati akizungumza Jumatano Agosti 3, 2016 katika kilele cha mpango wake wa kuwawezesha vijana wakiafrika unaojulikana kama Mandela Washington Fellowship. 

Raisi Obama alimsifu mwanasheria huyo kutoka LHRC ambaye ni moja  ya vijana 1000 waliokuwa jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo ili kuweza kusaidia Maendeleo katika Nyanja zote za maisha katika nchi zao.

RaisiObamaalisifujuhudizaGelinezakuibuawazo la kuanzishakwamaraya kwanza Kanzidata ya Katiba nchini Tanzania kwa kutekeleza wazo hilo chiniya LHRC. 

Raisi Obama alikaririwa akisema Marekani itaendelea kushikamana na wanaharakati kama Geline Fuko kutoka Tanzania. 

GelinenimwanasherianamwanaharakatiwahakizabinadamuambayeamefanikishakuanzishwakwaKanzidatayaKatibaya kwanza nayapekeenchini Tanzania inayowawezesha watanzania kusoma Katiba kupitia simu zao za mkononi”.

Programu ya Mandela Washington Fellowship yenye lengo la kuwa wezesha vijana wa Kiafrika katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia na kijamii ilianzishwa na Rais Obama mwaka 2014. 

Programu hii hujumuisha vijana elfu moja (1000) kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao hugharamiwa na serikali ya Marekani kwenda jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo zaidi.


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzisha Kanzidata ya Katiba mwaka mmoja uliopita mnamo Julai 15, 2015. 

Kupitia tovuti maalumu (http://katiba.humanrights.or.tz/) na simu za mkononi, watanzania wanaweza kusoma Katiba katika Kanzidata hiyo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akikagua vijana wa mafunzo ya Mgambo kutoka vijiji vitano vya Dung’unyi, Munkinya, Kipumbuiko, Samaka na Damankiya vinavyounda Kata ya Dung’unyi katika Tarafa ya Ikungi
 Kundi la vijana wa Mgambo kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakionyesha umahiri wao katika mafunzo waliyoyapata mbele ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Ikungi
 Kundi la vijana wa Mgambo kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akijadili jambo na Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi Fortunatus Ndalama
Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturua akizungumza na watendaji Kata, na viongozi wa vijiji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya mgambo yatakayodumu kwa wiki 16

 Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Udalai ya Yono Auction Mart na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bibi. Scholastica Kevela wakiwa wameshika Tuzo na Cheti walivyopewa kutokana na kutoa huduma kwa viwango na ufanisi.Tuzo hiyo inajulikana kwa jina la The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence) imetolewa tarehe 25, Julai 2016 Jijini Rome Italia na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa.
 Mwenyekiti wa Yono Auction Mart & Co Ltd Bw. Stanley Kivela akielezea jambo kuhusu Tuzo ya Almas ya Ubora, Uwajibikaji na Ufanisi (The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence) iliyotolewa na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa ambapo takribani nchi 49 dunia zilishiriki mchakato huo huku Tanzania ikiwakilishwa na taasisi mbili ambazo ni Mamlaka ya Angaa (TCAA) kwa upande wa Serikali  na Yono Auction Mart kwa upande wa Sekta binafsi
 Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart Bibi. Scholastica Kevela akiwa ameshika Tuzo waliyopewa kutokana na kutoa huduma kwa viwango na ufanisi.Tuzo hiyo inajulikana kwa jina la The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence imetolewa tarehe 25, Julai 2016 Jijini Rome Italia na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa.

Na Frank Shija, MAELEZO.
Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imeendelea  kuungwa mkono na wadau mbalimbali kutokana na jitihada zake za kurejesha heshima na uadilifu miongoni mwa jamii ya Watanzania.
Haya yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya  Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd Bw. Stanley J. Kevela aliokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tuzo iliyopata leo Jijini Dar es Salaam.
Kevela ameseme kuwa wao binafsi kama kampuni inayoaminiwa na Serikali na taasisi zake wanayosababu ya kuunga jitihada zinazoonyeshwa na Serikali katika kupigania maendeleo ya watu wake kwa kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, ubunifu na ufanisi unaostahili.
“Tunatoa Tuzo hii muhimu kwetu kwa Mhe. Dkt. Magufuli kama ishara ya kuheshimu mchango wake katika kuliletea taifa letu maendeleo  na kuhakikisha mambo yanafanywa kwa ufanisi na  viwango vyenye ubora wa hali ya juu”. Alisema Kavela.
Amesema kuwa tokea Rais Magufuli aingie madarakani mambo mengi yamekuwa yakienda vizuri hivyo ikiwemo suala la ukusanyaji wa Kodi kazi ambayo wamekuwa wakiisaidia Serikali kwa muda mrefu sasa.
Aliongeza kuwa Kampuni yake imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma zenye viwango tena kwa uadilifu na uwajibikaji usiotiliwa shaka ndiyo maana wanamuunga mkono Mhe. Rais kwakuwa naye ni muunini wa falsafa ya uwajibikaji, uadilifu na ubunifu.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa katika kuendeleza jitahada za Serikali katika kukuza ajira wameajiri zaidi ya vijana 200 ambao wako mtaani wakifanya kazi ya ukusanyaji wa Kodi kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Marts &Co Ltd Bibi. Scholastica Kevela ametoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kuiamini Kampuni hiyo kwa kupata huduma zao zikiwemo wakala wa Udalali wa Mahakama na Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali kwa niaba ya TRA.
Yono Auction Mart imekuwa ikifanya kazi na Serikali katika Nyanja mbalimba ikiwemo ukusanyaji wa Kodi kwa niaba ya TRA, udalali wa Mahakama, Uuzaji wa viwanja vya Serikali na mambio mengine yanayohusu ukusanyaji wa Kodi za Serikali.
Kampuni ya Yono Auction Marts &Co Ltd ilipata fursa ya kushiriki katika hafla ya ugawaji wa Tuzo za Diamondo Eye kutokana na Ubora, Uwajibikaji na Ufanisi (The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence) iliyotolewa tarehe 25 Julai 2016 Jijini Rome, Italy iliyotolewa na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa ambapo takribani nchi 49 dunia zilishiriki mchakato huo huku Tanzania ikiwakilishwa na taasisi mbili ambazo ni Mamlaka ya Angaa (TCAA) kwa upande wa Serikali  na Yono Auction Mart kwa upande wa Sekta binafsi.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, wakati akiingia mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Agosti 5, 2016. Mbunge huyo, ameachiwa kwa dhamana na Mahakama hiyo kufuatia kesi inayomkabili ya uchochezi.
Kesi yake imeahirishwa hadi Agosti 19, 2016.
OFISI za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge, jijini Dar es Salaam zitakuwa wazi kwa siku mbili, Jumamosi, Agosti 6, 2016 na Jumapili, Agosti 7, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri ili kutoa fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha mikopo kupata taarifa kuhusu madeni yao.
Bodi ya Mikopo imeshaanza kuwachukulia hatua wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kwa kutangaza majina yao katika vyombo vya habari. Hatua zingine zitakazochukuliwa ni pamoja na:
i.              Kufikishwa mahakamani;
ii.             Kutozwa faini;
iii.            Kunyimwa fursa za kupata mikopo;
iv.           Kunyimwa fursa za masomo nje ya nchi; na
v.            Kuzuiwa kusafiri nje ya nchi.
Nyote mnakaribishwa ili kutumia fursa hii muhimu.
Imetolewa na:
Bw. Jerry Sabi,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
S.L.P. 76068,
DAR ES SALAAM
Baruapepe: info@heslb.go.tz

‘Kuwa Mzalendo, Rejesha Mkopo wa Elimu ya Juu’

Kutoka Kushoto ni Eng Sadick Chakka Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga, na Kulia ni Abel Suri Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

Jeshi la polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida limemtia nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Emmanuely Njingu kwa kosa la kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali kufanya kazi yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha awali kabla ya kuwekwa nguvuni na jeshi la polisi alivuliwa ujumbe wa kamati hiyo kutokana na kukiuka taratibu na makubaliano ya baraza la madiwani jambo ambalo limepelekea kuhamishiwa katikakamati nyingine.
Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa diwani huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Irisia Ally Juma Mwanga amesema kuwa Diwani huyo amekamatwa kwa mujibu wa sheria hivyo yeye kama mwenyekiti hawezi kuingilia taratibu, sheria,na kanuni za serikali.
Mwanga amesema kuwa tarehe 19 mwezi Julai moja ya maadhimio ya kamati ya fedha na vikao vya baraza ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri lakini diwani huyo amekiuka makubaliano hayo kwa kung’oa mageti ya vizuizi vya barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa mazao jambo ambalo limepelekea kuzorota kwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Ameongeza kuwa Mjumbe yeyote anayekiuka maazimio wanayokubaliana na kutoa siri za kamati adhabu yake kisheriani kupoteza sifa ya kuwa mjumbe wa kamati husika.
Amesema diwani huyo ameondoshwa katika nafasi hiyo baada ya maridhiano ya kamati hiyo na kukubaliana kumuhamishia katika kamati nyingine ya huduma za uchumi.
“Jambo mkishakubaliana kisheria tena kwenye vikao vya kisheria maana yake linakuwa ni sheria hivyo kwa kiongozi yeyote akikiuka taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake, kanuni za Halmashauri ni za watu wote hazichagui upande mmoja” Alisema Mwanga
Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alihutubia Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mara yake ya mwanzo kabisa tangu alipochaguliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na kuzungumzia kuwepo kwa changemoto ya uhaba wa maabara, afya duni na miundombinu pia alizungumzia kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato jambo ambalo linairudisha nyuma Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Bajeti ya Wilaya ya Ikungi kwa Mwaka 2013/2014 ilikuwa na Shilingi 509,701,044 namakusanyoyakeyakawa ni 338,325,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kuwa na upungufuwa shilingi 171,376,044.
Mwaka 2014/2015 ilipangwa bajeti ya shilingi 631,455,000 lakini makusanyo yake yakawa ni shilingi 457,555,172 ambapo mwaka ulimalizika kwa kukusanya 173,899,828.
Mwaka wa bajeti 2015/2016 bajeti ya Halmashauri iliyopangwa ilikuwa ni shilingi 1,127,030,000 makusanyo yalikuwa ni 679,283,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kwa kuwa na upungufu wa shilingi 450,747,000 hivyo kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji.
Mwanga amesema kuwa Kutofikiwa malengo hayo kumesababishwa na kutopewa ushirikiano watendaji katika ukusanyaji wa mapato hii ikiwa ni kufuatia kauli za mazuio zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.
Hata hivyo ametoa Mwito kwa viongozi wa serikali, wanasiasa, taasisi za dini na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo ya kuifanya Ikungi kukua kiuchumi . 

No comments :

Post a Comment